Nilipomuamsha shetani wa mme wangu

Nilipomuamsha shetani wa mme wangu

NILIPOMUAMSHA SHETANI WA MUME WANGU--- SEHEMU YA TANO!

“Nilipojua kuwa unachepuka nilipaniki sana, kwa kifupi nilichanganyikiwa, niliangalia wanawake wengine namana wanavyoachwa nikaona kuwa namimi ipo siku utaniacha. Nikiangalia wanangu namna walivyozoea maisha mazuri nikasema hapana, lazima nifanye kitu, niliamua kufungua Biashara kimya kimya bila kukuambia. Kuna rafiki yangu mmoja alinipa dili la Pikipiki, kutoka china, akanipa mchongo nikaona kuwa ni kitu ambacho natakiwa kufanya.”

“Rafiki yako au Bwana wako?” Mume wangu aliniuliza, alikua kakasirika sana, nilijau kuwa atanipiga na kuniua lakini hakufanya hivyo.
“Hapana, si wmanaume wangu, mume wangu wewe unanijua, nina kisirani na wakati mwingine nafanya mambo ya kijinga ila tangu zamani nakupenda wewe, ninachanganyikiwa sana inapokuja kuhusu wewe, unakumbuka zamani kipindi hatujaoana, nilikua nagombana na wanawake wengi kwa kuongea na wewe, nakupedna sijawahi kukusaliti na siwezi kukusaliti.”

Nilimuambia mume wangu, nilikua nalia sana, nilidanganya lakini sikua na namna. Baada ya mume wangu kupokea simu na kuambiwa kuhusu mkop alinigeukia na kuniuliza. Mume wangua likua kapigiwa simu na rafiki yake mmoja, yeye ni dalali wa kampuni moja ambayo inauzaga nyumba zilizochukuliwa mkipo na benki. Nyumba yetu watu walishaanza kuipigia mahesabu, baada ya kushindwa kupeleka marejesho mawili walishaanza kuitafutia wateja.

Alipoambiw akutafuta watu wa kimya kimya kabla ya kupigw amnada ndiyo alishangaa na kuamua kumuambia mume wangu. Mume wangu alionekana kukataa kuwa hakuna mkopo, alikataa hata mimi alikua aniuliza kama kiutani utani lakini hakutilia maanani. Nakumbuka ilipita siku mbili bila mume wangu kulikumbushia hilo swala, usiku mmoja ndiyo niliamua kumuambia ukweli, nilijua kabia kuwa nyumba itauzawa kwanis ikua na hata shilingi mia, pesa kwa wakati huo tulikua tunadaiwa kama milioni mia hamsini hivi, silikua ni pesa nyingi sana kwangu na hata kwa mume wangu.

Niliamua kumuambia mume wangu ukweli kuwa nilichukua mkopo kwaajii ya kufanya Biashara kwakua nilijua kuwa ataniacha na kwend akusihi na mwanamke mwingine hivyo nilitaka kujipanga na si kumdhulumu. Kwakua nilijua kuwa akichunguz aatagundua mtu niliyekua nikifanya naye kazi nilijifanya kuwa ule mchepuko wangu ni rafiki yangu na aliamua kunitapeli yeye na rafikii yake. Nilisema kila kitu isopokuwa kua na mahusiano na yule Kaka.

Mume wangu alinisikiliza kwa makini, niliona kabisa kakasirika lakini kama kawaid ayake ni mtu wa kutulia, anazizuia hasira zake sana.
“Unajua umenikwaza sana?” Aliniuliza, nilimuangalia usoni, tulikua tumekaa kitandani nilishuka chini na kupiga magoti kutaka kumuomba msamaha, alinishika na kuninyanyua.
“Acha kukufuru mume wangu, goti halipigwi kwangu.” Alinikalisha kitandani na kuniangalia usoni kwa kama nusu saa hivi bila kuongea kitu chochote. Baada ya hapo alinyanyuka na kutoka, hakurudi tena mpaka asubuhi na mimi sikulala mpaka asubuhi, alirudi akiwa amechangamka sana, nilijua atanifanyia kitu kibaya lakini haikua hivyo.

“Kwanini unanitesa hivyo lakini? Hivi unafikiri kuna kitu kinaweza kunifanya mimi kukuacha na kutelekeza watoto wangu?” Aliniulzia, nilijikuta nabaki tu kimya, sikua na jibu.
“Kwanini unajitesa hivyo unajua una wivu sana, yaani naona kama huna maisha, unaishi kwa kuteseka kuwaza kuwa nitakuacha, kwanini nikuache, ni mambo mangapi navumilia. Umejaribu kunitenganisha na familia yangu, umejaribu kunigombanisha na kila mtu, umenidhalilisha mara kibao nakuvumilia, lakini bado huniamini, hivi kweli nifanye nini wewe mwanamke ili ujuwa kuwa nakupenda na siwezi kukuacha?”

Aliniuliza, kusema kweli sikua na jibu, mume wangu nilishamfanyia vituko vingi, mara kibao nilishataka kuondoka na kumuacha kwa makosa kidogo tu, nilikua na kelele nyingi kiasi kwamba nyumba haina amanai, ilifikia kipindi mume wangu alikua anataoka kazini badlaa ya kuingia ndania naaka kwenye gari hata masaa manne ili tu akiingia nimechoka nimelala.
“Hata sijui, nimekufanyia mengi mume wangu lakini sijui hata ni kwanini bado unanipenda?” Nilikua sina jibu, kusema kweli nilsihakata tamaa, nilijua kwua mume wangu hawezi kunisamehe nishajiandaa kwa chochote.

“Umesema kuwa wamekutapeli? Una uhakika?” Alibadilisha mada, alikua tofauti kabisa, alichangamka kidogo, nilitaka kumuomba tena msamaha lakini alinikataza.
“Ndiyo mume wangu, ni watu ambao niliwaamini lakini wamechukua kila kitu.” Nilijitetea, mume wangu aliniangalia kwa uchungu, niliona hasira zake ni kama zinataka kupanda, nilimsogelea na kutaka kupiga magoti tena kumuomba msamaha lakini alinishika na kuninyanyua.
“Sitaki msamaha wako, sijui kwanini sikuamini lakini sitaki tena msamaha wako, sijui ulipozipeleka hiso pes alakini nazitaka, utalipa hilo dani la watu na nyumba itarudi.” Alininyanyua kwa hasira na kunisukumiza pembeni, alianza kutafuta aliingia kabatini na kuchukua nguo zangu, alizikusanya na kunipa.

“Kila iku nakudekeza, ukinikosea wewe naomba msamaha mimi, naondoka mimi lakini sasa hivi nimechoka, naona umeamua kunifanya ndondocha, sitaki tena upuuzi wako. Ninachotaka ni pesa zangu, ulipe hilo deni na hata ya nyumba niione hapa.” Alinitupia nguo zangu, niliomba msamaha sana lakini mume wangu hata hakunisikiliza. Nililia na kuigalagala chini ila hata hakujali, alinichukua na kunitoa nnje, akanitupia nguo zangu na kuniambia niondoke kwani hataki tena kuniona.

Nikiwa pale nnj endiyo nilijua kuwa mume wangu alikua yupo siriasi, ainmifungia na kurudi ndani. Kwa aibu nilichukuanvitu vyangu, nikachukua Bajaji mpaka kwa rafiki yangu. Nilimuambia kila kitu kuhusiana na mkopo na namna ambayo mume wangu alikua kanifukuza. Alinisikiliza sana kisha akaniambia.
“Huwezi kulala kwangu, ninachoweza mimi nikukupa pesa ukatafute sehemu ya kulala au urudi kwenu. Mume wangu amebadiolika sas ahivi anajali na kaniambia kuwa wewe ndiyi unaniharibu, tena ndiyo uondoke kabla ya kuniharibia ndoa yangu, ushavunja yako sitaki uvunje na yangu.”

Mwanzo nilijua kama ni utani, lakini shoga yangu alinifukuza kwake, kusema kweli shida yangu kwa wakati huo haikua pesa bali mtu wa kunifariji na kuongea naye. bado nilikua na pesa kidogo, niliend kupangisha chumba gest nikisubiri mume wangu kunipigia simu kutaka kurudiana na mimi, kwa nilivyokua namjua mume wangu nilijua kabisa hawezi kuishi bila mimi, nilijua kuwa hawezi kuniacha, ingawa nilikua na huzuni lakini nilijua ni jambo la muda tu atarudi.

Ulikua ni usku mrefu sana kwangu lakini ilikua ni lazima kulala, kesho yake ilikua ni siku ya kazi, ingawa usingizi ulikua ni wa shida lakini ilikua ni lazima niende kazini kwani kulikua na ukaguzi. Nilienda huku nikijifanya kuwa akuna kitu kilichotokea, nilisalimiana na kila mtu vizuri na wote ilikua kawaida kwani ni rafiki yangu mmoja tu ambaye alikua anajua kuhusu maisha yangu. Mambo yalikua mazuri mpaka ilipofika saa nne, nakumbuka nilikua nakunywa chai kantini, nilishangaa kila mtu ananifuata na kunipa pole.
“Pole ya nini?” niliuliza, walianza kunaimbia kuwa wanaume si watu wa kuamini, mara hivi, mara vile, yaani watu walikua wanaongea ongea mpaka nikaanza kuona aibu.

Niolimfuata rafiki yangu na kumuuliza kama amemuambia mtu kuhusu ishu yangu, mwanzo alikataa, baadaye akanimbia kuwa kuna mtu mmoja tu alimuambia, nilimlaumu sana kwa kuniaibisha na kunitangzaa.
“Mama, usinileteee, jilaumu kwa ujinga wako, nyie ndiyo washenzi mnachukua waume za watu, mnawachukulia mikopo! Mume wangu naye kuna mwba kwama wewe alifanya hivyo hivyo! Acha kuniletea umalaya wako hapa na kuniona sinich kwa kukutangaza wewe ni shetani tena unikome, sitaki hata unisogelee!

Usivyo na aibu unakuja kwangu kutaka eti nikupokee, unataka umchukua na mume wangu mbwa wewe, tena unikome sitaki na mazoea, kwa taarifa yako ukinitibua naenda kumwagia mume wako kila kitu ulichofanya na huyo Malaya wako, niondokee mshenzi mkubwa mbwa kabisa wewe! Nimeteseka sana kwenye ndoa yangu kwasababu ya washenzi akam wewe mnaojiona kuwa mnajua kila kitu!”

Alinitukana kwa sauti mpaka nikaishiwa posi, ni kama alikua na mambo yake moyoni alikua anashidnwa kuniambia. Niliumia sana kwani yeye ndiyo alikua ni rafiki yangu mkubwa, ndiyo mtu alikua akinishauri na mimi kumuambia kila kitu. Kinyonge kabisa nilirudi ofisini kwangu, kuna kazi nilikua na malizia kabla ya kuonana na wakaguzi, nisingeweza kuondoka na wala nisingeweza kufanya chochote, nilikaa mpaka jioni mume wangu hakunipigia simu wala kutuma meseji.

Nilirudi hotelini ambapo nilikaa kwa wiki nzima bila mume wangu kunitafuta, hata ndugu zangu alikua hajawaambia chochote kwani walikua wakinipigia simu tunaongea kawaida. Nilikua kwenye mawazo makubwa sana, nilikodnaa ndani ya wiki moja na kuwa kama mgonjwa wa muda mrefu. Kazini sikua na rafiki tena, kila mtu alinikimbia, hakuna mtu aliyeniamini, Benki napo walikua wakipiga simu mara kw amara wakitaka pesa.

Baada ya kama wiki moja hivi mume wangu alinipigia simu, aliniambia kuwa anataka kuonana na mimi, nilishukuru Mungu nikajua kuwa kashidnwa kuishi bila mimi hivyo anataka turudiane. Lakini nilikata tamaa tulipoonana mabapo alikua ananiulizia kuwa nimefikia wapi kuhusiana na kulipa deni. Sikua na jibu kwani sikua na kitu chochote, aliniambia nimpeleke wkenye duka ambalo nilifungua, nilimpeleka na kulikua hakuna kitu, pikipiki zilikua zimebaki kama 12 ambazo zilikua na thamani kama ya milioni 20 na kitu.

Aliangalia kwa masikitiko sana, niliumia kumuona katika hali ile.
“Nataka kuonana na hao jamaa, nataka kuonana na hao watu waliokutapeli.” Aliniambia, nilimuambia kuwa hawapokei simu zangu na wamenitishia kuwa hawawezi kunipa.
“Si unajua nyumbani kwao, au ulimpa mtu pes ayote hiyo hata hujui kwake?” Aliniuliza, sikua na jibu, nilibaki kimya, alinisisitiza kuwa anataka kuonana nao na kusisitiza zaidi kuwa anataka kwend anyumbani kwao. Kusema kweli nilitamani kumpeleka mume wangu lakini nilihofia, kwanza mke wa yule Kaka alikua akinifahamu, nahisi alishaona picha zangu ingawa nilikua sijawahi kuonana naye moja kwa moja.

Pili nilihofia kuwa labda wanaweza kupandishiana na mume wangu akasema kuwa nimewahi kutembea naye. Mume wangu alikua akiniamini sana kuhusiana na ishu ya mapenzi, alijua kuwa nampenda na mambo yote niliyokua nayafanya ilikua ni ujinga wa wivu, kwa namna alivyokua ananiamini alijua kuwa siwezi kumsaliti. Nilijua kuwa anaweza kunisamehe kitu kingine chochite kile lakini si usaliti. Lakini sikua na namna, ilikua ni lazima kumpeleka mume wangu kwa huyo Kaka.

Nilimkubalia, nikachukua simu yangu harahaharaka na kumtumia yule Kaka, nikamuambia kuwa mume wangu anakuja kwake, ameshajua kila kitu hivyo asijekusema kuwa alishawahi kutembea na mimi. Hakujibu meseji ingawa niliona kuwa imefika, tuliongozana na mume wangu mpaka kwa yule Kaka, kwa bahati nzuri mke wake alikua hayupo, alikua kasafiri kikazi. Mume wangu kwa kawaida ni mstaarabu, aliingia kistaarabu na yule Kaka alinisalimia kama ananijua.

Mume wangu alijitambulisha na kumuambia sababu ya sisi kwenda pale. Alipoambiwa alinmiruka kabisa, alisema ni kweli ananifahamu, ni kweli tulishawahi kuongea naye kuhusu kufanya biahsara lakini baada ya kluona Biashara yenyewe ni kubwa basi aliamua kuacha, hajawahi kuchukua pesa zangu wala kitu chochote kutoka kwangu.
“Mimi nimeoa Broo, nina maisha yangu, ni kweli mke wako namjua, tulikutana Baa, na aliniambia kuhusu Biashara, lakini mimi sikua na mtaji, mimi ni mtoto wa mjini tu, sina kazi ya maana.

Niipoteza kazi miaka mitano nyuma na tangu hapo nasimamia Biashara ndogo ndogo tu za mke wangu, mke wangu yeye anafanya kazi, anaanigiza mzigo china, mimi kwakua sina kazi naenda huko nachukua mzigo na kila kitu ni cha mke wangu. Sijawahi kufanya Biashara na mke wako kabisa, ningeanzia wapi, halafu hizo pesa unazotaja ni nyingi sana, hivi kwa maisha ninayoishi nipate milioni mia tu si ningekua mbali, wewe mwenyewe unaona, sasa hivi nipo nyumbani mke kasafiri sasa kweli niwe na milioni 100 nibaki hivi hivi.

Alichofanya mke wako ni hivi, mimi alinifuata na kutaka kufanya naye Biashara, alinaimbia kuna mchongo kapata china na kwakua mimi naenda huko bvasi nimpeleke na tufanye Biashara. Kuna watu ambao wanafanya biashara huko, akanitajia nikamuambia kabisa kuwa hiyo ni pesa nyingi kuwa makini na hao watu, usiwe unatoa toa pesa hivyo. Basi nikmsahauri kuhsu china lakini niliamua kukata mawasiliano na mke wako kwakua baada ya kuanza tu kuongea haya mambo basi mke wangu alihisi kuwa labda nachepuka.

Mkeo alikua anapiga simu mara kwa mara tena usiku, anatuma mseji, yalikua ni ammbo ya Biashara lakini kamka unavyojua ndoa zetu, mke wangu alikasirika sana mpaka ikafikia hatua nikakatisha mawasiliano na mke wako. Kama huamini basi angalia simu yangu, hizi meseji angalia nilimtumia lini, angalia nilivyokua namuambia.” Huyu Kaka alikua kajipanga, alikua anaongea kistaarabu,a likua anaongea kama malaika, alionyesha kana kwamba mimi ndiyo nilikua namsumbua.

Kama mnakumbuka kipindi kile baad aya kufumaniwa alitinumia meseji nyingi kunitukana, lakini mimi nilikua namtumia meseji nyingi kutaka kuoanna naye, kumuomba msamaha na mambo kama hayo. Nhuyu Kaka alikua ni tapeli kwania lifuta meseji zote zkuonyesha kuwa tulikua wapenzi, akabakiza meseji za mimi kuomba msamaha, mimi kutaka kuonana naye na kuacha meseji zake akinitukana na kuniambia kuwa nimuache kwani nitamharibia ndoa yake.

“Sijawahi kuwa na mahusiano na mke wako, lakini kuna vitu vilinichanganya kwani wakati anataka kuchukua mkopo aliniambia kuwa hajwahi kuolewa, aliniambia kuwa alikua anaishi na mwanaume wakaachana ndio maana hata nikakubali kuwa mdhamini wake, lakini si hivyo tu, alinionyesha hati ya nyumba ambayo ina majina yake, mimi nilichofanya ni kusaidini na kumsiadia kumuunganisha na watu wa Benki ili kuupata mkopo wake kwa urahisi. Lakini baadaye nilikuja kujua kuwa ameolewa, na kibaya ziadi akawa ananitumia msejei usiku na kunipgia simu.

Wewe upo kwenye ndoa, naamini mtu akimpigia simu mke wako usiku utajisikia vibaya na kudhani kuwa unasalitiwa, basi ndiyo kilitokea kwa mke wangu, baada tu ya kuona ananisumbua nikajua kuwa atanivunjia ndoa yangu nikampiga marufuku kabisa, sikutaka tena mawasiliano naye. Nahisi alitafuta watu wake wengine ambao walimsanganya ila mimi nilimuelewesha kila kitu kuhusu china na jinsi Biasharainavyokua na kumuambia awe makini.”

Aliongea hukua kimuonyesha mume wangu baadhi ya mesji ambazo alikua ananitumia kunielezea kuhusu Biashara ya Pikipiki huo china. Mimi sikua na chakuonyesha, nilikumbuka kuwa mara nyingi alikua ni mtu wa kuniambia nifute meseji zangu ili mume wangu aisje kuziona.

“Samahani kwa kukusumbua, nashukuru nimekuelewa, nilikua nimewaza kufanya mengine ila sasa hivi nimeshajua shetani ni nani?” Mume wangu alimuambia yule Kaka, alinyanyuka kwa hasira, bila hata kuniambia tunyanyuke wote aliondoka mpaka kwenye gari, nilimfuata na kutaka kupanda kwenye gari pamoja naye lakini alinikataza.
“Ukiingiza kichwa chako humu naenda kukugongesha kwenye nguzo kama ni kufa tufe wote!” Mume wangu aliniambia ksiha akaingia kwenye gari na kuondoka
Haikutakiwa kuishia hapa
 
Duh. Stori hii nzuri kweli. Yaani kuna vitu nimejifunza hapa lazma nivifanyie kazi. Na stori iendelee
 
Huyo mwanamke anayepitia hayo magumu yote atakua ni wale warembo/wazuri kupindukia ndiyo wanapitiaga misukosuko sana kwa tabia zao...

Ngoja tuone...



Cc: mahondaw
 
MULIZI; NILIPOMUAMSHA SHETANI WA MUME WANGU--- SEHEMU YA NANE!

Mume wangu hakuongea chochote, alikaa pale sebuleni na dada yake huku akilia kisha akaingia chumbani. Aliniambia kuwa kachoka sana anataka kulala.
“Kuna nini mbona uko hivyo, unarudi unalia namna hiyo?” Nilimuuliza kwani nilikua nimechanganyikiwa kwa uoga.
“Hakuna kitu mke wangu, ila jua tu kuwa nilikupenda sana, nilikupenda mpaka nikapitiliza lakinmi umeharibu maisha yangu.” Aliniambia kisha akapanda kitandani, hakuongeza neno jingine, hata nilipomsemesha tena hakuongea./

Nilirudi sebuleni ambapo nilimkuta dada yake kakaa, alionekana kuwa na mawazo mengi sana, nililazimika kumuuliza kuna tatizo gani kwani namuona Kaka hayuko sawa.
“Unajua kuna wanawake wana bahari sana, hivi kwanini na mimi nsiingepata mume kama Kaka yangu?” Alianza kuongea, nilibaki na mshangao kwani sikujua anaongelea nini, nilitamani kumuuliza ni kwanini anasema hivyo lakini kuna kitu kama kiliniambia, acha, acha usuulize, lakini aliendelea.

“Unajua pamoja na yote uliyomfanyia lakini bado hataki kukaucha, badoa nakupenda, yaani sijui umemloga au ni nini?” Wifi yangu aliongea, nilimuuliza ni kitu gani lakini aligoma kuongea, aliniambia kuwa kama ni kuniambia ataniambia mume wangu.
“Akuambie mwenyewe, mimi nimekuaj naye hapa kuhakikisha kuwa hafanyi kitu kibaya, lakini wewe mwanamke ni shetani, sijui ni namna gani mtu anaweza kulala kitanda kimoja na wewe na bado akapata usingizi!” Aliongea kwa hasira, mimi sikumuelewa lakinia ligoma kuongea nini kilikua kimetokea.

Bvado nilikua na wasiwasi, sijui nini kimetokea, sijui kama yule mwanamke amekufa au la? Nesi alikua hapatrikani hivyo ilikua ngumu kwangu kujua chochote. Nilika sebuleni kama sakika kumi hivi, mume wangu alitoka, alionekana kama mtua liyekua anatafuta usingizi na kuukosa, alikuja na kukaa karibu yangu. alikua kashikilia simu tatu mkononi, mbili zilikua zake nazifahamu na moja ilikua mpya siiijui, ilionekana kama ya kike kutokana nakava lake. Alinipa ile simu mpya na kuniambia niiangalie.

***
Mume wangu alikua na hela, angeweza kuupeleka mchepuko wake katika hospitali yoyote ile, lakini mwanamke alikataa, si kwakau alikua anapenda huduma za pale hapana ni kwakua, dada yake, mtoto wa Mama yake mdogo ambaye pia alikua ni shoga yake alikua akifanya kazi pale. Wakati anaanzisha mahusiano na mume wangu baadhi ya ndugu zake walijua,w alianza kumshauri kuachana na mume wa mtu lakini kama unavyojua wanawake wakishapenda basi huchanganyikiwa.

Kwa maana hiyo baada ya kupata ujauzito yule dada alitaka iwe siri, alienda kupimwa na ndugu yake, akapata majibu palepale na alikua anaenda kiliniki kimya kimya mpaka mimba ilivyokua kubwa ndiyo wakawa wanafanya waziwadi, hata mume wangu alikua anaongozana naye na hata kumsubiri, hwakufanya siri tena. Nesi ambaye nilimtafuta kwajaili ya kumtoa mimba mchepuko wa mume wangu alikua ndiyo huyo huyo dada yake.

Kwa maana hiyo nilichezewa, baada ya kujua huyo mwanamke ahakumuambia mume wangu mpaka siku ile usiku, alimpigia simu na kujifanya kuwa mimba imetoka, ndiyo maana alliongea na mimi kidogo na kuanza kutuma meseji ili kutengeneza ushahidi. Mume wangu alipofika aliambiwa, usiku wakati anaenda hospitalini akijua kuwa mwanamke wake mimba imetoka alimpigia simu dada yake ambaye waliongozana wakijua wamepoteza mtoto kumbe ulikua mchezo.

Mume wangu baada ya kuambiwa na kuona uthibitishoa likasirika sana ndiyo maana aliongozana na dada yake kuja kuniona. Alinipa ile simu ambayo ilikua ni ya nesi, tayari alishafungua meseji zanguambazo nilikua nimemtumia, nilishindwa hata kuzisoma, nilijua kuwa nishaharibu, ingawa nilijua kuwa ndoa imesiha lakini angalau nilijisikia vizuri kuona kuwa sijaua mtu, nilipomuona mume wangu anakuja analia nilijua moja kwa moja kuwa jela inanisubiri.

Kama kawaida yake mume wangu hakuongea sana, aliniambia tu kuwa imefika mwisho hivyo anaondoka. Mwanzo nilijau ni utani, lakini baadaye kama mchana hivi lilikuja gari, alichukua kila kilichochake na kuondoka. Nilijaribu kuomba msamaha lakini aliniambia kuwa imetosha, anahitaji kuwa na furaha. Mume wangu alihamia kwa yule mwanamke, baada ya kama wiki mbili hivi alianzisha mchakato wa talaka ambapo mimi niligoma kuachana naye.

Tulienda kanisani kusuluhishwa lakini mume wangua likataa katakata, hata hakuongea maneno mengi alisema tu kuwa hataki kuendelea kuishi na mimi, lakini bado hatukupewa barua ili mume wangu kwenda mahakamani. Tuliruidi nyumbani na siku iliyofuata mume wangu alienda ustawi wa jamii, sijui alifanya nini lakini alipata barua ya kwenda mahakamani na mchakato wa talaka ulianza.

Ingawa vitu vingi vilikua na majina yake lakini katika kuachana mume wangu aligawana na mimi kila kitu nusu kwa nusu na vitu vingine akaandika majina ya watoto. Mpaka napewa talaka sikuamini kama mume wangu ameniacha, nilikuja kuamini baada ya kufunga ndoa ya serikali miezi miwili tu baada ya kunipa talaka. hapo ndipo nilijua kuwa ndoa yangu imeisha na sina mume tena.

Nilibaki na watoto lakini nilikuja kunyang’anywa kwakua nilianza kunywa pombe, nilikunywa pombe kutokana na mawazo ya kumpoteza mume, upwek wa kutendwa na ugumu wa maisha. Haikuishia hapo, nilijikuta naingia kwenye dawa za kulevia, aada ya kuona hivyo mume wangua liingilia kati, alinipeleka Sober house ambapo nimefanikiwa kutoka nina mwaka sasa naishi kwa uangalizi wa mume wangu na ndugu zangu.

Watotyo wangu wanakuja kuniona mara moja kwa wiki, sina tena maisha na kila nikikumbuka namna nilivyochezea nafasi nazidi kujichukia. Nimeamua kuandika kisa changu ili angalau na wengine wajifunze, kama mtu ukipendwa basi chukulia upendo kama heshima na sikuona kuwa yule anayekupenda ni zuzu na hawezi kukuacha. Hakuna mtu ambaye hawezi kukaucha, jifunze kuacha baadhi ya mambo yapite, natamani kipindi changu kungekua na Kaka Iddi kwani sidhani kama ningefanya ujinga huu wa kuamsha shetani wa mume wangu ambaye alikua amekufa kabisa.

MWISHO.
 
Kuna wanaume wana uvumilivu aisee


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom