Vionjo vya Arsis 3 Kumwokoa Msukule 1.
Hiki kisa kilitokea kama miaka 2miwili baada ya kurudi sagfari yangu ya Shinyanga.
Siku hiyo nimepigiwa simu na mtu nisiemfahamu, yaani halikutoka jina kwenye simu Kupokea ni mwanamke akajitambulisha kua yeye kapewa namba zangu na Sharifu Ali wa Shinyanga, kamwabia aongee na mimi mwenyewe moja kwa moja.
Nikamwabia, karibu sana, Sharufu ni mzee wangu. Akaanza:
Mwanamke; Sisi baba (sauti ya mtu mzima) limetutokea tatizo kubwa sana inakaribia miezi sita sasa, tumehangaika sana mpaka kwa waganga wa kienyeji huko, ndio tukaletwa kwa Sheikh Ali na mama ambae binti yake aliumwa akafanikiwa kuponeshwa kwa Sharrifu. Tumeongea na Sharreifu amesema alieifanyia hio kazi ya yule binti yupo Dar, alikuja tu hapa kwa kazi zake. Ndio katupa namba tuongee na wewe.
Sema tu mama; Mimi baba nimepoteza mwanagu wsa kunzaa mwenyewe, wa kiume, mtu mzima ana miaka 33, sio mtoto mdogo. Huyu mwanangu alikua na biashara zake hapa ikawa hayupo mbali kuoa, akapata maradhi kama ya kurukwa na akili, tukampelka hospitali haikusaidia, akawa anatoroka toroka nyumbani, haendi kwenye kazi zake, siku hio katoroka nyumbani ndio mpoaka leo hatujamuona. Sasa baba tunahotaji msaada wako, hatujuwai yu hai au kafa, tumemaliza Shinyanga, Mwanza, Tabora, Singida kumtafuta na kuhangaika kila sehemu, ndio tukaelekwa kwa Sharifu. Hivi nipo hapa Shinyanga lakini nimetokea Mwanza, nipo hapo lo wiki nzima.
Mimi;Upo hapo kwa nyumbani kwa Sharrifu?
Mama: Hapana baba, hua nakwenda tu kumsikiliza ndio mpaka leo kanipa namba yako, naomba baba tusaidie.
Mimi; Mama nimekusikia nimekuelewa, mtangukize Mwenyezi Mungu mbele. Nitakupa jibu mimi au Sharrufu, leo hii au kesho. Toa shaka.
Mama: baba hata ukiniambia nisubiri wiki, mimi nitasubiri, sina cha kufanya,mwanagu najua kwa ugonjwa ule anapata shida hajiujui hajitambui. Moyo wangu haukubali kua kafa baba.
Mimi; Usijali mama, nitakupigia. Kwaheri, usiwe na wasiwasi.
Nilikua nipo kazini na mzee lakini hakuna za maana ambazo zinanihusu sana mimi, nikamuaga mzeenikaenda nyumbani. Hata mke wangu kashangaa nimerudi mapema.
Wife: Vipi, kwema?
Mimi: kwema wacha nikoge kwanza nitakuelezea, wifa anafahamu nikiwa na jambo linanizonga, akaniwacha nikaingia kukoga nikabadili nguo nikatoka jje nikaenda kunywa juice kwanza.
Wife; Nikuletee kahawa?
Mimi; No, sio sasa hivi, mbona kimya? Wametoka na mwanao kamlilia bibi yake amchukue na bibi yule anavyo mdekeza nikaona isiwe kero aende nae tu.
Mimi; Si mama mwenyewe kamzowesha kwenda nae mizunguko yake?
Wife; Bira haswa, na imi napata kufanya yangu.
Mimi ; Nipo ofisini kwamgu.
Wife anajua nikiwa ofisini kwangu nyumbani sitaki kero kabisa, hata akija mtu wtanipigia simu, hawagingi mlango.
Nikachukua bakora nikaisimamisha mbele yangu, nikamwita Jini Bakora, akaja, tukaslimiana pale, nikamweleza kisa chote. Kanambia mwite Jini wa Arsis, mweleze. Mimi hio sio kazi yangu. lakini nikihitajika kwa lingine nitakuja.
Tukaagana, nikamwita jini 1, hua hachelewi kabisa, akaja dakika hio hio, siku hizi nikiwaita ofisini kwangu wanajua wapi watokee na wapi wakae, tuongee. Nikamweleza mwanzo mpka mwisho. Akasema ngoja nakuja nipe nusu saa. Akaondoka zake. Ile anaondoka natazama simu kama kuna mtu kanitafuta nikakuta miss call ya Sharrifu Ali. Nikapigia, baada ya kusalimiana.
Sharrifu Ali, yule mama kakupigia kanambia sasa hivim kasema utamjibu wewe au nitamjibu mimi. Sawa?
Mimi; Sawa, Sharrifu. Inabidi unisurbirie mpaka baadae au kesho nitakupigia, sijui tufanye nini, hii kesi ya polisi.
Sharrifu; Wamemaliza polisi zote, polisi wakijua kama jamaa aliwehuka wanakuwa hawaitilii mkazo sana. Kuna polisi Mwanza huko kamwabia "mama zungukeni majlala yote ya mwanza, watu namna hio wanapenda sehemu chafu chafu". Ndio hivyo mama akija kwangu anaia tu. Hata sijui tufanye nin, leo wiki hapa tunapiga kitabu na vijana wangu, ndi wife wangu akasema nikwambie, akanishauri nimpa namba yako mama yule aongee nawewe, nisamehe kwa hilo, ilikua nikujulishe kabla sijamwabia.
Mimi; Umefanya la maana Sharrufu, maana Sharrufu wala usijali.
Sharrifu: Kama si Anti yako hapa nisngempa namba wala nisingewambia, toka ulipoonambia hii kazi huifanyi, ni bahati tu ulikuepo lakini hufanyi tiba. Nikawa naogopa kukubesha mizigo, maana niyie vijana na kazi hizi wapi na wapi.
Mimi; Kweli mzee wangu, lakini tuombae Mwenyezi Mungu, tukaagana nikaenda kufanye mengine.
Kam nusu saa hivi, akaja yule jini lakini hakujitokea nilikua uani kwetu, nikaongpoza chumbani ikawa nimeingia nae akakaa sehemu yake.
Jini 1; Nimekuja na mama, nimwite?
Mimi: Mwite, kidogo mlango wa ofisini ukagongwa nikafungua akaingia mama yule jini. Tikaslaimina. Akaanza;
Jini2; Nimepata ujumbe wako na nimeufanyia kazi, tumeongea na Arsis kasema tukueleze tu nini cha kufanyika.
Mimi: Sema tu.
Jini e: Chukua kahawa ukae utulizane, nikueleze kwa kituo.
Nikaenda kuchukua kahawa jikoni, nikauta chupa nzima nikaingia nayo ofisini, nikawakuta wananisubiri/
Mimi: hya jamani nipeni habari.
Jini 2; Habari zjnuri sio mbaya, huyo kijana yupo hai lakini hajijui hajitambui, Arsis anasema atapatikana na huko aliko, kawekewa ulinzi na Arsis ili wasinedelee kumfanyia mambo ya kishirikina.
Mimi ; Yuko wapi?
Jini 2: Hilo atakufahamisha Arsis, Arsis kasema leo usiku uende kule mkaongee. Mimi alinipa kazi na akanambia nije kukufahamisha hilo, usiwe na wasiwasi lakini usiwaambie chochote watu wake mpaka ukishaongea na Arsys usiku.
Mimi' Sawa. kunalingine?
Jini 2: Ndiyo yapo kidogotu. Hii simba ni mamaboi ya kichawi, uchawi wa kishenzi kabisa, ndio maana wameniita mimi nikaifanye hii kazi. Mimi nimekwenda nimuona kijana, hali yake sio nzuri, wachawi ni watu wabaya sana. lakini, Arsis kasema hakuna wasiwasi, atapona kila kitu kwa muda mfupi sana, yeye anaanza kufanya kazi kuanzia ssa, wewe nenda usiku. Mimi nimemaliza;
Mimi; haya mwabieni nitakwenda.
Tukaagana wakaondoka.
Itaendelea.