rabson john
Member
- Jan 22, 2020
- 27
- 10
Sehem ya kumi vpWakuu leo naomba kuleta Story yangu ya kweli ya jinsi nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu kule wala mtu wa kunipokea.
Ukweli kuna wakati ilifika nilichoka sana maisha ya hapa nyumbani, ilikuwa Mwaka 2014, nilikuwa napitia changamoto nyingi za maisha hasa katika familia. Ukweli akili ilikuwa imechoka sana ilisababishwa na kutokuwa na ajira muda mrefu.
Hata baadhi ya watu sikuwa napenda kukutana nao sana. Nikajiuliza kwani Maisha ni hapa tu nyumbani? kwani hakuna sehemu nyengine? Nikajisemea labda sikuandikiwa kutoboa hapa nyumbani ngoja nikajaribu bahati yangu sehemu nyengine.
Kabla ya kufanya maamuzi ya kwenda South Africa, Kwanza niliwaza kujaribu bahati yangu Marekani, nina ndugu kama watatu huko. Nikamcheki ndugu yangu mmoja akanitumia Invitation Letter. Nikaanza kupambana pale Ubalozini. Nilifika kwenye Usahili lakini nilikosa VISA.