Nilizalishwa na kudhalilishwa

Nilizalishwa na kudhalilishwa

Katika harakati za kutafuta mkate nilikutana na mwanaume ambaye hatimae akawa mzazi mwenzangu, tuliishi kipindi kirefu sana tukiwa kama mke na mume, mwisho wa siku jamaa akaamua kuachana na mimi kwa mbwembwe na udhalilishaji wa kimataifa,mabaya mengi sana alinizushia ili tu azma yake ya kutaka kuniacha kiholela ipate waungaji mkono, Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa wengi walimuunga mkono, kejeli matusi vilikuwa vikipishana mitaani vikinisaka mimi ,na haikuwa mimi tu mpaka familia yangu iliunganishwa kwenye hiyo dhihaka, kilikuwa kipindi kigumu sana haijawahi kutokea, maradhi msongo wa mawazo viliandama kiasi kwamba niliichukua dunia, nilijuta kwanini nilizaliwa, wakati mwingine nilitamani nife niondokane na haya mateso, lakini nilikuwa nikimwangalia mwanangu naishia kulia, nawaza nikifa leo huyu kiumbe asiyekuwa na hatia nitamwacha katika mazingira gani? Mungu si James kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele nikawa naizoea hali ile, nikaikubali hali ile na niambiwe au nisikie nini sikuweza kuumia tena, mpaka naandika uzi huu nina amani na yaliyopita yamebaki simulizi tu wala hayaniumizi tena. Kilichonileta kwenu ni hiki -Mpuuzi yule ana kila dalili ya kutaka kujiletaleta kwangu, najua iko siku ataleta swaga zake za kiduwanzi, nimetafakari ikitokea nimjibu nini ili naye ayapate maumivu mara mia ya niliyoyapata mimi nimeshindwa, nisaidieni wana MMU.
Katika harakati za kutafuta mkate ulikutana na mwanaume???

Ina maana Huyo jamaa akawa riziki kwako, means akawa km ndie source of income kwako??
Kuna kila dalili kuwa bado unampenda Huyo jamaa unless usingetaka kuja kuomba ushauri hapa!

Lakini pia sisi hatuwezi kuhukumu upande mmoja maana Ww hujaeleza mapungufu yako, huwezi kushawishi watu hapa kuwa Ww ni malaika hukuwa unamkosea mme wako!
 
Ni kweli mimi sio malaika hata wewe sio malaika pia, ila sio kweli kwamba bado nampenda
 
Katika harakati za kutafuta mkate nilikutana na mwanaume ambaye hatimae akawa mzazi mwenzangu, tuliishi kipindi kirefu sana tukiwa kama mke na mume, mwisho wa siku jamaa akaamua kuachana na mimi kwa mbwembwe na udhalilishaji wa kimataifa,mabaya mengi sana alinizushia ili tu azma yake ya kutaka kuniacha kiholela ipate waungaji mkono, Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa wengi walimuunga mkono, kejeli matusi vilikuwa vikipishana mitaani vikinisaka mimi ,na haikuwa mimi tu mpaka familia yangu iliunganishwa kwenye hiyo dhihaka, kilikuwa kipindi kigumu sana haijawahi kutokea, maradhi msongo wa mawazo viliandama kiasi kwamba niliichukua dunia, nilijuta kwanini nilizaliwa, wakati mwingine nilitamani nife niondokane na haya mateso, lakini nilikuwa nikimwangalia mwanangu naishia kulia, nawaza nikifa leo huyu kiumbe asiyekuwa na hatia nitamwacha katika mazingira gani? Mungu si James kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele nikawa naizoea hali ile, nikaikubali hali ile na niambiwe au nisikie nini sikuweza kuumia tena, mpaka naandika uzi huu nina amani na yaliyopita yamebaki simulizi tu wala hayaniumizi tena. Kilichonileta kwenu ni hiki -Mpuuzi yule ana kila dalili ya kutaka kujiletaleta kwangu, najua iko siku ataleta swaga zake za kiduwanzi, nimetafakari ikitokea nimjibu nini ili naye ayapate maumivu mara mia ya niliyoyapata mimi nimeshindwa, nisaidieni wana MMU.
Mpaka hapa usituambie kitu zaidi ya kuwa unampenda na niongeze kitu, utakachomfanyia ujue mtashare maumivu cz tayar mtakuwa pamoja......

Ila kama kweli umeamua kuwa peke ako basi kulipa kisasi ni kazi ndogo sana....
1)KAA KIMYA
2)KAA KIMYA
3) KAA KIMYA

silence is the best revange
 
Mrudie akishakolea umwage kama kiporo cha ugali
Mmmnh anaweza kolea yeye akapigwa kingine.

Akistuka ana watoto wawili baba yao kasepa. Kwa jinsi ninavyoona huyo mwanaume mwenzetu ana tabia za jogoo yaani kuzalisha na kukimbia kulea.
Anaoga majukumu au akipata mchepuko anatupa jongoo na mti wake.
 
Uandishi wa kiume huu.sorry au umeandika kwa niaba ya dada ako?

Pole sana dada.

Kasema alizalishwa, hajazaa.
Kuzalishwa ni kwa lazima Bila hiari yake.
Kakamuliwa hata kama lilikuwa hamna kitu tumboni akajikuta kimekuja automatically

Kwani jf ndo ilikuzalisha na kukudhalilisha,kumbe ndo maana jamaa alikukimbia unaonekana si mzima kichwani baadhi ya boliti zimelegea

Huna akili ndo maana umezalishwa na kukimbiwa + kudhalilishwa na bado unaendelea kuuthibitishia ulimwengu kuwa bado dish lako liko tenge,
Huyu mleta mada ni dume jike?
Thread zake kama za sexless, kwenye thread anakuwa na jinsi tofauti tofauti!
Aliyekuwa mke wangu sasa ni mchepuko wangu
 
Hakuna haja ya kusubiri arudi umuumizi roho. Fanya mambo yako bila kutamani kuonana naye tena ikitokea akakutafuta m block wala usikubali kuwa na vikao naye itamwumiza sana wala usimpe nafasi ya kumwona mtoto hiyo nayo itakuwa adhabu kwake
 
Back
Top Bottom