Smart911
Platinum Member
- Jan 3, 2014
- 167,040
- 185,339
MULIZI; NILIPOMUAMSHA SHETANI WA MUME WANGU--- SEHEMU YA NANE!
Mume wangu hakuongea chochote, alikaa pale sebuleni na dada yake huku akilia kisha akaingia chumbani. Aliniambia kuwa kachoka sana anataka kulala.
“Kuna nini mbona uko hivyo, unarudi unalia namna hiyo?” Nilimuuliza kwani nilikua nimechanganyikiwa kwa uoga.
“Hakuna kitu mke wangu, ila jua tu kuwa nilikupenda sana, nilikupenda mpaka nikapitiliza lakinmi umeharibu maisha yangu.” Aliniambia kisha akapanda kitandani, hakuongeza neno jingine, hata nilipomsemesha tena hakuongea./
Nilirudi sebuleni ambapo nilimkuta dada yake kakaa, alionekana kuwa na mawazo mengi sana, nililazimika kumuuliza kuna tatizo gani kwani namuona Kaka hayuko sawa.
“Unajua kuna wanawake wana bahari sana, hivi kwanini na mimi nsiingepata mume kama Kaka yangu?” Alianza kuongea, nilibaki na mshangao kwani sikujua anaongelea nini, nilitamani kumuuliza ni kwanini anasema hivyo lakini kuna kitu kama kiliniambia, acha, acha usuulize, lakini aliendelea.
“Unajua pamoja na yote uliyomfanyia lakini bado hataki kukaucha, badoa nakupenda, yaani sijui umemloga au ni nini?” Wifi yangu aliongea, nilimuuliza ni kitu gani lakini aligoma kuongea, aliniambia kuwa kama ni kuniambia ataniambia mume wangu.
“Akuambie mwenyewe, mimi nimekuaj naye hapa kuhakikisha kuwa hafanyi kitu kibaya, lakini wewe mwanamke ni shetani, sijui ni namna gani mtu anaweza kulala kitanda kimoja na wewe na bado akapata usingizi!” Aliongea kwa hasira, mimi sikumuelewa lakinia ligoma kuongea nini kilikua kimetokea.
Bvado nilikua na wasiwasi, sijui nini kimetokea, sijui kama yule mwanamke amekufa au la? Nesi alikua hapatrikani hivyo ilikua ngumu kwangu kujua chochote. Nilika sebuleni kama sakika kumi hivi, mume wangu alitoka, alionekana kama mtua liyekua anatafuta usingizi na kuukosa, alikuja na kukaa karibu yangu. alikua kashikilia simu tatu mkononi, mbili zilikua zake nazifahamu na moja ilikua mpya siiijui, ilionekana kama ya kike kutokana nakava lake. Alinipa ile simu mpya na kuniambia niiangalie.
***
Mume wangu alikua na hela, angeweza kuupeleka mchepuko wake katika hospitali yoyote ile, lakini mwanamke alikataa, si kwakau alikua anapenda huduma za pale hapana ni kwakua, dada yake, mtoto wa Mama yake mdogo ambaye pia alikua ni shoga yake alikua akifanya kazi pale. Wakati anaanzisha mahusiano na mume wangu baadhi ya ndugu zake walijua,w alianza kumshauri kuachana na mume wa mtu lakini kama unavyojua wanawake wakishapenda basi huchanganyikiwa.
Kwa maana hiyo baada ya kupata ujauzito yule dada alitaka iwe siri, alienda kupimwa na ndugu yake, akapata majibu palepale na alikua anaenda kiliniki kimya kimya mpaka mimba ilivyokua kubwa ndiyo wakawa wanafanya waziwadi, hata mume wangu alikua anaongozana naye na hata kumsubiri, hwakufanya siri tena. Nesi ambaye nilimtafuta kwajaili ya kumtoa mimba mchepuko wa mume wangu alikua ndiyo huyo huyo dada yake.
Kwa maana hiyo nilichezewa, baada ya kujua huyo mwanamke ahakumuambia mume wangu mpaka siku ile usiku, alimpigia simu na kujifanya kuwa mimba imetoka, ndiyo maana alliongea na mimi kidogo na kuanza kutuma meseji ili kutengeneza ushahidi. Mume wangu alipofika aliambiwa, usiku wakati anaenda hospitalini akijua kuwa mwanamke wake mimba imetoka alimpigia simu dada yake ambaye waliongozana wakijua wamepoteza mtoto kumbe ulikua mchezo.
Mume wangu baada ya kuambiwa na kuona uthibitishoa likasirika sana ndiyo maana aliongozana na dada yake kuja kuniona. Alinipa ile simu ambayo ilikua ni ya nesi, tayari alishafungua meseji zanguambazo nilikua nimemtumia, nilishindwa hata kuzisoma, nilijua kuwa nishaharibu, ingawa nilijua kuwa ndoa imesiha lakini angalau nilijisikia vizuri kuona kuwa sijaua mtu, nilipomuona mume wangu anakuja analia nilijua moja kwa moja kuwa jela inanisubiri.
Kama kawaida yake mume wangu hakuongea sana, aliniambia tu kuwa imefika mwisho hivyo anaondoka. Mwanzo nilijau ni utani, lakini baadaye kama mchana hivi lilikuja gari, alichukua kila kilichochake na kuondoka. Nilijaribu kuomba msamaha lakini aliniambia kuwa imetosha, anahitaji kuwa na furaha. Mume wangu alihamia kwa yule mwanamke, baada ya kama wiki mbili hivi alianzisha mchakato wa talaka ambapo mimi niligoma kuachana naye.
Tulienda kanisani kusuluhishwa lakini mume wangua likataa katakata, hata hakuongea maneno mengi alisema tu kuwa hataki kuendelea kuishi na mimi, lakini bado hatukupewa barua ili mume wangu kwenda mahakamani. Tuliruidi nyumbani na siku iliyofuata mume wangu alienda ustawi wa jamii, sijui alifanya nini lakini alipata barua ya kwenda mahakamani na mchakato wa talaka ulianza.
Ingawa vitu vingi vilikua na majina yake lakini katika kuachana mume wangu aligawana na mimi kila kitu nusu kwa nusu na vitu vingine akaandika majina ya watoto. Mpaka napewa talaka sikuamini kama mume wangu ameniacha, nilikuja kuamini baada ya kufunga ndoa ya serikali miezi miwili tu baada ya kunipa talaka. hapo ndipo nilijua kuwa ndoa yangu imeisha na sina mume tena.
Nilibaki na watoto lakini nilikuja kunyang’anywa kwakua nilianza kunywa pombe, nilikunywa pombe kutokana na mawazo ya kumpoteza mume, upwek wa kutendwa na ugumu wa maisha. Haikuishia hapo, nilijikuta naingia kwenye dawa za kulevia, aada ya kuona hivyo mume wangua liingilia kati, alinipeleka Sober house ambapo nimefanikiwa kutoka nina mwaka sasa naishi kwa uangalizi wa mume wangu na ndugu zangu.
Watotyo wangu wanakuja kuniona mara moja kwa wiki, sina tena maisha na kila nikikumbuka namna nilivyochezea nafasi nazidi kujichukia. Nimeamua kuandika kisa changu ili angalau na wengine wajifunze, kama mtu ukipendwa basi chukulia upendo kama heshima na sikuona kuwa yule anayekupenda ni zuzu na hawezi kukuacha. Hakuna mtu ambaye hawezi kukaucha, jifunze kuacha baadhi ya mambo yapite, natamani kipindi changu kungekua na Kaka Iddi kwani sidhani kama ningefanya ujinga huu wa kuamsha shetani wa mume wangu ambaye alikua amekufa kabisa.
MWISHO.
Inasikitisha sana... sikio la kufa halisiki dawa... na ... Mwisho wa ubaya ni aibu...
Chapter Closed...
Cc: mahondaw


