Kumbe wewe tayari moyoni mwako unacho kitu ambacho umepanga kukifanya kwa huyo unayemwita "mpuuzi"; sasa umetuomba ushauri ili iweje wakati tayari unajua nini cha kufanya?
Kama wewe ni MKRISTO basi kumbuka imeandikwa hivi; "wapenzi msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya MUNGU maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi, mimi nitalipa anena BWANA. Lakini adui yako akiwa na njaa mlishe, akiwa na kiu mnyweshe, maana ufanyapo hivyo utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema". WARUMI 12:19-21
Tena imeandikwa; "kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na BABA yenu wa Mbinguni atawasamehe ninyi makosa yenu. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala BABA yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu". MATHAYO 6:14-15