Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Umenena vyema ukristo na uislamu ni Iman tofauti
Ila ktk imani ya kikristo wapo malaika walioasi. Wakristo tunaamini hivyo.
Ufunuo wa Yohana 12:7-9
[7]Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

[8]nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

[9]Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Kuhusu dini ni ipi au ni nini wakristo tunaamini hivi.
Yakobo 1:27
[27]Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
 
haya Lidafo, Etugrul Bey na waislam wengine tupeni msimamo wenu kuhusu malaika kwa ushahahidi wa Qur'an kama alivyotupa mambio kwa ushahidi wake wa Biblia.

Hizi elimu ndio kufunguana macho huku.
Simba.
 
safi sana,ila mkuu umesahau kitu kimoja muhimu hiyo aya inapatikana katika sura gani na aya ya ngapi?
Mkuu maneno haya siyo aya ya Qur'an. Haya ni maelezo na dua maarufu katika Hadithi za Mtume Muhammad (s.a.w.) na hutumika kwa ajili ya kutafuta kinga kutokana na madhara.
Yanapatikana katika vitabu vya Hadithi kama vile Sunan Abu Dawood na Sunan At-Tirmidhi. Hadithi inasema:

"Anas bin Malik (R.A.) amesema: Mtume (S.A.W.) alisema: ‘Mtu anayesema: Bismillahi alladhi la yadurru ma'a ismihi shay'un fil-ardi wala fissama'i wa huwa as-sami'ul-'alim mara tatu kila asubuhi, hatadhuriwa na kitu chochote mpaka jioni. Na anayesema hivyo mara tatu kila jioni, hatadhuriwa na kitu chochote mpaka asubuhi.’"

Sunan Abu Dawood
, 4/323; Sunan At-Tirmidhi, 5/464.
 
Tabaraka Allah.

Nilijua Sheikh wangu utaweka tafsiri ya kina.
Simba.
 
Mimi nashauri, kama msimamo wako ni kinyume na yeye au mimi au mwengine yeyote, mwekee ushahidi wako wa Qur'an badala ya kukubali tu kutokukubalina. Sasa kama unakubali tu bila kuweka ushahidi wako, hapo haiwi kukubaliana kutokukubaliana, hapo inakua umekubali ushahidi wake bila pingamizi.

Mjadala wa wawazi huu, kama hauna jibu lenye ushahidi kwa wakati huo, unaweza kuita Waislam wengine walete mistari yao kama nilivofanya mimi juu hapo kuhusu tafsiri.

Lengo ni sote kwenye uzi huu kufaidika kielimu. hatutafuti mshindi nani wala mshindwa nani.

Tukipata elimu sote tunaosoma hapa tunafaidika, kila mtu kivyake.
Simba.
 
Ndugu, Umesema ukibatizwa na kumfuata yesu una uzima wa milele, Je ukibatizwa na usimfuate yesu kwa maana wewe ni mkristo ila unazini, unadhulumu, unaua N.k utakuwa una nini ?
 
Ndugu, Umesema ukibatizwa na kumfuata yesu una uzima wa milele, Je ukibatizwa na usimfuate yesu kwa maana wewe ni mkristo ila unazini, unadhulumu, unaua N.k utakuwa una nini ?
Sheikh kwani Uislam unasemaje kuhusu kubatizwa?
Simba.
 
Sheikh kwani Uislam unasemaje kuhusu kubatizwa?
Simba.
Katika Uislamu, kubatizwa kama ilivyo katika Ukristo, hakutambuliwi kama sehemu ya ibada au utaratibu wa kuingia katika dini.
Katika Uislamu, mtu anaingia katika dini kwa kusema Shahada, tamko la imani ambalo linatamkwa "La ilaaha illallah, Muhammadur rasoolullah" (Hakuna mungu ila Allah, na Muhammad ni mtume wa Allah).
kwenye uislamu kuna kushika udhu tu ambacho ni kitendo cha kunawa baadhi ya sehemu za mwili kwa maji kitendo hiki ni lazima kabla ya sala na mtu huweza kushika udhu hata kama haendi kusali.
Tofauti na hivyo sijaona kubatizwa kukizungumzwa katika quran, Japo kuwa mtu anaweza uliza waislamu tunasema tunamwamini yesu(isa) na kwa mujibu wa biblia yesu alibatizwa MATHAYO 3:13-17 inasema yesu alibatizwa na yohana katika mto Yordani sasa kama tunamuamini mbona atubatizwi?
Jibu hapa ni kuwa waislamu tuna muamini yesu kama mtume wa Allah tu na tunawajibika kwa quran ambayo alipewa Mtume Muhammad s.a.w ambayo haijasema tubatizwe kwa maji marefu au mafupi sisi tumesisitizwa kuiishi shahada yetu.
 
Arsis kupitia simba naomba unijuze, kupata kipato imekuwa shida sana, ila masheikh wanasema natakiwa kusali sana maana hakuna anayeweza nisaidia zaidi Mungu na mimi mwenyewe kwa kuswali sana , maana nina vita kubwa
 
Nikawaambia haya kina dada, nyie jitayarisheni na sisi tunakwenda kujitayarisha kwangu kule..
H1; Haondoki mtu hapa, hata sisi tuna chumba chetu, tunajitayarisha kuondoka hapa, tupeni dakika 10 tu. Tufatane.

Mimi; Poa, mkiingia ndani humo mwambieni mhudumu atuletee kahawa wakati tunawangoja.
Wakaingia ndani, wakati wanaingia...
H2; Twendeni basi mkatukogeshe.
Mimi; Si mmesema hapa tuwape dakika 10 tu?
H1; Wewe nae mpaka tukufungikie, anagekua babako haambiwi mara mbili. twendeni tukanyanduane.
Swahiba; Astaghafirullah.
Mimi; Msisahau kumwambia mhudumu atuletee ahawa mbili.

Wakaingia zao ndani.
Swahiba; Si tunaweza kushuka beach wakati tunawangoja?
mimi; Sasa hivi huogopi vibwengo?
Swahiba; Siogelei hata kwa pesa huku. Natembea tembea tu mchangani.
Mimi; Ngoja basi kahawa ije.
Swahiba; Siendi tena. Kuna kitu nilikua nataka nikuulize lakini sikutaka kukuuliza mbele ya watu.
Mimi; Uliza tu.
Swahiba; Unajua mara ya mwisho ulipokuja hapa Unguja, tulikua hatujuani, lakini lile tatizo la yule binti lilivyokwisha Sheikh alikuwepo kwenye kikao, katiika kutuhadithia jina lako lilitajwa sana. wewe na Sheikh mmoja kutoka Tanga, Hata sheikh hamjui jina mpaka leo na kijana wa Kiarabu katokea wapi sijui, ulikua nae sana wewe. Lakini anaongea Kiswahili vizuri tu, sema Sheikh anasema unajua kua hiki Kiswahili cha Kiarabu...

... Ndugu yangu kile kisa kilituacha mdomo wazi Unguja nzima, Sheikh anahisi wewe ndio ulikua Master wa ile game mpaka binti akapatikana.
Mimi; Si alikuepo Sheikh wa Tanga.
Swahiba; Hilo mzee kalisema, na yule Sheikh wafiwa wote hawamjui, sio ndugu, jamaa wala rafiki. Bora wewe mama'ko anajulikana ni mtu wa karibu na wafiwa. na mkeo alikuepo. Kasema Sheikh, ulikua nao sana wale watu wawili.
Mimi; Mwarabu mgeni wangu, umetokea Msiba tuko nae. na Mzee yule mimi namfahamu, tumekutana kwenye boti akasema na yeye atakuja msibani kwa kua tunajuana.
Swahiba; Nipe kisa ilikuaje, maana wewe ulikuepo mwanza mwisho, mimi nimeyasikia tu kwa Sheikh.

Unajua mumewe yule mama mwenye mtoto yupo jela mpaka leo, halafu kuna jamaa alikua boss serikalini, na yeye yupo ndani mpaka leo, na wengine kama wawili watatu hivi sina uhakika...

...Yule mtoto wa kike, tulisikia alitoroshwa kimya kimya, yupo huko bara na mamake mpaka leo. Halafu yule jamaa wa serikalini katemeshwa mali zote kapewa yule mama amlee mwanae, maana mume ndio yupo jela, hata kesi zao hakuna anaezifatilia. Wamesuswa na watu wote. Simba usinifiche, kuna vitu unavijua sisi hatuvijui, maana hata Babangu kasema...
Mimi; Kasema nini?
kasema ' Mtazame swahiba yako pete anayovaa, sio ya kitoto ile na huwezi kumuona mtu yoyote kaivaa. Ina mambo makubwa ile. Nambie ukweli Simba.
Mimi; Mwamba usijitie wasiwasi kabisa.
Swahiba; haladu unajua Simba, yule mama ulivotoka nae ndani siku ile, alikua kama mtu ambae anauoga fulani hivi. Akatunyenyekea sana mpaka katusindikiza, unajua kasema siku nyingine tukienda tusiweke gari nje? Sasa Simba najiuliza, hawa kinadada wa Dar wamemjua mamako wakaasema yule ni kiboko, anahudhuria mpaka shughuki za vibuki lakini yeye hana kibuki. Hapo kuna maswali mengi.

Mimi; usiwe na shaka Swahiba, hata yule mama tulipokua ndani nikamtajia mamangu anamjua ni partner wao miaka, sema yeye hana kibuki, anamjua, ndio maana akatuwekea heshima.

Swahiba; Mimi bado akili haijaridhika. twende tukajitayarishe ku[iga misosi ya Kitalii.
Mimi; Mbona unaharaka sana, si tunawangoja kina dada watoke?

Swahiba; Imenitoka, nataka kuwahi kuongea na Meneja dili alilonambia la kazi za hapa.
Mimi; Si kakwambia mwenyewe, yule mtu wa misimamo, hata ukisahau yeye hasahau.
Swahiba, Mimi hata leo naweza kumuonesha game akiwa tayari.
mimi; Yule mpaka kakwambia ujue ana kitu mawazoni. Msikilize, umkumbushe mara kwa mara. Maana mimi si unajua leo nimeongezea siku tu, In sha Allah kesho bomba.
Swahiba; Saa ngapi hujasema.
Mimi; Hata mimi sijajua, lakini tukienda chumbani kwangu labda itakua nishapata taarifa, niliwaambia hapa hoteli wanifanyie booking ya ndege, nikitoka airport mie nashukia kazini kwanza. Tutajua tukienda chumbani kwangu.

Mijimama ya dar ikatoka.
H1; haya twendeni, bado mpo?

Tukaondoka tukaachana tulipofika karibu ya vyumba, wao wakaenda kushoto, sisi tukaenda moja kwa moja.

Nikafungua mlango wa chumba changu, nikamwambia swahiba kama unajmwagia maji jimwagie, hpa sioni bahasha yoyote ya ujumbe wangu wa safari, ngoja niende resepshen, wewe koga jifarague usiwe na shaka, mimi nakupa dakaika 30 hazikutoshi Mwamba?

Swahiba; Nyingi sana hizo dakika 10 tu zinanitosha.

Mimi; Wewe ukimaliza njoo pale resepshen, kuna sehemu ya kunywa kahawa pale, nitakua nakungoja pale, Usijali kadi ya mlango ninayo, wewe ukitoka funga tu mlango.

Swahiba; Poa.


Nikaenda resepshen.
Mimi; Aah Martha, leo boiss peke yako kote hapa?
Martha: leo Sunday na hakuna wageni wengi wakuja au kuondoka, staff wengi wanapumzika. Nikuhudumie nini Mr. Simba?
Mimi; Niliwaambia resepshen wanifanyie booking ya ndege kesho, sijaikuta note yoyote chumbani.

martha; Umetazama messages za simu yako? Siku hizi hakuna maticket kama zamani, wanakupa ticket numbar, ukija nayo hapa wanakuprintia boarding Pass.

Mimi; Ooh, ngoja nicheki, jinayo simu yangu.

Nikakuta miss calls kama ishirini, nikaenda kwenye messages, ya kwanza hio ya hoteli notification ya kuchukua boarding pass reception. Ya pili ya shirika la ndege, wana cnfirm safari yangu na maelezo nifike airport mapema, boardin time ni saa tano kamili. departure saa tano na dakika 20. Nikajua boarding time ndio hio hio derture time maana vindege vya unguja vodogo tu, abiria 20 au 25 tu, kuboard ni faster tu.

mimi; Martha nimeiona notification ya boarding pass, nikupe uni printie biarding pass? Akaitazama meseji kwenye simu yangu huku anaandika numbers, akanambia 3 minutes utapata boarding Pass. Nikamwambia nipo pale coffe table. Akasema; Sawa Mr. Simba nakuletea.

Nikaenda coffee table ile nakaa tu kaja mhudumu nikamwabia niletee fresh orange juice na sparkling water moja. Na martha akawa kishaniletea boarding pass. Hijapita muda, hata simu sijapiga kurudisha miss calls, Mwamba kaingia, kakoga yupo fresh. Nikamwabia kaa wewe sasa nisubiri, agiza chochote mimi nitasaini usijali. Ooh mwamba natakiwa niwe airpost kabla ya saa nne asubuhi, boarding ni saa tano kamili. Akanambia huo muda mzuri.

Nikaenda chumbani nikakoga faster, nikatoka nikaanza kupiga simu, kwanza ya wife.
Wife; Vipi huko, hutaki kurudi mume wangu? Tumekumiss kweli nyumbani, wanao wananisumbua huku. Dad wapi, dad wapi?

Mimi; hata mimi nawa miss sana.

Wife na mama hapa utafikiri mtoto wadogo, kila saa huyu anarudi lini, anarudi lini> Namwambia mpigie mwenyewe mwanao, labda kaoa huko Unguja. Nikacheke tu. Waambie wote nitawapigia baadae kidopo kuna mtu ananisubiri. Wife akachomeea, njaa kali huku.

Nikampigia Mzee, tukaongea kidogo; lini uanrudi kazi zinakusubiri au ushaoa huko Unguja?
Mimi: Wewe si ndio utakua wa kwanza kujua, unafikiri posa atanipelekea nani?

Mzee: Aah, wewe na babu yako siku hizi mna siri zenu, mnaweza kuozeshana bila sisi kujua. Mamako huyu ongea nae. Nikasalimiana na mama pale. Nikamwambia nimekutana na shoga yako mmoja anaitwa H1;

Mama; Huuyo basi huko kuna kupandisha vibuki, maana haendi Unguja huyo mpaka kuwe na shughuli za vibuki.
Mimi; Tumekutana hoteli niliofikia.
Mama; basi mwanangu umefikia Hoteli ya maboss huko, huyo hakai hoteli ndogo ndogo, hio lazima ya kitalii, huyo ana pesa kama njugu. Umejuje kama rafiki yangu huyo muhuni?

Mimi; katika kujulishana tu.

Mama; Wewe mwanagu nae, huyo humjui, na unampeleka mkeo na kumrudisha kila siku akiwa na kazi zake pale kwa BIn Sulum Kariakoo?

MImi; Nilikua simjui, ndio kanambia.
Mama: Unarudi lini, wanao wanakumiss huku.

imi; n shaa Allah kesho joni maana nakuja na ndege, nikifika kabla ya kuja nyumbani niutapita kazini, mzee akitoka narudi nae.

Mama; Okay. safari njema.

nikaona nyingine ilikua miss call ya hapahapa hoteli, nadhani walikua wananijulisha kuhusu booking ya ndege. Namba zingine sizijui, nikasema hizi baadae nitazipiga. Nikatoka nje.

Ile nafika coffe table Mwamba ananambia, twende hapo chini beach, Menejea ameleta maagizo twende pale, wote watakua pale.

...
 
Arsis kupitia simba naomba unijuze, kupata kipato imekuwa shida sana, ila masheikh wanasema natakiwa kusali sana maana hakuna anayeweza nisaidia zaidi Mungu na mimi mwenyewe kwa kuswali sana , maana nina vita kubwa
Pole sana.

Vita ipi ndugu yangu?
Simba.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…