Niliyoyaona Mumbai(Bombay)

Kwa uchafu umelenga hata zile hoteli kubwa unaweza pishana na mtu anajisaidia haja kubwa kwenye lango la kuingilia...
Pia kuna maeneo yana ombaomba balaa, ombaomba anakuganda haswa yaani akikufuata usipompa chochote hakuachi ataenda na wewe kama unatembea hata kama ni km5 hadi umpe chochote...
Makazi kiukweli yanachangamoto huwezi jua makazi ya proffesor au ya mtu ambae hajaenda shule, kuna maeneo unaweza mkuta prof anaishi chumba ambacho store ina uhafadhali....
Vyakula vinapilipili sana, hadi pipi utakuta ina pilipili...
 

Hospitali za Apollo sio za kitabibu bali ni kitengo maalum cha utalii, wanaendesha kitu kinaitwa "Medical tourism", kaa chonjo!!
 
Hizo honi hapa bongo naweza zipata dukani?? nataka nisumbuane na shemeji zangu wa kimakonde mahuta huku
Mkuu hamisj hivi basi la Mahuta kupitia Kisangara bado lipo??duuuh huko utawasumbua sana Wamakonde dadeki...hasa pale Newala mjini karibu na Posta kwa Braza Adam...Inapikwa sambusa moja tamu sana!Msimu wa mihogo kila mtu na kipisi cha muhogo mdomoni....Daaah Newala kuchereeeee
 
INDIA umetoka wiki iliyopita thread unaanzisha leo baada ya narendra modi kuhutubia mie nawaambia hivi.... mtaisoma namba na mikataba imeshasainiwa tufanye kazi, tujenge nchi chadema hamuwezi chukua nchi kwa thread zisizokuwa na kichwa wala miguu kama hizi
 
Vipi, uliweza kuonana na Amita Bachani na Misuni Chakalaboti...?
 
Ungeangalia vizuri ungegundua wako location wanaigiza muvi tu.
 
Uko sahihi.... kwa usafi sasa wanajitahidi... miaka ya 2008 nilienda kule ulikuwa ukitoka hotel kwenda nje kutembea hata kama ni 10mis ... ukirudi lazima uoge.... kulikuwa ni kuchafu kweli kweli.... kwa sasa naona kuna paving blocks na sehem nyingi za uchafu wanazisafisha....
 
Mwenye kujua kidogo kuhusu jiji la #Bangalore anidadavulie
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwa namba 1 na 2. Uko sahihi kabisa. Ila kwa namba 3 sijui maana sijabahatika kuingia kwenye hiyo migahawa uliyosema. Mimi pia nilikuwa huko mwaka jana. Nitarudi hapa jukwaani kuongezea mkuu...good for memory!
 
Mumbai ni kusafi ukilinganisha na Kolkata. Magari ni mengi lakini hukuti ajali kama kwetu. Heshima ya uhindini huwezi ipata popote, hebu fikiria mtoto anamwogopa baba utadhani ni malaika. Bikra uhindini ni jambo lenye tija. Ingawa uchafu, kutema mate ovyo, kukojoa barabarani hata kama Samora Avenue ni jambo la kawaida na watoto wa kiume kwenda kujifunza au kupunguza uhanga kwa machangu ni kawaida.
 
Uhanga ndo nini?
 
Sioni maana kuwadiscuss wahindi. Watu wajaabu sana wale. Nimetembea nchi nyingi na kukaa marekani kidogo lakni india naomba Mungu nisikanyage,ptuu!
 
Wanathamini sana bikra.?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…