Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Mkuu nipe list ya stori zilizowahi kukimbiza humu JF hata za zaman before ile ya KHUMBU maana zamani nilikuwa sifatili sasa huu wa PAUL naona speed yake ya kuandika imeanza kuwa na mashaka.

Pia uniambie nyuzi,hizo zinapatikana jukwa lini.

Asante
Kuna mtu anaitwa Kitoabu sikumbuki majina ya nyuzi ila ziko 2 na zote ni za moto sanaa kuhusiana na issue zake za uchimbaji wa madini
 
Huyu jamaa mwenye 'siredi' naona anachungulia uzi wake kwa mbali na kusepa.

Wajuaji wamemfukuza na vijiswali visivyokuwa na kichwa wala miguu.
Hii ni hadithi kama hadithi nyingine...sio lazima iwe kweli kama ripoti ya mahakamani.

Muhimu inakidhi vigezo(kufurahisha na kuelimisha)
Keagan Paul rudi hapa chap na umalizie huu mtanange.
Mkuu wewe kama upo akilini mwangu. JITU LINAKUJA KUPINGA KILA KITU UTADHANI LIMELIPIA HII SIMULIZI.

DAH NIMEUMIA SANA KUKOSA MUENDELEZO WA HII SIMULIZI.

HUMU JF HAKUNA SIMULIZI ZINAZOSISIMUA KAMA ZA SOUTH AFRICA. ILE NDIO ULAYA YETU MKUU KWA HAPA AFRICA.
 
Tatizo la watu humu JF wanapenda kusikia kile wanachotaka kusikia. Mtu ukiwa na mawazo kinzani kidogo japo ya kuwasaidia wanakuona kama umekuja kuharibu stori wakati hayo mawazo huenda yakawasaidia vijana ambao wengependa kujaribu bahati zao nje ya nchi. Story ya bwana Keagan Paul ni nzuri sana na inatoa darasa kwa vijana wenye ndoto za kutaka kusaka maisha nje.

Tatizo kuna details ambazo kuna watu humu huenda wakazichukua kama zilivyo bila kuchanganya na za kwao wakajikuta matatani. Naweza kusema bwana Keagan alikuwa na bahati sana tena sana, nadhani waliokaa South Africa watakubaliana na mimi kuwa alikuwa na bahati sana. Kitendo cha kuishi bila permit halafu unajiachia hivyo ni bahati sana kusurvive.

Kwa hiyo vijana wale mnaotaka kwenda huko muwe makini, bwana Keagan kama aliweza kujiachia bila permit msidhani maisha ndio yako hivyo, utadakwa dakika moja tu na kupelekwa sehemu inaitwa Lindela kusubiria kuwa deported. Kama nilivyosema kitendo cha kusafiri kwenda Lesotho wakati viza imeexpire ni bahati ya mtende na pia nampongeza sana kwa huo ujasiri.

Viza ikiexpire ukiwa ndani ya nchi ni kesi kubwa sana halafu akaamua kusafiri kwenda nchi nyingine wakati anajua hata kibali cha kuwemo nchi husika hana, huo ni ujasiri mkubwa sana na nachelea kumpa pongezi maana alikuwa kama anajiweka kwenye mazingira ya kurahisisha ukamatwaji wake.

Kwanza najiuliza walifikaje boarder ya Lesotho bila kukutana na roadblock hata moja na kukaguliwa ID zao? Pili yule immigration officer wa upande wa South Africa aligongaje exit stamp bila kumkamatisha kwa kosa la kuishi nchini illegally, najua amesema aliweka rand 300 kwenye passport.

Haya wakati wa kurudi aliwezaje kuingia tena SA wakati viza ilishaexpire? Bwana Keagan ukipata muda naomba uelezee kidogo kuhusu issue ya kutoka na kuingia tena South Africa wakati viza imeisha ili vijana wajifunze maana kuna wengine wanaweza kudhani kuishi bila vibali South Africa sio tatizo wakati ni tatizo kubwa sana linaloweza kuwapeleka jela.

Viza ikiexpire kisheria huwezi kurenew ukiwa ndani ya ardhi ya South africa hata kama unatoka SADC lazima utoke nje, na utapata misukosuko sana.
Bado tunaisubulia ile uliyoikatisha konda msafi
 
Nobody would like to read a plagiarized story, one that was once posted here before. I lost interest in his story after learning that plus the key points his missed as pinpointed by Honorable Konda msafi.
 
Ilipoishia.....

Nywele za Tsheispo zilikuwa zimeangukia mgongoni, chuchu saa sita oclock, guu sasa ndio nilichoka asee, guu nilidhani ni paja la mange kimambi, nikasema hapa keagan lazima leo nimueleze hisia zangu, baada ya kufika pale akesema mbona unaniangalia sana, nikamwambia hapana umependeza sana akacheeka huku tukiongozana kwenda restaurant .

Sasa endelea...

Tulipofika restaurant niliagiza viazi vya kukaanga na kuku Tsheispo yeye aliagiza kuku na juisi basi tulikula weee hadi pale muumini mmoja alipotufata kua tunaitwa na pastor! Tuliondoka na kurudi kanisani nilifurahi sana maana Tsheispo ndie alilipa bili hivo akiba yangu ilibaki salama.

Tulirudi kanisani pastor alisema tujiandae twende tour kwenye national park moja inaitwa Sehlabathebe National Park. Basi tujiandaa na kupanda coaster ambayo ilitumia masaa matatu kufika. Tulienjoy hadi jioni na kurudi pale kanisani tulilala mapema ili asubuhi tuanze safari ya kurudi south.

Sasa tulipofika pale boda ya kuingia south ndo kilitokea kizazaa. Askari wa migration walikua wakali kama wamekula pilipili za mto ruvu hawakutaka kucheka na kima kabisa siku hiyo ndo nilijuta kuwajua makaburu. Waligoma kua siwezi kuingia south maana permit yangu ilikua imeshaisha muda dah! Nilipagawa sana sikujua nifanyeje. Wale wenzangu waliruhusiwa kuondoka, waliondoka na kuniacha pale peke yangu tena chini ya ulinzi mkali kama wa mwendazake! aisee nililia sana nilipojua sitamkula Tsheispo baadae wale askari walinipeleka mahabusu.

Kesho yake nilitakiwa kupelekwa mahakamani lakini huwezi amini kolichotokea askari mmoja alikuja na kuniita kwa nguvu KEEGAN PAULO niliitika kwa uoga naam afande! Yule kaburu alinikata kibao akasema we nyani nikikuita itika Sir nipo Sir. Hilo neno Sir lilimaanisha bwana mkubwa. Basi bwana niliitika kama alivoniekeza. Alitabasamu na kusema njo unifuate nilitolewa nje wakati tunatoka nje nilishangaa kusikia mtu ananiita jina langu kabisa la Keegan Bashite nikazuga kama sijasikia. Mara akanigusa bega na kuniita kwa nguvu we Keegan amka.

Nilishituka sana kumbe nilikua naota. Aisee kumbe aliekua akiita ni Dada wa kazi! alimua akiniamsha nikale. Aisee ndoto za mchana mbaya nilikua nshafika south kimasikhara! Kumbe toka episode ya kwanza nilikua naota huku nakoroma kama jenereta bovu!! Lakini tuache utani Kanya alikua na tako balaa. Ngoja ninywe kiroba nilale nimechoka type. Mwe!!!!..

Mwisho

" jina langu kabisa la Keegan Bashite"

Umejua kunichekesha
 
Back
Top Bottom