Nimeamini kweli mke ni ubavu wa pili

Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,097
2,000
Kwa kweli Mungu ni mwema sana na Namshukuru kwa siku hii ya leo. Imekuwa na changamoto nyingi sana hii siku ya leo ila najua nimezishinda na usiku umeingia hapa ni kwenda kulala tu hakuna purukushani za ziada.

Kwanza kabisa wife kasafiri kaenda kwa wazazi wake, leo nimejikuta niko kwenye mitihani kidogo. Mke wangu amejaliwa kweli kwenye mapishi, huwa akiwepo nyumbani amepika; lazima niwahi nyumani nikapate maakuli. Napenda sana kula mimi na nafurahi sana kumpata mtu mwenye kujua kupika mapishi mengi sana.

Asubuhi imeanza nimeamka na njaa kali sana, imenibidi nikatafute sehemu nipate kifungua kinywa. Kwa kweli kila napoenda ukiangalia mazingira ya upishi na hata sehemu zenyewe kuna mainzi nimeshindwa kula ikabidi ninunue mkate nipike chai ninywe

Ile nimebandika chai nimeweka majani na sukari nikasubri ikachemka ili ninywe. Nilivyokunywa tu chai ilikuwa chungu sana kama mwarobaini. Ikanibidi nipige simu nimulize wife vipi mbona chai chungu majani leo mbona yamekuwa machungu. Akanijibu nitakuwa nimezidisha majani na yeye huwa anaweka vitu vingi zikiwemo mdalasini, iriki na vingine kanitajia sivijui. Kwa njaa ile nilimeza na ile mikate kama nyoka anavyomeza kuku.

Nilipomaliza nikaenda washa moto jiko la mkaa (Jiko Koa). Ule mkaa ulikuwa umelowa na maji. Niliuwasha sana kama saa nzima hivi ndo mkaa ukawaka. Niliwasha na karatasi wapi nikajikuta nimechana daftari la mtoto la shule lote kesho nina kazi ya kwenda kununua jingine. Nikaenda store kwenye makorokoro nitafute tu hata kimfuko cha plastiki, nilipokipata ndio kikawashia moto

Kazi ikaja bhana kuzisukuma, nilisukuma sukuma sukuma kila nikisukuma duara haliji naona linakuja ovyo ovyo. Huwezi amini nilisukuma ile chapati moja nusu saa. Nikasukuma sana mwisho nikaona nipike hivyo hivyo. Ile kuiweka jikoni tu na mafuta wacha niungue lile frampeni lilikuwa la moto sana. Mkono wangu nimeungua karibia vidole vyote, cha kusikitisha ile chapati ya kwanza ikatoka kama ina macho vile inanishangaa. Nimeshindwa kuila hii chapati hebu angalieni inavyonitizama kwa dharau kama hivi:

IMG_20200305_140330_9.jpg

Nikapika chapati ya pili nayo imeungua imekuwa kaukau. Kwa kweli nimemkumbuka sana mke wangu na vyakula anavyonipikia. Nimejua hata kama mwanamke ni mama wa nyumbani hapaswi kudharauliwa kazi ya moto si kazi nyepesi ina shughuli pevu. Ukila chakula cha mkeo ujue ni damu yake, jasho lake, nguvu zake, upendo wake, maumivu yake ya kuungua nk. Kubeza chakula kilichopikwa na mwenzio ni dhambi kubwa Mungu atusamehe tu.

Ila nashukuru chapati moja tu kati ya kumi na tano ndio iliyotoka vizuri nyingine nimeunguza sana. Sijui kama kesho zitafaa kula kiporo, ila kwa kweli kuna haja ya kujua kupika hata kama una mke. Nimekulia katika familia za mfumo dume mwanaume hakai jikoni, siwezi kujilaumu mwenyewe kwa kutojua kupika. Kwa kweli leo nimejua umuhimu wa mke wangu katika maisha yangu, Nakupenda sana Mke wangu, Mungu akujalie maisha marefu, ukiniacha mwenyewe nitakonda. .
IMG_20200305_141000_4.jpg

At least this one came out better compared to others: (Sadly, It is the only one)
IMG-20200303-WA0001.jpeg

Kwa jinsi nilivyoungua Yesu tu ndio anajua, Nawasisitizia tu tuwaheshimu sana wake zetu. Hata kutofanikiwa ni kwa sababu tu ya kutoheshimu nafasi za wenza wetu katika maisha yetu. .
 
Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,097
2,000
Ukoo wetu wanaume kuingia jikoni ni kosa kubwa na inatokana na mfumo dume tu. Hicho ndicho kimefanya hata nishindwe kupika chakula changu mwenyewe. Kama unajua kupika usitake kunipa fedheha kwenye uzi wangu pita kule. Dharau, ugomvi au kubishana sipendi kabisa kwanza nina maumivu ya kuungua sana na lengelenge linauma kwa joto kali hili
 
Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,097
2,000
Wakati wengine wanaombea wake/mume afariki aoe au kuolewa upya.hongera mkuu
Tena sisi wakristu kwa sababu ndo haivunjiki mpaka kifo kitenganishe basi ndio huwa tunaongoza kwa hayo
Ila ndugu zetu waislamu mke akikushinda unamwacha aende zake

Kupika kazi sana kwa kweli nilikuwa naona simple sana. Nitakapokula chakula sasa nitaweka appreciation kubwa hata kama kina chumvi
 
Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,097
2,000
Najua kiasi chake
Mama was a good cook
Turns out I have a passion as well
You have a passion for eating definitely utakuwa mpenda kula kama mimi. Leo nimekula chakula nikakumbuka sijasali dah kitu ambacho si kawaida yangu kabisa. Nimeenda kuzunguka na msalaba njia ya msalaba jumuiya nimerudi njaa inauma hatare nikajisemea tu usiposali mda mwingine unakuta unakula na kishetani alafu huwezi shiba

I like watching cooking shows kwa sababu mie napenda kula mapocho pocho sana sana

You still have time to learn how to cook. Some people wanadhani wanajua kupika coz they are cooking every day but if you watch cooking channel unaweza ambiwa unaunguza chakula sana and unakiharib
 
Tansy

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
3,545

Ooh you're right , Of course I'm a foodie
Pole for what you have gone through today
I also love watching cooking videos on YouTube siku hizi nimehamia Facebook pia
Nitaenda hata cooking class hapo baadae niwe na experience zaidi
 
Hahah you eat in the kitchen and when the food is ready unawaambia "nimeshiba hata silagi sana" eh. Ukiwa mbele ya wageni unajifanya hata silagi kumbe umepakia maviporo ya tokea majuzi haha ila they say hakuna chakula kitamu kama kiporo

You are not late to go to cooking classes. Ila sasa siku hizi wanazilipia, you could start small and level up the ladder

Unapendelea kupika vyakula gani currently??
 
Haha so true
Nitaenda tu kujifunza tu
Vyakula vya kiafrika tu hivi haswa vya Nazi au karanga , vitafunio .
 
Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,097
2,000
Haha so true
Nitaenda tu kujifunza tu
Vyakula vya kiafrika tu hivi haswa vya Nazi au karanga , vitafunio .
Watu wanafagilia sana kisamvu cha nazi ila ukila cha karanga kwa kweli utasahau cha nazi

Ubaya wa Africa there is less food to make vyakula viko aina tatu: cha unga wa mahindi au ngano; ndizi; na wali

Asia wanaonekana wana vyakula vya aina nyingi sana, you should learn their cooking. It wont be fun if you learn African. It will be like an adventure if you learn others

African foods might be good when they go in themouth but they come out badly, constipation
 
Cha karanga ni kitamu zaidi kwa kweli
Ohh you're right learning something new is actually a good thing to do .
 
Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,097
2,000
Cha karanga ni kitamu zaidi kwa kweli
Ohh you're right learning something new is actually a good thing to do .
You have tried it huh. Your mom isn't alive?

Do teach your kids to cook wasije wakawa kama mie am grown up man and I don't even know how to cook chai
 
Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,097
2,000
Yeah hayupo
I will definitely teach them that
I bet chai unaweza na vingine
What do you remember about mom cookings?

I dont think so inabidi nijifunze kupika by the end of this year nijue hata kupika five cookings
 
Tansy

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
3,545
2,000
What do you remember about mom cookings?

I dont think so inabidi nijifunze kupika by the end of this year nijue hata kupika five cookings
Alikuwa anapokea tenda hizi
Nilikuwa sizipendi since kazi ni nzito Kama kuserve , kuosha vyombo n cooking the whole day lkn namiss zile moments Sana
Hakuna alichopika kikataste vibaya
That's a good thing to learn for starters .
 
Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,097
2,000
You hold to memories and you remember her by
When we remember the loved ones they are not truly dead to us
I believe she is far away watching you grow into this wonderful woman
She will rest easy knowing you follow her foot steps
When you have kids tell them about your mom cookings

What was your mom favorite food?
 
Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,097
2,000
Ya nini kujichosha na chapati mkuu? si ungepika tu ugali mambo yaishe
Huo ugali ndo kabisa nisingeweza

Kachumabri kukata naweza, kwa kweli ningejua kuopika ugali basi hata kachumbari ningelia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom