Nimeachwa tena, sijui tatizo langu ni nini?

Nimeachwa tena, sijui tatizo langu ni nini?

Sasa ndio ujue kwamba wewe sio intelligent wala hujaelimjka japo una kisomo cha darasani.

Maelezo yako tu yameonesha tatizo lako lote lakinj pamoja na kuonekana intelligent na msomi wa chuo umeshindwa kugundua tatizo ama changamoto binafsi.

Siku zote tunafundishwa kitu kimoja kinaitwa Adabu, ukiikosa hiyo au ukiiasi lazima itakuletea matokeo mengine. Labda nijuulize tu kama kati ya wanaume hao watano ni wangapi uliwahi kuwatambulisha kwenu na wewe ukatambulishwa kwao kama mchumba?

Hujui kwamba unafanya makosa makubwa, narudia tena, unafanya makosa makubwa kuingilia nafasi ya mke wakati wewe sio mke wa huyo mwanaume?

Ikiwa unaweza kuishi kwa mwanaume, ukashiriki naye mapenzi, ukamfulia, kumpikia, kumfanyia massage, kuoga naye na kufanya yote yampasayo mke wake kwanini haangaike na wewe?

Unaposikia ndoa ni chungu halafu watu hawaachani ila wanavumiliana ni kwa sababu ya kiapo cha ndoa tu.

Kiapo cha ndoa ndio pona pona ya ndoa nyingi, watu wakifikiria jinsi watu wake wa karibu walivyohangaika kumfanikishia tukio lake anaona ni aibu na hasara kuachana na mkewe kwa sababu ambazo zinaweza kumalizika kwa muafaka bila kutengana, hapo ndipo kunakoitwa uvumilivu wa ndoa.

Sasa wewe dadaangu, unamvulia nguo mwanaume, unamfulia, unamuogesha na mambo mengine meengi, hutambuliki kwao, unategemea ufanyiwe nini?

Yaani binti wa miaka 20s umeachwa na wanaume watano, ukijumlisha uliyemuacha jumla wa sita, hapo hujachumbiwa wala kuolewa, jiulize hadi utakapoolewa utakuwa umejiuza kwa wanaume wangapi?
 
nahisi ni tabia yako tu hairidhishi...
hata nikiku-judge kwa kutumia avatar yako(whatever sio pic yako or not) naona kabisa kuna kasoro huwezi date na gentleman...
pia inaonesha huna malengo hasa ya ndoa..
unataka mahusiano tu huwazi mbele.
 
Altitude is averythng,wanawake wengi wanaona kama uzuri ndo unawapa mume!i don't point fingers but if the story is valid then chek yo altitude
Najua uzuri si kila kitu,sawa my attitude nibadili nini specifically, honestly sijuii
 
Slow down girl, mid twenties...5+ relationships which I'm certain involved sexual intercourse, damn it..!!! Too cheap to my liking. Vaeni pichu jamani, ukigota 30+ bila ndoa si utakuwa umemaliza mtaani kwako!
 
Katika watu wote huyu ndie alikuwa anaanza kukwambia ukweli ila kaishia njiani.

Wataalam wa mahusiano wanaamini uhusuano, kwa mahusiano mengi yanayodumu zaidi ya miezi sita lazima yafe na hayazai ndoa.

Bila shaka unahtaji ndoa ndio maana unaumia kuachwa, kama ingekuwa ni kula bata tu kimjini kisha kila mtu kimpango wake isingekuumiza, na ndio maana huo ni uhusiano wa 5.

Kosa lako ni...kutamani kuanza mapenzi mapya kwa wepesi, na inaonesha ukiwa desperate kama saizi hivi, atakaeonekana anakuja mbele yako unampa nafasi na unakuwa na tumaini kubwa kuwa hapo umetibu tatizo, kumbe umefungulia mlango jambazi la kiume.

Unapaswa kutulia kwanza, usiteswe na mahusiano, ya dharau mapenzi, kisha uwe na kibuli cha mapenzi, usivue chupi kwa kila mwanaume, wanaume wengi tuna watu wetu na ninyi wazuri wa sura/umbile ni wakurukia tu, na kusafisha bunduki, na ukivuliwa nguo unabaki kuwa big G iliotafunwa, hapo utaachwa milele.

Napenda kipande kimoja cha wimbo wa MB dogg Ratifa, alisema penzi la dhati ratifa utajua tu. Hatanww uwe na akili ya kupimaapenzinya dhati.

Na ukweli ndio huo usiwe mwepesi wa ndio mzee, wanaume wengi walaji na kupita ukiwazingua kidogo tu wanapotea (japo sio wote). Ila kuna hii pia mwanaume anaekuangaikia kukupata usiku na mchana mfululizo kwa muda mrefu hata wa mwaka mmoja tu, kukuacha huyo ni ngumu, wape wanaume ugumu kukupata.

Akijua hustle ya kukupata hakuachi kiurahs. So ushauri wangu mkubwa usipende vua chupi haraka, usipende penda mpk unaoza kama ushatolewa mahali vile, usipende kuanzisha uhusiano mpya kutibu jeraha la uhusiano wa zamani. penda ila kwa kiburi, jamaa atakuwa makini, atajua akizingua anaaachwa.

Kama unalenga ndoa hakikisha ndani ya miezi sita walau muoaji anaonesha nia tena iliopimwa ukaiona ni ya dhati.

Unapotongozwa penda kuwa na maneno yanayomkatisha mwanaume tamaa mapema, ya kukera, wagongaji huyakimbia haya mapema. Wa dhati wengi huyavumilia.

Jioni njema.

Mhhh haya bwana ahsante,kosa nnalo liona ni kupenda sana,will work on it,nipende kidogo,nijipende kwanza
 
Pole mamii. Kuna kipengele hujagusia. Kunako 6x6 inakuaje? Hilo ni eneo muhimu ktk mapenzi. Uko fit? Hakunavitu vidogo2 vinavyoweza kuwa vinachangia? K kavu hupendwa. Mihemko na madoido pia. Kinywa kinatoa harifu mby? Unamhudumia vp baada ya tendo? Una overdo kwenye game? Jitafakari ktk nyanja hiyo
Siwezi elezea yote hadharani but najitahidi sioni kama ni ishu,K haina harufu kwa usafi binafsi niko vizuri namjali mwanaume sana kadri niwezavo,si unajua ukimpenda mtu inavokuwa
 
Maisha yanabadilika we umeachwa mi nipeta mtoto mkare ila pole sana funga na maombi then toka nje mungu atakuonesha mtu mpya..
 
Sasa ndio ujue kwamba wewe sio intelligent wala hujaelimjka japo una kisomo cha darasani.

Maelezo yako tu yameonesha tatizo lako lote lakinj pamoja na kuonekana intelligent na msomi wa chuo umeshindwa kugundua tatizo ama changamoto binafsi.

Siku zote tunafundishwa kitu kimoja kinaitwa Adabu, ukiikosa hiyo au ukiiasi lazima itakuletea matokeo mengine. Labda nijuulize tu kama kati ya wanaume hao watano ni wangapi uliwahi kuwatambulisha kwenu na wewe ukatambulishwa kwao kama mchumba?

Hujui kwamba unafanya makosa makubwa, narudia tena, unafanya makosa makubwa kuingilia nafasi ya mke wakati wewe sio mke wa huyo mwanaume?

Ikiwa unaweza kuishi kwa mwanaume, ukashiriki naye mapenzi, ukamfulia, kumpikia, kumfanyia massage, kuoga naye na kufanya yote yampasayo mke wake kwanini haangaike na wewe?

Unaposikia ndoa ni chungu halafu watu hawaachani ila wanavumiliana ni kwa sababu ya kiapo cha ndoa tu.

Kiapo cha ndoa ndio pona pona ya ndoa nyingi, watu wakifikiria jinsi watu wake wa karibu walivyohangaika kumfanikishia tukio lake anaona ni aibu na hasara kuachana na mkewe kwa sababu ambazo zinaweza kumalizika kwa muafaka bila kutengana, hapo ndipo kunakoitwa uvumilivu wa ndoa.

Sasa wewe dadaangu, unamvulia nguo mwanaume, unamfulia, unamuogesha na mambo mengine meengi, hutambuliki kwao, unategemea ufanyiwe nini?

Yaani binti wa miaka 20s umeachwa na wanaume watano, ukijumlisha uliyemuacha jumla wa sita, hapo hujachumbiwa wala kuolewa, jiulize hadi utakapoolewa utakuwa umejiuza kwa wanaume wangapi?
There are things i do out of love,lakini naona ndio kosa langu hilo,
Ni vile let's say mpenzi wako weekend akwambie mgongo unamuuma sana,why not nimfanyie massage,
Kama kupenda ni kosa then i am paying the ultimate price,sijawahi ishi kwa mtu zaidi ya siku moja,sijawahi mfulia mwanaume,kupika na usafi sawa mara chache,sio kwamba napenda kuranda randa t happens wanaondoka and i can't shoot the exact reason
Hata hivo ahsante kwa ushauri,will have to change my methods
 
Hi All,

Jamani honestly nina stress acha tu.

Nataka nitumie jioni hii online walau nipunguze mawazo mana hata ubusy wa kazi haupunguzi maumivu ya mapenzi.

Story ni nimeachwa tena, yes, ni jambo limejirudia sanaa maishani mwangu kiasi kwamba nishasali sana na ninaendelea kuomba Mungu anisaidie.

Hii ni mara ya 5 naachwa, kama kuacha mtu nimeacha only mara 1.

Am the type of woman ninayeitwa mzuri na wengi, charming, intelligent nk.

Sawa kama binadamu nina kasoro lakini naamini zinaweza vumilika, sioni kama nina anything extreme.
Umri mid 20's,elimu chuo
Kinachoniliza jmn ,nilikua na uhusiano mzuri sana kama mwaka hivi na mwanaume nnaeshindwa msahau mpaka sasa,kama baada ya miezi 6 alipunguza sana mawasiliano,nikavumilia badae nkaona nimuite tuongee anambie tatzo ni nini,
Kweli tuliongea na alisema wazi hana tatzo na mimi,yuko tu off mood so anataka tu muda ajitafakari,mhhh inaumiza lakin nilipata relief kdogo nkamwambia sawa d,ntakuwepo kwa ajili yako,yeye tangu siku hyo yuko kimyaa,hajibu msg hapokei simu nk,jibu la ukimya linaumiza jmn acha tu,
Imepita miez 4 sasa hanitafuti wala nini,mara 2 nilipata hasira sana nkamjibu vibaya nilimwambia ukimya huu ni ujinga hatuwezi endesha mahusiano hivi,
Siku hio akasema mi na yeye basi tuwe marafiki,nikishaumia sana iliniumiza zaidi lakini nkasema yatosha God knows i tried ,na mi sijamtafta zaidi ya mwezi sasa najiuguza,
Ishu ni hii trend ya kuachwa,mpaka lini,tatzo ni nini,nimechoka hii hali,
Sijawah achana na mtu kwa ugomvi mkubwa,niliemuacha once several tyms nilishamuomba msamaha if ts karma i paid the price niliachwa na wawili baada yake,wanaoniacha wanasemaga tu ur so beautiful and still young bla bla,ts not u ts me,wengine distance inavunja mahusiano bila sababu, nk...
I don't get it,tatzo langu nini hasa
Nimepoteza apetite ya mapenzi kabisa,mana naachwa najipa moyo namove on naachwa tena khahh,
Ukiniambia kupenda saivi ni jambo impossible kwangu
MY BEHAVIOUR KWNY MAHUSIANO
Jmn sijisifu but ni mtu ninaependa mwanaume mmoja in a time,sio ombaomba japo naweza omba hela nikiwa na shida like 3,4 times a year,(sijui ni mara chache au nyingi),najali,nacare,napika,nampa mapenzi ,namuuguza akiugua,namsikiliza,namheshimu,mambo ya massage na madeko yote nnayojua,siko desperate,sijawah zungumzia ndoa japo i may give some hints,inshort am a total woman n i let him be the man,
Hakuna alowahi ntajia any shortcoming nirekebishe mana huwa nauliza jmn nmekukosea nini japo niweke sawa ,wanasema hamna,pls assist nina maumivu makali kila nikiwaza nimeachika tena

siku hizi mahusiano au ndoa ni kama ajira.. kila mtu anaagalia vigezo.. so inawezekana amekutana na anaekuzidi vigezo..

nowdays only fittest ndio wanaosurvive..

asilimia kubwa ya ndoa nilizouzuria miaka hii ni madem majembe darasani/maishani au mambo safi kwao.


siku hizi kawaida sana kpmg anaoa pwc au mtoto wa dewji anaoa kwa bakhressa.. mkwere anaoa asas..

so isije kuwa dada yangu ulikuwa na mtu unampenda sana but kwenye vigezo hamuendani may be mambo safi kwao au jembe maishani, mwenzangu na mie dressing table na lips shine umeridhika ni kiajira chako cha laki 5 na ka degree kako cha msaada helsb, so kajichekecha kaona hapa tutasumbuana mbeleni bora nisepe tu.

muhimu ni kukubaliana na ukweli maisha yamebadilika sana na uchumi wa kibepari hauna ndoa za kizembe zembe
 
Dada pole sana ila naomba niwe mkweli kwako kwani nakupenda.
Kuna msichana alikua mzuri ka ww ila alikua ananuka mdomo na ye alikua hajui. Embu jicheki. Pia harufu sehemu za siri.
 
Kuachwa noma, usiombee.Me nliachwa na ma'mtoto wangu kwa kudanganywa kuwa mchepuko wake atamwoa kwa sharti la kunifungulia mashtaka mahakamani ili apate talaka.Alinipa talaka ila mchepuko kamwacha soon baada ya talaka.Me nilimlea mwanangu tangu akiwa 3yrs.Huyo mama alitaka kurudi baada ya kuona kaachwa na mchpk nikakomaa miezi 18 baadaye nkamruhusu kurudi.Tuliishi naye tena kwa miezi 20 akapack tena na kuniambia aenda pumzika na kuwa anipenda na atarudi tena.Alitaka kuondoka na mtoto nkakataa na nkamwambia kwangu hawezi rudi tena.Baada ya miezi 6 akatuma watu kuomba arudi lakini nlikomaa hadi leo mpaka kakata tamaa kahama mji.Hadi sasa niko single na siamini tena mwanamke yeyote labda mamangu.Ila maumivu ya kuachwa handanganyi mtu.Nimekomaa na dogo wangu hadi leo hii yuko form one ingawa mamake anasumbua sana kumfuatafuata na bahati mbaya yuko boarding.So Badiebey pole sana yote ni maisha na wenzetu wasema ''LIFE IS WHAT YOU MAKE''
 
Am the type of woman ninayeitwa mzuri na wengi,
charming, intelligent nk.

Hicho unachoita imtelligence inawezekana likawa tatizo, hakuna mwanaume anapenda mwanamke mjuaji juaji...nina sister angu ana tabia kama zako, possible ukawa ni wewe...!!
Heheheh imebidi nicheke tu,kuna tofauti kati ya kua mjuaji/much know na kuwa intelligent tu na mambo ya hapa na pale,
But hey i can't play dumb to boost a man's ego,..
Kama wanaume mnapenda vilaza sitakua hivo ,i am humbly a smart lady,been raised hivo
 
There are things i do out of love,lakini naona ndio kosa langu hilo,
Ni vile let's say mpenzi wako weekend akwambie mgongo unamuuma sana,why not nimfanyie massage,
Kama kupenda ni kosa then i am paying the ultimate price,sijawahi ishi kwa mtu zaidi ya siku moja,sijawahi mfulia mwanaume,kupika na usafi sawa mara chache,sio kwamba napenda kuranda randa t happens wanaondoka and i can't shoot the exact reason
Hata hivo ahsante kwa ushauri,will have to change my methods

Unaanza uchumba ndipo inafuata ndoa. Lakini, baadhi yenu mnavunja kanuni ya asili kwa kufanya ndoa iwe ya kwanza halafu uchumba ndio ufuate, si kiroja hicho? Hizo siku moja moja ndizo zinazokuponza.

Hayo waliyokuambia kuhusu usafi nk. ni ziada tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom