Aiseee juzi nilipita maeneo ya Mbagala pale karibu na kituo cha daladala cha Rangi tatu. Daaah huku barabarani hii mitaro ina maji yametuama mpaka yamekuwa meusiiii na yanatoa harufu mbaya kwelikweli, alafu jirani tu kuna mama ntilie, kuna watu wanauza matunda na wengine sijui mitumba na chipsi yanii nilishangaa mno.Mkataa kwao mtumwa.. wewe unatuponda wakati ndege zinafululiza kuja bara na visiwani wazungu wanapagawa na bongo hii hii chafu..kila mtu ashinde mechi zake tulipo leo ni pazuri kuliko Jana..au nasema uongo ndugu zangu?
Usitetee ujinga mkuu, Dar ni chafu na inatia kinyaa.. Mara nyingine bora hata tunaoishi mikoani.Aisee nimeishia tu kuguna Yani unavyo ponda Kama sio kwenu ndio Mana katika story zako zako hujazungumzia hata nyumbani kwenu inamana hujafikia kwenu umeishia hotel nilivyo kuelewa Mimi ni kwamba unatusimulia Kama umefika ulaya we tuache na Tanzania yetu kaishi ulaya
Tatizo hujawahi kufika Marekani ,ungemuuliza na Harlem,Manhattan jeKuna rafiki yangu mmarekani aliwahi kaniambia Mnawezaje kuishi sehemu mko congested namna hii
Ni bora na wewe umeliona hili... aisee ile ni aibu sana, na kama wale wachuuzi wanatoa ushuru na hali iko vile wana haki ya kugoma kutoaMitaro hiyo ni michafu zaidi ya miaka kumi na maeneo hayo wapo watendaji wanakusanya ushuru na migambo wanatumwa kukamatwa wamachinga bila kujali kufanya usafi, kupanua eneo la kufanyia biashara ili kuepuka ajali huko askari wa trafiki wakihangaika kuongoza magari yasiyo na nafasi yoyote ya kupeana ili kupishana. Mbagala Rangi Tatu ni AIBU ya mwaka.
Wazungu wanapagawa na uchafu.Mkataa kwao mtumwa.. wewe unatuponda wakati ndege zinafululiza kuja bara na visiwani wazungu wanapagawa na bongo hii hii chafu..kila mtu ashinde mechi zake tulipo leo ni pazuri kuliko Jana..au nasema uongo ndugu zangu?
Kuna rafiki yangu mmarekani aliwahi kaniambia Mnawezaje kuishi sehemu mko congested namna hii
Unajua hizo nchi unazozisifia zilipata Uhuru lini? Na tz ilipata Uhuru lini? Ukijua Hilo utaelewa kitu
Sio lazima kuishi kama wao inawezekana tunavyoishi kwa msongamano ni kivutio tosha kwa nchi nyingine kuiga wakidhani ndo utamaduni wetuKwetu Mwanza. Nitapaongelea siku ingine. Lengo siyo kujionesha, ama kwamba napachukia nyumbani. TANZANIA NI KWETU. LENGO LANGU NI KWAMBA TUNATAKIWA KUJITATHMINI. KUDHANI TUMEFIKA KUNATUPOTOSHA.