Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,918
- 30,259
RAFIKI YANGU PROF. KAI KRESSE WA ZENTRUM MODERNER (ZMO) ORIENT, BERLIN, UJERUMANI
Vipi nilifika Ujermani kwenye taasisi kubwa ya utafiti iitwayo Zentrum Moderner Orient ni kisa kirefu na kinaanza na Prof. Ibrahim Noor Shariff.
Sauti ya Ujermani ilikuwa inataka kufanya kipindi katika Meza ya Duara kuzungumza kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 na walikuwa wamepanga jopo la Ahmed Rajab kutoka London, Dr. Harith Ghassany kutoka Washington DC, Prof. Ibrahim Noor Shariff kutoka Muscat na Saleh Feruzi Makamu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar akiwa visiwani.
Mwenyekiti ni Othman Miraji akiwa DW Bonn.
Prof. Ibrahim Noor Shariff akasema yeye hawezi kushiriki na akapendekeza jina langu.
Hawa washiriki wote mimi tukifahamiana ila Saleh Feruzi.
Mimi nilikuwa Tanga.
Hivi ndivyo nilivyoshiriki katika kipindi kile na kipindi hiki kikasababisha mimi kualikwa ZMO na Prof. Kai Kresse nifanye mhadhara mmoja na niandike mada moja.
Hii ilikuwa mwaka wa 2011 na ndiyo kwanza tumetoka katika uchaguzi wa 2010 uchaguzi ambao Zanzibar kama ilivyo kawaida uligubikwa na matatizo makubwa.
Katika kipindi kile kufupisha mambo mimi na Saleh Feruzi tulipambana sana.
Nadhani kule kwa Saleh Feruzi kutonifahamu ndiko labda kulikofanya kipindi hiki kipendeze sana kwani yeye hakuwa anategemea kutoka kwangu yale ambayo mimi nilikuwa nasema nikimkabili yeye.
Saleh Feruzi hakuwa amepata kukutana na mtu wa aina yangu na hakujua anikabili vipi ninapoeleza katika hsitoria ya CCM Zanzibar yale ambayo wengine wangeyakwepa.
Kipindi kilipokwenda hewani wasikilizaji wengi walivutiwa na jinsi nilivyokuwa naieleza CCM Zanzibar katika chaguzi zote walizoshiriki na kupata shida ya kupata ushindi unaoeleweka.
Wasikilizaji wengi wa DW Idhaa wa Kiswahili walioko nje ya Tanzania wakawa wanampigia simu Othman Miraj kutaka kunifahamu.
Katika hao walikuwa ZMO na Othman Miraji akawaunganisha ni mimi na hivi ndivyo nilivyoalikwa Ujerumani na Kai Kresse ambae akaja kuwa rafiki yangu.
Nilipanda Egypt Air ndege ya usiku hadi Cairo kisha kutoka Cairo ndege ya mchana hadi Berlin.
Kai Kresse alikuja uwanja wa ndege kunipokea.
Nakumbuka ilikuwa inanyesha mvua.
Bahati mbaya sana begi langu likawa halionekani.
Haikunishughulisha sana kwani nilichokuwa nakithamini ni laptop yangu nayo nilikuwanayo ndani ya ndege.
Huu ni moyo wangu siku zote safari zote nakuwanao mkononi ndani ya ndege.
Wakati tunatoka nje ya uwanja likatoka tangazo kuwa natafutwa Customs nikachukue mzigo wangu umeonekana.
Nakumbuka wakati tuko katika gari Kai ananipeleka waliponipangia nyumba sehemu inaitwa Wedding katika mazungumzo akaniuliza kama mimi ni mpenzi wa mpira.
Nikamwambia naipenda Liverpool.
Hapo akaniahadithia Berlin ilikuwaje Fainali ya Kombe la Vilabu Vya Ulaya Bayern Munich walipofungwa na Manchester United wakati Bayern walikuwa wakiongoza kwa magoli mawili.
Magoli yote yalirudi na wakaongezwa goli moja.
Kazi ya Ferguson Boys, Paul Scholes na wenzake.
Anasema siku ile mji mzima wa Berlin ulikuwa kimya umejiinamia.
Mazungumzo yetu yote tunazungumza Kiswahili na hakimpi shida hata kidogo.
Nilishangaa kidogo.
Akanishangaza aliponiambia kuwa mhadhara wangu wenye jina ''Baraza'' utakuwa kwa Kiswahili.
Mada yangu ilikuwa nimeiandika kwa Kiingereza.
Nimekaa ZMO kwa mwezi mzima na Kai Kresse alikuwa kila siku ananikagua ofisini kwangu kuangalia naendeleaje.
Alikuwa kanipangia siku mbili tu za kuja kazini Jumatatu na Alkhamisi.
Mimi nikawa nakuja siku zote isipokuwa Jumamosi na Jumapili.
Berlin ni katika miji migumu niliyopata kufika Ulaya.
Wajerumani si watu wenye kubeba sana tabasamu kwenye nyuso zao na hali ya mji ni hivyo tofauti na miji mingi ya Ulaya niliyopata kufika kama London, Paris, Amsterdam ambako kuna sehemu nyingi tu ambazo mtu anaweza kwenda na kuchanganyika na wenyeji.
Siku moja katika mazungumzo nilimuuliza Kai kuhusu historia ya Ujerumani.
Akaniambia inasomeshwa kama funzo watu wajifunze kutokana na yale yaliyopita hata kama ni machungu.
Kai anakuja sana Tanzania na kila akija atanitaarifu nami nitamfuata hotelini kwake.
Kila akija huwa hakosi kuja na zawadi ya kitabu kwangu.
Kai ni mwenyeji wa Dar es Salaam kiasi kuwa kuna wakati alipanga hoteli Sinza na wakati mwingine New Africa Hotel katikati ya Jiji.
Kote huko nilimfuata kumkagua na kufanya mazungumzo na yeye.
Nimefurahi kuwa Kai kaja kuhudhuria Kongamano la Kimataifa la Shaaban Robert na Kumbukizi zake MUM na nikapata bahati ya kuwaleta yeye na Prof. Ibrahim Noor Shariff Maktaba.
Kai Kresse alichukua muda mwingi sana kupitia kitabu baada ya kitabu katika Maktaba.
Picha ya kwanza Kai Kresse akiwa New Africa Hotel na picha ya Pili akiwa kwenye hoteli moja Sinza.
Picha ya tatu nikiwa Maktaba na wageni wangu na picha ya nne nikiwa na Kai Kresse ZMO, Berlin.