Niliyoyaona Mumbai(Bombay)

Niliyoyaona Mumbai(Bombay)

Nimeamini kumbe jamiiforum ina wahindi tena wengi
 
Halafu mbona wanaoenda huko kwa wazungu huwa hawaji na mabaya ya huko muda wote husifia tu.
 
Wadau wikiiliyopita nilibahatika kwenda matembezi ya wiki moja nchini India Nilifikia katka jiji la Mumbai. kama ilivyo kawaida sehemu yeyote ukifika kwa mara ya kwanza lazima kuna mambo kadhaa kama si yote yatakuwa ni mageni kwako. Yafuatayo ni baadhi ya yale niliyo yashuhudia huko Mumbai.

(1) Foleni ya magari na Pikipiki Sijawahi katika maisha yangu kudhani hata siku moja kama kuna sehemu kunawezakuwepo na msongamano wa magari na pikipiki kama ilivyo mumbai

(2) Kelele za honi za magari na pikipiki nadhani kuna maeneo india kama chombo chako cha moto hakina honi huwezi kuendesha Ninaposema kelele za honi ni kelele kweli huwezi amini pikipiki imefungwa honi ya gari

(3) Uchafu jamani ukweli ni kwamba hawa ndugu zetu ni wachafu Ukiingia kwenye mighahawa hii ya hali ya chini kwakweli kama una kinyaa huwezi kula. Nimambo mengi sana nimejionea mwenyewe huko kwa wenzetu lakini sio rahisi kuyaeleza yote hapa.

Mwingine aliewahi fika huko kwa wadosi amwage hapa alichojifunza. Sikunyingine nitaelezea nilichofahamu kuhusu zile Hospitali maaarufu za Appolo Nawasilisha
Huko uchafu ndio kwao ila kama Dar tu kuna maeneo ya wenye nazo kusafi sana
 
Nasikia huko kuna chawa wa kwenye nywele ambao ili kumuua lazima utumie nyundo, uliwaona?
 
Back
Top Bottom