Nimeamua kuwa Atheist

Sasa wanachosahau ni kwamba imani sio kwa masuala ya dini na Mungu tu, sasa mtu anaposema hataki imani kabisa hunishangaza.
kwa muktadha huo unaosema wewe nadhani ni mambo ya misamiati tu,
 
Wewe ndio unapaswa kujielimisha kuhusu uthibitisho.

Mpaka useme Mungu yupo, ina maana tayari unajua na una uthibitisho wa uwepo wake.

Sasa mkiambiwa mthibitishe Mungu yupo, hamuwezi. Ila mnakataa kwamba hayupo.

Kama unakataa Mungu hayupo na umeshindwa kuthibitisha Mungu yupo, Unataka nini zaidi?
 
Ni nani alikutofautisha kati ya wanyama kama mbwa, mbuzi, ng'ombe na wengineo wasiojua kuchati Wala kutumia sim kama wewe unavochati hadi Kwa kiingereza,

Na hii oxygen unayoivuta inatoka wapi na imeundwa na nani na kwanini iwe tuu hapa duniani na sio kwenye sayari NYINGINE.

Haya maghorofa marefu yanayojengwa na ndege/plane zinazopaa walotengeneza hizo akili walizipata wapi au walipewa na nani
 
Unavyouliza "ni nani..." unajuaje "ni nani..." ndiyo swali husika?

Oxygen inakuwa formed katika photosynthesis. Hujasoma photosynthesis? Na kabla ya hapo chain ya atomic synthesis kwenye supernovae inatengeneza oxygen.Kuna sayari nyingine zina oxygen, Mercury ina oxygen, kuna exoplanets kama HD 209458b ina Oxygen.

Ukiuliza waliojenga maghorofa akili wamepewa na nani unajuaje nani ndiyo swali sahihi?

Hayo maswali yako yote, hata nikisema sijui jibu la hata swali moja, hayathibitishi Mungu yupo.

Maswali yanathibitisha wewe hujui sayansi ya msingi ndiyo maana unaona haja ya Mungu kuwepo.
 
Mungu ambaye anataka kuaminiwa hana tofauti na Demu anayetafuta attention ya kuaminiwa.
mkuu,natoka nje ya mada kidogo

unahisi dini na imani kuhusu Mungu ilikuwa na mchango wowote chanya kwenye maisha yako kabla ya kuacha kuamini katika hayo yote
 
Endelea kusubiri uthibitisho, mimi naendelea kumwamini Mungu.

Nyie endeleeni kusubiri uthibitisho

Kila mtu aendelee na imani yake
 
Sasa unajili vipi kitu ambacho hakipo?
 
Hiyo photosynthesis inayotokana na mimea au jua ni nani alibuni hio mimea au alifanya Hilo jua

Na hizo chain za atomic kwanini zitengeneze oxygen sio carbon dioxide yani nani alizidizaini zitengeneze oxygen

Na hiyo sayansi yote na mpangilio wote kwanini usiwepo kwenye jua au bahari au sayari kama mercury au jupita

Kwanza hiyo sayansi mpaka ikawa sayanzi ilidizainiwa na nani au kivip
 
Endelea kusubiri uthibitisho, mimi naendelea kumwamini Mungu.

Nyie endeleeni kusubiri uthibitisho

Kila mtu aendelee na imani yake
Hawa atheists hawasubiri uthibitisho ndio maana wameshafanya hitimisho kwa kudai hakuna Mungu, ndio maana hata Agnostics wanawashangaa wamewezaje kujua tena kwa uhakika kuwa hakuna huyo Mungu hadi kutoa madai ya kwamba huyo Mungu.
 
Ndio maana nimesema kwa uelewa wako wewe huo ina maana hata mie nikiuwa mtu halafu mahakamani ukakosekana uthibitisho wa kunitia hatiani kwa hiyo kesi ya mauwaji maana yake kwako wewe ni kwamba sijauwa kwa kuwa hakuna uthibitisho badala ya kuwa umekosekana tu uthibitisho wa kunitia hatiani.
 
Nitakuwa mwema hadi kwa Bacteria na virus. Hata nikiumwa sitaki matibabu wala kumeza dawa kwasababu zitaua hawa viumbe ambao nao wana haki ya kuishi.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Mkuu usiwe serious sana usije ukajinyonga.

Ukiachana na kina bacteria 🦠 na virus kuna viumbe hai wengine kama vile nafaka karanga mpunga ngano mahindi maharage miwa etc...(zile ni mbegu ujue na zinaishi ukipanda zikaota zinakua zimeingia ktk phase nyingine ya maisha,

Pia matunda mboga mboga nk.
Sasa unaposema unawaonea huruma inamaana wewe ukatishe maisha yako ili hivyo viumbe viishi... Inabidi uvionee huruma na vyakula vya aina yoyote.

We amini nature tu na uelewe kua katika nature kuna kuishi kwa kutegemeana kikubwa tu nature i-balance (balance of nature (food web &food chain) nature haijali nani kaliwa au nani ana umuhimu sana hapa duniani yenyewe inahakikisha kulaneni kadri muwezavyo ila kusiwe na extinction ya species yoyote.
 
Kwamba unataka kusema kuwa nani aliileta ile BIG BANG kabla haijabanguka,πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ na kuzi-form hizi sayari katika huu ulimwengu.
Kiranga
 
Haikuwa na mchango wowote.

Sanasana ilinipotezea muda kumtegemea Mungu ambaye hayupo.
i don't think so,na imani kwamba the way unawatreat watu uko nje kwenye real life achana na hii life ya JF

80% imetoka katika dini na hofu ya Mungu,pengine utapinga hili kuonesha members hapa how intelligent you are.

pengine sijasoma sana kama wewe na sijui vitu vingi kama wewe lakini i keep learn kila siku.

lakini maisha ya watanzania kwa asilimia kubwa yanafanana

dini zina michango mikubwa sana kwenye malezi yetu pengine you're not ready for this Gumzo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…