Nimeamua Kuwa Machinga, Degree nimeiweka Mfukoni Kwanza

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,303
23,055
Hakuna namna, hakuna kuremba. Nimeamua kuwa Chinga, ninauza raba za mtumba na sendo. Kwasiku nalaza net 10000-30000 baada ya kuondoa matumizi yangu.
Sina mke, sina mtoto.

Ni kazi tu, ukija na degree mtaani maisha ni magumu. Jamaa yangu nae anapiga bodaboda.
Mpango ni Malengo.
Tupige kazi wakuu, kazi ni Kazi.

Usiifikirie sana elimu uliyonayo, utaozea nyumbani.
 
Digrii pia unaitumia. Maarifa uliyoyapata mpaka kiwango cha digrii yanakusaidia kufanya mambo mengine. Ufahamu wako hauwezi kuwa sawa na.layman. digrii ni nyenzo tu. Kuwa makinj na namba unazotoa hapa at a time unaweza kutaka msaada watu wakakuziria. Laki moja mpaka tatu kwa siku bila shaka we ni mfanyabiashara unayekaribia kufanikiwa
Laki gan mkuu mwenzio anazungumzia efu kumi au thelathin
 
Hakuna namna, hakuna kuremba. Nimeamua kuwa Chinga, ninauza raba za mtumba na sendo. Kwasiku nalaza net 10000-30000 baada ya kuondoa matumizi yangu.
Sina mke, sina mtoto.

Ni kazi tu, ukija na degree mtaani maisha ni magumu. Jamaa yangu nae anapiga bodaboda.
Mpango ni Malengo.
Tupige kazi wakuu, kazi ni Kazi.

Usiifikirie sana elimu uliyonayo, utaozea nyumbani.

Hongera hongera sana. Mkuu. MUNGU awe nawe kwa kuchapa kazi.
 
Hongera sana mkuu kwa hatua uliyofikia,hata wafanya biashara wakubwa walianzia hivyo hivyo
 
Mimi nimesubiri teuzi za mweshimiwa, nilivoona kila teuzi zinazofanywa nakosa nikaingia kitaa kuhaso bila kujali elimu yangu na mambo yanaenda, vyeti nimehifadhi
 
Haina maana kuwa ukisoma ndo hupaswi kuafanya kazi hizo mkuu. Elimu yako ndo inatakiwa ionekane sasa kwenye hiyo biashara. Fanya kitu tofauti na wenzako katika kuboresha huduma kwa wateja, namna ya kutafuta masoko etc.
Uzuri wa pesa huwa haisemi ilikopatikana.
 
Hakuna namna, hakuna kuremba. Nimeamua kuwa Chinga, ninauza raba za mtumba na sendo. Kwasiku nalaza net 10000-30000 baada ya kuondoa matumizi yangu.
Sina mke, sina mtoto.

Ni kazi tu, ukija na degree mtaani maisha ni magumu. Jamaa yangu nae anapiga bodaboda.
Mpango ni Malengo.
Tupige kazi wakuu, kazi ni Kazi.

Usiifikirie sana elimu uliyonayo, utaozea nyumbani.
HYO DIGRII YAKO NDO UIFANYIE KAZ KWENYE BIASHARA YAKO, MI SIONI KILICHOHARIBIKA KM KWA MWEZI TAYARI UNA LAKI 9 YAKO PEMBENI,,, AJIRA YA NINI TENA.................
 
Mie nilianza mda kazi ya kuokota makopo. Siku nkaenda kwa usaili wakanihoji maswali uzoefu wako nkawaambia garbage collector officer since 2015. Post niliyoomba ni system analsts. Nahisi yule alikuwa meneja wa uajiri akasema kijana usilete utani wakati unakazi..
Nkamjibu Kazi ninayo ila nimekuja kujikumbusha kingereza nkakusanya vyeti nkasepa. Maana nlfanya udukuzi wanatoa 350000 wakate kodi narudi na nini nyumbani. Wakati mtaani napata nyingi bila kodi wka kugombania daladala.
 
Tatizo la wasomi wa kitanzania hajui namna ya kujiajir
Mnao htaji msaada wangu karibuni!
 
biashara ya kujiajiri ina faida zake na hasara inakuwaje pale mtaji mdogo alafu biashara nayo inaweza kuanza kwa hasara
 
Back
Top Bottom