Niliyoyaona nchini German katika tour yangu

Wakuu mpo pouwa?
Miez miwili iliyopita nilikuwa na tour yangu binafsi nchini Ujerumani, safari yangu ilianzia ktk uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro airport hadi Dubai nikitumia Ethiopian airline.

baada ya kufika Dubai nilichukua air Berlin hadi uwanja wa kimataifa wa Frankfurt ujerumani
nilikaa mjini Frankfurt siku mbili kabla ya kupanda treni ya umeme hadi ktk mji uitwao Cologne (koln) ambapo nilikutana na ndugu yangu ambaye ni padre wa kanisa katoliki.

Nilichokiona huko ni kuwa watu wa kule wapo busy sana hawana hata sekunde moja ya kupoteza, wanachakarika sana yaani, vile vile sitasahau siku hiyo nikiwa natoka Frankfurt kwenda koln niliporwa Pesa kama dola 200 nilikuwa nimeziweka mfuko wa mbele wa shati kumbe kuna vibaka kama huku sema wapo more advanced

Mwenyeji wangu aliniambia kuwa vibaka na matapeli wapo sana tu

Siku moja tukasafiri hadi mjini Dortmund kumsabahi padre mmoja hivi mtanzania jina lake padre Mosha nilienjoy sana siku hiyo nilipelekwa hadi uwanja wa mpira ktk mechi ya Borrusia Dortmund ilikuwa ikicheza na timu iitwayo Hertha Berlin ktk uwanja uitwao signal iduna arena hapo mjini Dortmund

Nilimuona live Aubemyang aliekuwa mchezaji wa Dortmund kabla ya kuja Arsenal

Basi nilimaliza ziara yangu ya siku 15 huko German na nikarejea bongo wakati nikirudi nilitumia etihad aiways nikapita Amsterdam Uholanzi then tukapumzika kidgo safari ikaanza hadi Dubai baadae. Nikachukua Ethiopia airline hadi Kilimanjaro international airport
I enjoyed my tour.
Nchi inaitwa Germany sio german
 
Mkuu suala la ubize hata tz tuko bizee saaana!! ila ukiuliza busy for what, mbongo ataanza aisee mambo mengi kwelikweli!!! Ili hali hata family hana!! Ila ndo hivyo!!! Tuendelee kuwa busy
 
simulizi yako imeni kumbusha comedy ilikuwa inaitwa MIND YOUR LANGUAGE...mwalimu akasema kila mmoja aeleze likizo yake kaitumia vp
 
Unajua unapotoa maelezo yakaacha mashaka lazima watu wakuulize mwaswali na unatakiwa uyajibu vzr! Umeulizwa mbona hakuna ndege ya Ethiopian ya kutoka KIA mpaka Dubai? Kwa nini hamkupitia Addis Ababa ambapo ndio kwenye ngome ya Ethiopian? Ukajibu wewe ni mgeni na pengine mlipitia lakini hukujua! Sasa huoni hili jibu ni kichekesho? Hivi ndege imekuwa dala dala ambayo inaweza kupita kituoni bila mtu kujua? Huoni ukimweleza mtu aliyewahi kusafiri na ndege kupitia Addis Ababa atakucheka sana? Ina maana uliteremka kwenye ndege na kubadilisha nyingine huku umelala na hujui kinachoendelea?
Wajinga vs welevu, takwimu zinasemaje?
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom