Niliyo yaona Agakhan Hospital | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niliyo yaona Agakhan Hospital

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MONTESQUIEU, Feb 2, 2011.

 1. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani mie si mwendaji sana wa hospital ya agakhani.
  Lakini kwa haya niliyo yaona kwa mara chache ninazoenda kutibiwa pale yananikera sana.
  Labda miye sina bahati.

  Siku ya kwanza nimeenda pale nilikaa zaidi ya masaa manne na nusu sijatibiwa.

  Skuingine nimekaa karibu siku nzima naangaika na matibabu.

  Ya jana sasa ndiyo kali kabisa,

  nimeenda na mtoto akiwa anatapika na kuumwa tumbo vibaya sana.
  nimefika pale saa 12 .30 hadi saa tatu ndio nikamuona dr.
  Dr mwenyewe hana hata mpango na hao wagonjwa.
  kakaa mlangoni anakuuliza unaumwa nini mbele ya wagonjwa wenzako .
  Kachukua kalatasi kaandika vipimo haya nenda kapime

  hata hujamuelezea vizuri ajue ni kipi hasa ambacho unatakiwa kupima.

  Hadi inafika saa nne mtoto hajahudumiwa na dalili za kuhudumiwa mapema hazipo.

  Kwa kweli nikaamua kuondoka na kumpeleka mtoto hospital nyingine ambapo tulipata huduma baada ya saa tukawa tumeondoka.

  Nilicho kiona pale:

  System yao inausumbufu sana
  Wahudumu hawana utu ni wajeuri na wana nyodo sana
  Ma dr wenyewe wapo pale kimaslahi zaidi na sikutoa huduma kwa wagonjwa, vichwa vyao viko juu juu!
  Na ukiwaangalia wengi wao hawana uzooefu sana
  Au wametoka shule juzi au hawajui ethics za kazi yao.

  Agakhani
  Uongozi haulioni hili?
  Cjui labda mie ndio nimeona hivyo but inakera sana labda je wenzangu mnao tibiwa pale vipi au mie ninabahati mbaya siku ninazoenda ndio zinakuwa hivyo?
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Unayoyasema yana ukweli kwa akisi fulani. hata mimi na familia huwa tunatibiwa hapo ingawa hilo la Dr wa watoto sijalishuhudia lakini wahudumu wake ni jeuri sana na wala hawana habari ya customer care.
  Nadhani tatizo ni kwua wengi wa tunaoenda pale tunatumia bima za afya hivyo wahudumu na wafanyakazi wengine wanakuwa hawana mwanya wa kupata kitu kidogo kutoka kwa wagonjwa
   
 3. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ilikuwa emergency alikuwa c doctor wa watoto
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hii nchi kila kona uozo
   
 5. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Nilikuwa pale wiki mbili zilizopita na nikastaajabu kukuta kulikuwa na choo kimoja tu kilichokuwa kinafanya kazi kwa ajili ya wanawake na wanaume cha wagonjwa wa nje. Pia usafi wa choo chenyewe ulikuwa unasikitisha sana ni bora hata vile vya uwanja wa taifa.
   
 6. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tufanyeje sasa jamani?kwani khalini mbaya sana
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tena wale jamaa wa emmergence ndo kiboko, wanakufanyia visa ili ukate kidogodogo... wanasahau kuwa siku hizi hospital ziko nyingi. Nina hakika uongozi wa agalhan usipolifanyia kazi hili watakosa 'wateja' muda si mrefu
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Aisee yani nitoe hela yangu halafu huduma mbovu nachapa makofii madk na manesi
   
 9. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapo unaumwa na hiyo nguvu utaitoa wapi mumie?
  Halafu serikali utaikimbia vp?
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sasa ndugu yangu siku ya kwanza, ya pili uozo ni ule ule lakini ukaamua kwenda tena kwa mara ya tatu!!!
  hata hivyo pole sana.
  Mimi nilifkiri hospital za gharama kama hizo hakuna mambo ya ki"mwananyamala na ki'amana' kumbe hata huko Aghakhan yapo!
   
 11. elimumali

  elimumali Senior Member

  #11
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Haya nimeyaona pia katika eneo hilo. Inasikitisha sana sehemu ya emergence ambako ndio huduma inatakiwa iwe ya haraka na uhakika! Wana JF tusiishie hapa, haya yaandikwe magezetini ili kuuamsha uongozi mzima wa Aga Khan. Hii ni Hospitali tunayoitegemea sana sisi wafanyakazi, inabidi tuwasaidie waboreshe huduma. Ili kuwasaidia, tuweke hadharani kasoro zao tusiandikiane humu tu. Wanahabari, p'se take action mkaichunguze hosp hii.
   
 12. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Siku nyingine ukienda na mgonjwa mwenye hali mbaya elekea moja kwa moja emergency room. Labda madaktari walikuwa wanawashughulikia wenye hali mbaya zaidi ya hapo. Hospitali zote duniani hakuna ambapo kuna express services, you have to wait, first in first out.
   
 13. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu nilidhani labda cku hizo zote wanapitiwa mh sasa nimeona hawa ndiyo kawaidayao
   
 14. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si bora uwe unaijua hiyo emergence room ndugu, mie ckuona hata mgonjwa mwingine pale ni usumbufu tu nenda rudi no maelekezo mazuri, nikukudharau tu na kukupuuza vile umewafuata
   
 15. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama wamo humu ni bora watusaidie kusafisha huu uozo hapo agakhani. mamabo yapo kienyeji sana
   
 16. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #16
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Bora Agha Khan....embu jaribu mwananyamala au Temeke hospital
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  kwa nini unalinganisha private hosp and public state owned? tatizo kubwa la aga khan ni racism and classification. kama si mhindi au kwenye fail haionyeshi kuwa unafanya kazi diplomatic mission, BOT na mashirika yanayofanana nayo. Please don't dare going to aga khan, you will only be frustrated.
   
 18. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huu uozo unaanzia mamlaka za juu. Viongozi wote wangekuwa wawajibikajia kama mama tibaijuka,magufuri,dr slaa,mwakyembe nazani uwajibishaji ungeshafanyika siku nyingi. Lakini kwakuwa hatuna uwajibikaji hata ma dr wanafanya watakavyo bila kuwajibishwa!! Hii ndo danganyika yetu
   
 19. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii kweli kabisa!
   
 20. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Jamani Agakhan pale hapafai,
  Ile hospital jamani kwanza ile process ya kujaziwa form (medical form) ili uende kuchukua queue ni issue, yaani mpaka usainishwe kwa kidole gumba.
  Pili hakuna uangalifu wowote kwa wagonjwa, yaani manesi hawajali (ikimaanisha wako busy sana)
  Tatu madokta pia wako busy tena ni mithili ya Ndodi, ile attentiveness ya kumsikiliza na kutumia sychology kubaini tatizo la mgonjwa nalo ni issue.
  The main source ya problem hapa ni UHINDI kukithiri, tazama wajapo wahindi pale wanaongea kihindi na kueleweshana tena kwa upendo sana, yaani credit pating patients hawathaminiwi kabisa na agakhan. Na huu uozo unaanzia kwa CEO wa pale, Director of medicine haelewani na madokta wenzake, manesi ndo usiseme.
  Kama unatatizo la watoto kuna daktari alikuwepo zamani agakhan anaitwa Yohana, ana dispensary yake pale ELIA COMPLEX. Ni dr mzuri saana kwa watoto na yupo nao in a friendlier manner. Tena anatibu pia hata kwa medical treatment card.
  POLE KWA YALIYOKUKUTA, hawafai wale nawajua vizuri saaana.
   
Loading...