Nimeahidiwa Q-Net kuwa bilionea baada ya miaka mitano

Supermind

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
259
243
Iko hivi;

Kuna dada fulani hivi tuliwahi kufahamiana huko nyuma, alinipigia simu na kunijulisha kwa kina kuwa kuna mchongo fulani hivi kashawishika kujiunga nao ni wa Q-net. Wenyewe unatakiwa mtu unahudhuria semina zao mbili then utatakiwa kujiunga kwa shs. Milioni tano na laki tano (5,500,000/-) kwa kima cha chini. Pesa hio unailipa kwenye account yao in terms of dollars Hong Kong au Malaysia. Ukishailipa unachagua moja ya bidhaa zao eidha saa, mikufu, au vito vingine vya thamani vilivyotengenezwa kwa madini.

Ukishamaliza hio process unakuwa tayari partner, sasa na wewe unaanza kutafuta watu wengine wa kuwaunga ili biashara iendelee. Utatakiwa kuunga watu mfano wa tree diagram au ngoe kwa wale waliowahi kusoma hesabu za ngoe, utaunga watu kulia kuanzia wawili na kuendelea na kushoto hivohivo. Unaeza unga mfano, kulia watu kumi na kushoto watu kumi. Gharama ni hiohio (mil. 5.5) kila mmoja. So the way wanavyoingia ndivyo na wewe kwenye account yako inafura mihela, maana kwa kila anayejiunga wewee unapata gawio.

Sasa patamu aliponiambia ni kuwa nikiwa na partiner kumi kulia na kumi kushoto, na hao partner wangu wakafanya hivo, na partner zao wakafanya hivo, na wa kwao tena wakafanya hivo yaani hivohivo na kuendelea, baada ya miaka mitano nakuwa bilionea wa kutisha hapa nchini.

Akanisisitiza faida unaanza kuiona kuanzia nikiwa na partner wawili. So juhudi yangu ya kupeleka watu kwenda kuungwa kwenye branch account yangu ndivyo ntakavyozidi kuwa milionea.

Mimi niko mkoani Singida ila wao hao Qnet ofisi yao ipo Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam.

Sasa ndugu zangu wanajamvi kabla sijafanya maamuzi magumu nimeona hichi kitu nikilete hapa kupata ushauri kabla sijakurupuka. Nimechoka kuwa maskini.

USHAURI JAMANI!
 
Kwa ushauri wangu bro, kama unayo hiyo hela fanya biashara unayoiweza kuliko kuchangia watu mitaji. Mke wangu pia alikua na rafiki yake alitusumbua sana tujiunge nikampiga na marufuku simu zake wala home asifike.
Nifafanulie kidogo, haina ukweli...!? Au ...
 
Umuulize na hiyo saa ya wanayokupa mfano ukitoa hizo mil 5.5 ukiamua kuiuza unawez ukauza kwa sh ngapi? Tusipende vitu virahisi, na wakisha ona unapotential ya kupata na kulipa hiyo hela wanakua rafik zako kweli na watakufuatilia hadi uchoke
Alisema bidhaa zao huruhusiwi kuuza. Ukinunua utumie wewe mwenyewe, ndio sharti la kampuni.
 
Ndugu achana na hao wote iwe forever iwe nini

Walimmendea kaka angu na kuanza kumshawishi,kaka angu akaniomba ushauri weee nilimkataza uzuri alinisikiliza. Utaliaa

Ukiwapa hiyo pesa unadhani ni rahisi kumpata mtu awekeze milion tano wewe upande juu. Sio rahisi bro

Uza hata nyanya sio hizo mishe; okoa pesa yako kama huna cha kufanya weka benki tu
 
Ndugu achana na hao wote iwe forever iwe nini

Walimmendea kaka angu na kuanza kumshawishi,kaka angu akaniomba ushauri weee nilimkataza uzuri alinisikiliza. Utaliaa

Ukiwapa hiyo pesa unadhani ni rahisi kumpata mtu awekeze milion tano wewe upande juu. Sio rahisi bro

UZA hata nyanya sio hizo mishe; okoa pesa yako kama huna cha kufanya weka benki tu
Asante kwa ushauri mkuu. Ndo uzuri wa jf, watu wanafungukaga.
 
Back
Top Bottom