Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Next episode pls
Tunamalizia mashetani ya Kibuki Unguja, halafu tutaingia vijini vya Kipemba huko Kojani, tukitoka hapo tutaelekea visiwa vya Comoros, huko Njuani, kwenye shina la mashetani ya Kibuki, yatatupeleka mpaka kwa wakuu wa Kabuki huko Japan.

Hivi vitu kama hujavishuhudia huwezi hata kuvifikiria.

Utajuaje kama mashetani ya kibuki ya wangazija ndio hayohayo ya kabuki wa Japan?
Simba.
 
Unampaka mara 1?,ama kama dozi flani hivi kwa siku labda kabla hajalala na pakikucha,kuna kunuia wakati wa hilo zoezi?
Akipandisha tu. majini ya kishetani na mapepo yanatoka mbio. Kama hajapandisha usimpake.

Elewa kua majini ambayo sio ya kishetani hayapandi kichwani kwa mtu, kabisa. Akija jini au pepo hata akijifanya mwema vipi lakini kapanda kichwani kwa mtu elewa kua huyo ni muongo tu, ni shetani.

Kila Mwenyezi mungu anapotujaalia kuendelea na hivi vionjo vya Arsis, tutaelewa kidogo kidogo tofauti za shetani na jini. Ni nyembamba sana kama unene wa unywele mmoja.
Simba.
 
Unampaka mara 1?,ama kama dozi flani hivi kwa siku labda kabla hajalala na pakikucha,kuna kunuia wakati wa hilo zoezi?
Ile kuchukua dizeli na kutaka kumpaka ni nia tosha kabisa, hakuna cha kunuia wala kusema. Kama unajua Qur'an unasema dua hii "Bismillahil-ladhi la yadurru ma'as-mihi shai'un fil-ardhi wa la fis-sama'i, wa Huwas-Sami'ul-'Alim".

Itafute maana yake kwenye mtandao.
Simba.
 
Unaweza pia kupunguza, ‘mungu akipenda’ una acha kabisa. Muhimu ni kubadili mtindo wa maisha.
Usipunguze, acha kabisa.

Ukitaka kufanya jambo lako jema lifanikiwe usiseme najaribu, fanya tu. Vikwazo na viunzi uviruke, ndio mafanikio. Ukisema unajaribu au unafanya nusu kwa nusu, sahau, usifanye kabisa.

Amua kwa nafsi yako au unaitaka njia ya Muumba wetu au unaitaka njia ya shetani.
Simba.
 
Hakuna cha ukiboko wala nini, mimi napenda kumsoma adui pia ili kujua nyendo zake na namna ya kumkabili.
Sheikh Mittoga, ndugu yangu kwa damu. Kwanini tufikie kwenye uadui? Tusifike kufikiriana hayo, ni roho ya kishetani hio. Mlaani shetani.

Nini killichoashria uadui kwenye uzi huu unapousoma?
Simba.
 
Simba, asikusumbuwe huyo, kaishiwa bando tu. Arsis naye kasema nini kuhusu huyo poyoyo, funguka.
Yaani napitia posts mpaka nacheka peke yangu. We bi FF ni mtata sana.

Punguza ukali, kua mpole. Arsis na wewe anakusifu sana, sio Sheikh Mittoga tu. Lakini mimi nakwambia poa (cool down) bi FF.
Simba.
 
Ifrit au shetani au jini au yupo kwa kazi na makusudio maalum ya Allah, ni kiumbe chake.

Cha kusoma na elimu kubwa sana ni majina, kuna siri ipi na Allah katuongoza kwenye qur'an kupitia mmoja kati ya Adam kua tusome majina aliofundisha.

Majina Sheikh wangu ni elimu kubwa sana, hakuna kisicho na jina. Tusichukulie juu juu tu.
Simba.
 
Nakusoma vizuri sana,
Swali lingine,nna kitu nimeweza kukigundua kwa muda mrefu sasa,nikipanga jambo kwa umakini sana na lenye tija napofikia kulianza tuu either linaharibika,au haliendi kwenye mafanikio,au linakufa kabisa,ama litaenda tararibu sana kwa case ya vitu vya maendeleo(kutoka mwezi/miezi mpaka miaka),hata upande wa kauli tuu pia nna hio kasumba.
 
Qur'an ipo wazi kwenye hilo;
Q 2:216. ... Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.216

Ukipata nafasi sikiliza mahojiano ya Kikeke na Assad, aliekua mkaguzi mkuu wa serikali.
Simba.
 


Umenikumbusha;

Q 26:88. Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana.88
89. Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi.89

Simba.
 
sasa mkuu hio dizeli unamaanisha mafuta ya gari anunue mapya kabisa sheli au aliyotumika atoe kidogo kwenye gari na hiyo dizeli anampakaje je,kichwani tu,usoni au mwili mzima.? na kama aliyepandisha ni mwanamke baadhi wana misitu ya nywele kichwani inakuwaje.?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…