Nilivyofurahia Bilicanas kuvunjwa

Nilivyofurahia Bilicanas kuvunjwa

kukumdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2011
Posts
2,892
Reaction score
2,803
Wakati club hii kongwe ilivyokuwa inaharibiwa mimi nilikuwa nafanya biashara ya chips pembezoni ya club. Kwakweli nilikuwa naingiza sio chini ya laki kila siku ya club.

Binafsi nilikuwa simpendi Mbowe kwa sababu nilihisi ni mwizi tu hivyo wakati club yake inaharibiwa nilifurai sana moyoni nikajua jizi limekamatwa.

Nilikuwa nina mawazo finyu kwasababu sikujua kuendelea kuwepo kwa club ile ndio ilikuwa maendeleo ya biashara yangu.

Sasa hivi biashara nimefunga na hali yangu mbaya sana kiuchumi na nikimuangalia Mbowe yuko vizuri tu.

Sasa hivi natamani bills irudi tu kama Zamani. Nimegundua wivu ni mbaya sana.

Unaweza hisi mwenzako akifilisika wewe ndio unapanda kumbe yeye ndio anaekufanya upate kipato bila kujijua.

Bora mbowe anisamehe na waliovunja club wapotee kabisa.
 
Wakati club hii kongwe ilivyokuwa inaharibiwa mimi nilikuwa nafanya biashara ya chips pembezoni ya club. Kwakweli nilikuwa naingiza sio chini ya laki Lila siku ya club. Binafsi nilikuwa simpendi mbowe kwa sababu nilihisi ni Mwizi tu hivyo wakati club yake inaharibiwa nilifurai sana moyoni nikajua jizi limekamatwa. Nilikuwa namawazo finyu kwasababu sikujua kuendelea kuwepo kwa club ile ndio ilikuwa maendeleo ya biashara yangu. Sasaivi biashara nimefunga na haliyangu mbaya sana kiuchumi na nikimuangalia mbowe yuko vizuri tu. Saivi natamani bills irudi tu kama Zamani. Nimegundua wivu ni mbaya sana. Unaweza hisi mwenzako akifilisika wewe ndio unapanda kumbe yeye ndio anaekufanya upate kipato bila kujijua. Bora mbowe anisamehe na waliovunja club wapotee kabisa.
Vipi kwa wazazi ambao watoto wao wamekuwa mateja kwa sababu kunywa madawa ya kulevya kwenye hiyo club?

Nao washangilie tu kwa sababu wewe ulikuwa unaingiza laki 2?
 
Roho ya korosho inakusumbua. Pole sana.

Wakati club hii kongwe ilivyokuwa inaharibiwa mimi nilikuwa nafanya biashara ya chips pembezoni ya club. Kwakweli nilikuwa naingiza sio chini ya laki Lila siku ya club. Binafsi nilikuwa simpendi mbowe kwa sababu nilihisi ni Mwizi tu hivyo wakati club yake inaharibiwa nilifurai sana moyoni nikajua jizi limekamatwa. Nilikuwa namawazo finyu kwasababu sikujua kuendelea kuwepo kwa club ile ndio ilikuwa maendeleo ya biashara yangu. Sasaivi biashara nimefunga na haliyangu mbaya sana kiuchumi na nikimuangalia mbowe yuko vizuri tu. Saivi natamani bills irudi tu kama Zamani. Nimegundua wivu ni mbaya sana. Unaweza hisi mwenzako akifilisika wewe ndio unapanda kumbe yeye ndio anaekufanya upate kipato bila kujijua. Bora mbowe anisamehe na waliovunja club wapotee kabisa.
 
nina kumbukumbu nzuri sana kuhusu club bilicanas. ndio night club pekee iliyonikutanisha na vijana wa mjini waliovuma late 90s to early 2000s.

ule usemi wa "kaunta ya juu" ulipewa umaarufu na vijana wala bata wa miaka hiyo kutokana na uwepo wa counter ya juu ya kuuza vinywaji ndani ya club hiyo.

ndiyo night club iliyonikutanisha na marehemu steve2k(castrol ponella), marehemu complex na vijana wengine wengi maarufu wa wakati huo.

ukiondoa majumba mengine ya starehe, club bilicanas ilikuwa ni moja ya meeting point yao.
 
Back
Top Bottom