Nchi inaitwa Germany sio germanWakuu mpo pouwa?
Miez miwili iliyopita nilikuwa na tour yangu binafsi nchini Ujerumani, safari yangu ilianzia ktk uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro airport hadi Dubai nikitumia Ethiopian airline.
baada ya kufika Dubai nilichukua air Berlin hadi uwanja wa kimataifa wa Frankfurt ujerumani
nilikaa mjini Frankfurt siku mbili kabla ya kupanda treni ya umeme hadi ktk mji uitwao Cologne (koln) ambapo nilikutana na ndugu yangu ambaye ni padre wa kanisa katoliki.
Nilichokiona huko ni kuwa watu wa kule wapo busy sana hawana hata sekunde moja ya kupoteza, wanachakarika sana yaani, vile vile sitasahau siku hiyo nikiwa natoka Frankfurt kwenda koln niliporwa Pesa kama dola 200 nilikuwa nimeziweka mfuko wa mbele wa shati kumbe kuna vibaka kama huku sema wapo more advanced
Mwenyeji wangu aliniambia kuwa vibaka na matapeli wapo sana tu
Siku moja tukasafiri hadi mjini Dortmund kumsabahi padre mmoja hivi mtanzania jina lake padre Mosha nilienjoy sana siku hiyo nilipelekwa hadi uwanja wa mpira ktk mechi ya Borrusia Dortmund ilikuwa ikicheza na timu iitwayo Hertha Berlin ktk uwanja uitwao signal iduna arena hapo mjini Dortmund
Nilimuona live Aubemyang aliekuwa mchezaji wa Dortmund kabla ya kuja Arsenal
Basi nilimaliza ziara yangu ya siku 15 huko German na nikarejea bongo wakati nikirudi nilitumia etihad aiways nikapita Amsterdam Uholanzi then tukapumzika kidgo safari ikaanza hadi Dubai baadae. Nikachukua Ethiopia airline hadi Kilimanjaro international airport
I enjoyed my tour.