Nilivyomhamisha mtaa kwa siku saba jirani yangu mjeuri

Habari zenu.

Kuna kabila moja kanda ya ziwa wakiwa jirani zako maugomvi hayaishi. Mara kakuibia mpaka, mara ajitape yeye ni tajiri sijui nini sijui nini.

Jirani yangu huyu ana tuvisenti twake akajifanya ana jeuri sana siku moja akaniambie we naweza kukuhamisha mtaa na mimi nikamwambia huwezi nitakuhamisha wewe.

Siku moja moja nilikuwa safari ya kikazi mkoa, nikaongea na rafiki yangu ana kandarasi ya kuzoa taka mtaani kutumia yale malori mabovu.

Tulichofanya sasa, gari ilikusanya taka mitaa yote ilipofika mbele ya nyumba ya Mr Misifa dereva akalizima na kufungua bonet kana kwamba limeharibika. Gari ilikaa pale wiki nzima na taka zake dereva anajifanya anatengeneza na ni msimu wa masika.

Ile harufu jamaa alihama nyumba kabisa mpaka siku gari ilipotoka, ndani ya wiki
Kuelezana kuhamishana mtaa, mlianzaje?

Yawezekana wewe mkuu ndiyo mkorofi!

Ona sasa, ulivyoenda kuswendeka taka mlangoni pa mwenzako, hapo nani mkorofi?

Sasa alivyokimbia hizo taka na kurejea, ulienda kumkumbusha ubishani wenu kwamba yeye ameweza kukimbia mtaa na wewe ndiye uliyemchomekea jalala na kwamba wewe ndiye mshindi?
 
Back
Top Bottom