Nilizalishwa na kudhalilishwa

Nilizalishwa na kudhalilishwa

Katika harakati za kutafuta mkate nilikutana na mwanaume ambaye hatimae akawa mzazi mwenzangu, tuliishi kipindi kirefu sana tukiwa kama mke na mume, mwisho wa siku jamaa akaamua kuachana na mimi kwa mbwembwe na udhalilishaji wa kimataifa, mabaya mengi sana alinizushia ili tu azma yake ya kutaka kuniacha kiholela ipate waungaji mkono.

Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa wengi walimuunga mkono, kejeli matusi vilikuwa vikipishana mitaani vikinisaka mimi na haikuwa mimi tu mpaka familia yangu iliunganishwa kwenye hiyo dhihaka, kilikuwa kipindi kigumu sana haijawahi kutokea, maradhi msongo wa mawazo viliandama kiasi kwamba niliichukua dunia, nilijuta kwanini nilizaliwa.

Wakati mwingine nilitamani nife niondokane na haya mateso, lakini nilikuwa nikimwangalia mwanangu naishia kulia, nawaza nikifa leo huyu kiumbe asiyekuwa na hatia nitamwacha katika mazingira gani?

Mungu si James, kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele nikawa naizoea hali ile, nikaikubali hali ile na niambiwe au nisikie nini sikuweza kuumia tena, mpaka naandika uzi huu nina amani na yaliyopita yamebaki simulizi tu wala hayaniumizi tena. Kilichonileta kwenu ni hiki -mpuuzi yule ana kila dalili ya kutaka kujiletaleta kwangu, najua iko siku ataleta swaga zake za kiduwanzi, nimetafakari ikitokea nimjibu nini ili naye ayapate maumivu mara mia ya niliyoyapata mimi nimeshindwa.

Nisaidieni wana MMU.
Kumfanya apate maumivu kama uliyoyapata sio kazi yako. Muombee aache tabia mbaya.
 
Si kila ushauri unafaa. Utakapomuambia huyo mzazi mwenzako mtoto si wake. Na siku mtoto akitaka kumuona baba yake utamuambiaje? Damu nzito kuliko maji. Angalia maisha yako na mwanao. Huyo mtu atakapotezea muda wako tu.
 
Hapo umesema upande wa mabaya yake, je na wewe mabaya yako mpaka ikapelekea kutokea hayo yaliyotokea ni yapi?

cc: mahondaw
 
Huyo sio wa kumkaribisha na kumpa nafasi aisee, vinginevyo kama bado una hisia nae..

Dawa yake ni kumfungia vioo milele, kumpuuza na kumdharau mazima mbona atashika adabu yake.
 
Ndugu Mzazi/ Mlezi

Uongozi wa shule unakukumbusha kuwa mtoto wako hataruhusiwa kupanda basi la shule wala kuingia darasani kama hujalipa ADA”
 
Ni ushauri pia ila siwezi kuufanyia kazi, asante.
Kumbe wewe tayari moyoni mwako unacho kitu ambacho umepanga kukifanya kwa huyo unayemwita "mpuuzi"; sasa umetuomba ushauri ili iweje wakati tayari unajua nini cha kufanya?

Kama wewe ni MKRISTO basi kumbuka imeandikwa hivi; "wapenzi msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya MUNGU maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi, mimi nitalipa anena BWANA. Lakini adui yako akiwa na njaa mlishe, akiwa na kiu mnyweshe, maana ufanyapo hivyo utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema". WARUMI 12:19-21

Tena imeandikwa; "kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na BABA yenu wa Mbinguni atawasamehe ninyi makosa yenu. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala BABA yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu". MATHAYO 6:14-15
 
Unataka kumuumiza?? akijileta mkaribishe halafu mletee wahuni wampe kisago cha nguvu, maumivu ya mwili atakayoyapata ndio atajua uliyapata wewe ya moyo.
 
Katika harakati za kutafuta mkate nilikutana na mwanaume ambaye hatimae akawa mzazi mwenzangu, tuliishi kipindi kirefu sana tukiwa kama mke na mume, mwisho wa siku jamaa akaamua kuachana na mimi kwa mbwembwe na udhalilishaji wa kimataifa, mabaya mengi sana alinizushia ili tu azma yake ya kutaka kuniacha kiholela ipate waungaji mkono.

Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa wengi walimuunga mkono, kejeli matusi vilikuwa vikipishana mitaani vikinisaka mimi na haikuwa mimi tu mpaka familia yangu iliunganishwa kwenye hiyo dhihaka, kilikuwa kipindi kigumu sana haijawahi kutokea, maradhi msongo wa mawazo viliandama kiasi kwamba niliichukua dunia, nilijuta kwanini nilizaliwa.

Wakati mwingine nilitamani nife niondokane na haya mateso, lakini nilikuwa nikimwangalia mwanangu naishia kulia, nawaza nikifa leo huyu kiumbe asiyekuwa na hatia nitamwacha katika mazingira gani?

Mungu si James, kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele nikawa naizoea hali ile, nikaikubali hali ile na niambiwe au nisikie nini sikuweza kuumia tena, mpaka naandika uzi huu nina amani na yaliyopita yamebaki simulizi tu wala hayaniumizi tena. Kilichonileta kwenu ni hiki -mpuuzi yule ana kila dalili ya kutaka kujiletaleta kwangu, najua iko siku ataleta swaga zake za kiduwanzi, nimetafakari ikitokea nimjibu nini ili naye ayapate maumivu mara mia ya niliyoyapata mimi nimeshindwa.

Nisaidieni wana MMU.
Huko ndiko kupata uzoefu. Utakuwa umeelewa wapi ulikosea/hukuwa makini, ukipata nafasi nyingine usifanye makosa.
 
fanya hivi,tafura bwana,mpe hiyo stori halafu muwe wote siku moja umuite huyo jama,uache mlango wazi akigonga mfungulie iki aone laivu mnavyogegedana na huyo bwana mpya
 
Visasi ni mambo ya kizamani...kama umuhitaji,atakapokutafta mwambie ukweli kua umuhitaji na aendelee na maisha yake.
Kwanini upoteze muda kuwaza jinsi ya kumuumiza?
Itaonekana utoto.
 
Back
Top Bottom