Nimeanza kupata marafiki wapya wanaojielewa kutoka huko duniani.

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,446
40,432
Nilianza kimzaa mzaa, nikaanza kujiunga kwenye magrupu ya wafanya biashara, wajasiriamali, wanaofanya fedha za kimtandao n.k kutoka huko duniani.

Nimekuwa namwaga nondo nzito, za kibiashara za kimataifa na namna ya kufanya uwekezaji wa hapa na pale popote duniani n.k

Nimejikuta napata marafiki wengi kutoka Canada, Marekani, Uingereza, Romania, India, Pakistani, Bangladeshi, Norway n.k, na wote tunashea mawazo ya kibiashara na namna ya kufanya uwekezaji mdogo mdogo na mkubwa.

Kuna mwingine ameanzisha kampuni yake huko Ulaya, lakini bado iko changa ila amekuja kuniomba ushauri wa namna ya kufikisha malengo yake huko mbeleni.

Nimejikuta nacheka mwenyewe na kusema kimoyo moyo, kumbe sikuchezea hela ya ada ya wazazi wangu.

Vijana tuchangamke, tuachane na marafiki wa mazoea mazoea; tutafute marafiki wenye tija huko duniani, muhimu lugha iwe inapanda tu, na pia 'argument' zako ziwe zakisomi zenye 'standard' zinazotambulika kimataifa.

Leo ni hayo tu; mwenye akili apambane.​
 
Hongera sana
 
Asante sana kwa ushauri huu muhimu kaka. Wewe Binafsi kuna Biashara unafanya au umejikita kwenye kutoa ushauri kwa hao marafiki wa nchi za nje tu?

Na kama jibu ni ndiyo na unaona Biashara hiyo inakupa faida, siyo mbaya ukitushirikisha katika Biashara hiyo. Itatupa msaada zaidi.
Kama una ujuzi wa 2d animation, njoo tupige kazi; ndani ya miaka mitatu tu utakuwa unakweya mwewe kwenda kwenye 'branches' huko nje.
 
Asante sana kwa ushauri huu muhimu kaka. Wewe Binafsi kuna Biashara unafanya au umejikita kwenye kutoa ushauri kwa hao marafiki wa nchi za nje tu?

Na kama jibu ni ndiyo na unaona Biashara hiyo inakupa faida, siyo mbaya ukitushirikisha katika Biashara hiyo. Itatupa msaada zaidi.
Huyu atakuwa fresh graduates ndio anaanza kupambana na social media groups kisha anajiona mjanjaa kuchat na Matapeli.

Mkuu nipo katika group za watu wa nje mbali mbalimbali hasa hizi za trades n.k ila ukweli mle 90% ni matapeli (scammers), kama kuombwa ushauri kwenye group za aina hiyo inaonekana mtu una akili basi ningejuwa ninazo nyingi zaidi.

Umezaliwa Kiziramimba Kule Kigoma, utashaurije ufanyaji biashara nchini Uingereza ilihal hata Uingereza hujawahi kufika.

Mkuu mode yao za biashara tofauti na sisi kule wako more formal na contracts.

Labda nisiseme mengi niishie kusema tu chat nao ila kuwa makini mtakapofika hatua ya kuitwa ukafanye kazi kwao, (kwenye hizo kampuni) wakisema tuma documents zako we tuma, ila ukisikia wanakuambia lipia document fulani tuifanyie kazi hapa, shtuka usitume hela yako ndio hatua ya kuliwa.

Kwa maisha yalivyo sasa huwa nashangaa watu wa zaman walifanikiwaje kukutana na watu online waka match successfully kwa sababu saivi mtandaoni ni full scammers
 
Muhimu kwanza wewe mwenyewe uwe na kampuni, na unavyochat nao hakikisha na wao wana kampuni, na ikitokea mnataka mfanye kazi pamoja in 'form of partnership', kuna 'MoU'; itategemea uelewa wako wa kibiashara ukoje; kama uko chini kimataifa, endelea kushughulika na hawa wa ndani tu (local).​
 
Back
Top Bottom