ABEL NESTORY
Member
- Oct 12, 2012
- 44
- 34
Habari ndugu zangu, naitwa Abel ni mvulana wa umri wa miaka 28. Nahitaji msaada wenu Tafadhali maana kwa kupitia humu nitaweza kupata hata nafuu maana akili yangu mawazo yangu nahisi yananifanya nakata tamaa japo naamin ninaweza. Nilimaliza Kidato cha nne 2008 na kupata daraja la kwanza (division one) na baadae form six 2012 ambapo sikufanya vzuri (nilipata division 3) kwakuwa kuna shida ilijitokeza na pia nahisi ilichangiwa na kuchagua mchepuo (combination) ambao haukuwa sahihi kwangu. Hapa ninamaanisha kuchagua masomo ambayo sikuwa nayapenda japo nlikuwa nikiyafaulu vizuri, hii ilitokana na ushawishi wa rafiki na kufuata mkumbo wa marafiki. Kwa kuambiwa nikisoma Sayansi ni miaka mingi chuoni, nitaweza kuwa na akili zisizovizuri, mchafu nk, Nikajikuta nasoma (EGM) ambyo ckuwa nmewahi hata kuiwaza maishani. Tangu nilipokuwa Kidato Cha kwanza/ form one nilipenda sana masomo ya PHYSICS, MATHEMATICS, CHEMISTRY na BIOLOGY na nilikuwa nikifaulu kwa alama za juu sana. Ufaulu wangu ulikuwa
Mathematics- B
Chemistry- B
Physics- B
Biology-B
na C kwa masomo yaliyobaki, Kiukweli mpaka sasa nayapenda toka moyoni na naamini ninaweza kufanya maajabu nikipata nafasi. Natamani sana kurudia kufanya mtihani wa Form six kwa PCM au PCB maana naamini ninaweza. Nilipojarbu kuomba ushauri niliambiwa naweza kusoma Diploma katika vyuo vya udaktari ORDINARY DIPLOMA Katika CLINICAL MEDICINE nk kwa kutumia vyeti vya form four. Pia licha ya mambo ya Sayansi napenda sana ufundi. Natamani sana kutimiza ndoto zangu ninaamini na hilo, pia Mungu anisaidie kwa hili. Ninaandika hii post nikijisikia amani maana nahisi kuna kitu nimekipata humu na nimetua mzigo fulani. Nitashukuruni sana ndugu zangu. Kwasasa ninafanya kazi katika kiwanda fulani na vitu vnavyotokea vinanifanya najuta sana kama unavyoelewa kazi za watu.
OMBI LANGU kwa wadau na ndugu zangu humu. Ninahtaji na ninaomba kufahamu yafuatayo
1/ Je kuna uwezekano wa kupata mtu wa kunisiadia kunisomesha???
2/ Je nawezaje kupata wafadhili kama kuna uwezekano huo??
3/ Nahitaji msaada zaidi wa mawazo maana nawaza sana nmeharibu mwelekeo wa maisha yangu na ndoto zangu. Inafikia kipindi sihitaji kuonana na mtu yeyote niliyesoma naye awali kitu ambacho nahisi ni tatzo la kisaikolojia.
Msaada please hata kwa mawazo mengine ya kunijenga na ushauri ili nitulie na kupata njia sahihi ambayo naamini nitaitendea haki. Mbarikiwe wote na kazi njema na masomo mema kwa wanafunzi.
NDUGU ZANGU, TUWE MAKINI KATIKA KUFANYA MAAMUZI ILI TUSIJE TUKAJUTA KAMA MIMI.