Niliyoyashudia Morogoro sitasahau

Niliyoyashudia Morogoro sitasahau

jerryempire

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
5,866
Reaction score
10,163
Tarehe 26, mwezi wa 4 mwaka huu nilikwenda mkoa wa Morogoro kwaajili ya kumpatia tiba mgonjwa wangu ambae alinitaka niende kwake.

Asubuhi niliianza safari na kufika msamvu stendi mida ya saa 9,nakuja kupokelewa na mgeni wangu.Pale kwa mwenyeji wangu maeneo ya jirani, kulikuwa na sheli(jina kapuni)ambayo mmiliki wake alikuwa anaishi nyumba kama ya 5 kutoka sheli kwake.

Wakati nimefika kwa mwenyeji wangu mida ya jioni, niliwaona mbwa wakubwa mno wa 2 wakiwa ndani ya fensi baada ya kuulizia nikaambiwa wanaitwa german shephard lakini wakati huo kuna mbwa wengine 3 wao walikuwa wamefungwa kwa mujibu wa wenyeji wangu walisema wale mbwa huwa hawafunguliwagi nikawa na shauku kubwa ya kutaka kuwajua na hata kuwaona japo mimi na mbwa ni kama chui na paka.

Basi mida ya usiku huwa kuna mzee anaingia lindo nyumba ile na yeye ndo huwa anawalisha chakula cha usiku.

Muda mwingi huwa anapenda kukaa nje akijinywea zake kahawa basi nilimfata na kuongea nae mengi tu na kuwajua kuwa wale mbwa wanaitwa rock teller na kunambia kuwa thamani ya kila mmoja ni shilingi milioni 7.

Nilishangaa lakini kwa ukubwa wa maumbile yao na jinsi walivyo sikushangaa sana but nilikuja kuchoka baada ya kuambiwa kuwa huwa anawapa chakula ambacho ni nyama mpaka kilo 10 kwa wakati mmoja.

Sasa yule mzee kumbe alikua na tabia ya kuwapa kilo 6 mpka 7 hivyo wakawa hawashibi, sasa kuna siku kawapelekea msosi hawakushiba, ile anataka kuondoka wakamvuta shati na kumla mpaka wakambakisha kichwa tu.

Asubuhi Mwarabu anaamka anawakuta rock teller wako uani akapiga simu fasta polisi ndo wakaja wakawadunga sindano kumtafuta mlinzi kabaki macho tu, lakini kwa nguvu ya pesa ya Mwarabu aliwajengea nyumba familia ya marehemu na kusomesha watoto wake.

Usia wangu;
Tuangalie vya kufuga huwezi fuga simba ambae baadae atakuja kukuwinda wewe mwenyewe
 
hilo hapo
images%20(2).jpeg
images%20(1).jpeg
images.jpeg
 
Back
Top Bottom