Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,172
- 34,282
; NILIPOMUAMSHA SHETANI WA MUME WANGU--- SEHEMU YA KWANZA.
“Kwahiyo ndiyo unanirudia saa nne? Unajiona mw3anaume sana na hao rafiki zako ambao kila siku wanakudanganya? Wenzako hawajaoa lakini kila siku ni kuhangaika nao, unazunguka nao kama vile hujaoa, saa nne mimi nikufungulie mpango?” Nilimuambia mume wangu kwa hasira, kusema kweli mume wangu hakua ni mtu wa kuchelewa sana kurudi nyumbani lakini karibuni kama wiki moja hivi alibadilika.
“Naomba uniache, nimechoka sana, nilishakuambia kwanini nachelewa lakini hunielewi, mimi si mtoto mdogo wa kugombezwa kila siku, nimechoka kupiga kelele!” Mume wangu aliongea kwa ustaarabu, alinipita na kuingia chumbani, moja kwa moja alijilaza bila kula wala kuingia bafuni kuoga. Nilimfuata na kuanza kumnusa kuona kama alikua kaoga huko na kujipaka mafuta mengine lakini sikusikia chochote.
Pamoja na kutokusikia kitu lakini bado sikuamini, niliwaza alikua wapi? kama ni kazi mbona hana ubize huo, ananirudia saa ne halafu hataki kula ikimaanisha kuwa ameshibana kuoga haogi ikimaanisha kuwa ameoga huko alipokua. Niliongea sana lakini mume wangu hakunyanyuka wala kunyanyua mdomo kunijibu, kwangu ilikua ni dharau kubwa, nilikasirika na kwenda kulala chumba cha watoto ambao wlaikua shule bweni.
Asubuhi kama kawaida niliwahi kuamka, sikumuandalia mume wangu kitu chochote, nilijiandaa ili kwenda kazini, nilipomaliza nilitoka kukaa kwenye gari kumsubiri anipelkekazini kwanza, mume wangu alijiandaa na alitoka, alinisalimialakini sikumuitikia, nilikua nimenuna, naye hakusema chochote, aliingia kwenye gari akaendesha mpaka kunishusha kazini kwangu. Aliniaga lakini sikujibu, aliondoka mpaka kazini kwake.
Mchana mzima nilikua na kisirani, nilikua nimekasirika nikiamini kuwa mume wangu ananidharau na mabadiliko yale ni ya mwanamke mwingine. Nilimsimulia shoga yangu ambaye alizidi kunichanganya.
“Hata mume wangu alianza hivyo hivyo, hawa mbwa hawana shukurani, wanaanza kuchepewa kurudi baada ya muda unasikia mtu ana mwanamke mwingine, kaaza sijui nini, si unakumbuka mume wangu, mwanzo alianza kusema kuwa ana kazi nyingi, anachelewa kurudi, nashtuka anasafiri kikazi mara ana mtoto, hapana, kuwa makini, chunguza, usiruhusu akukalie kichwani!”
Rafiki yangu aliongea kwa hasira sana, aliumizwa sana na kitendo cha mume wake kuzaa nnje ya ndoa wakati alikua anampenda na alikua ni kama anamhudumia kwa kila kitu kwani mume wake tofauti na wangu si mtu wa kuhusumia familia.
“Sasa nifanyeje?” nilimuuliza.
“Kuwa mkali, wanaume ukiwachekea tu wanakufanya mjinga, kuwa mkali, usimchekee chekee, akichelewa kurudi gombana una kazi yako asikufanye mjinga, mimi nilishakosea kwa yule mbwa, nilimdekeza sana!”
Tuliongea mengi na shiga yangu, hata kazi hazikuenda, lakini kwenye saa sita na nusu hivi mume wangu alinipigia simu, nilitaka nisipokee lakini niliona ngoja nimsikiliza.
“Aiseee! Hatuwezi kuishi hivi, tuna watoto, nashindwa kufanya kazi kwa mambo ya kijinga, aisee tunatakiwa kuongea, kama hauko bize nakupitia tukele chakula cha mchana.” Mume wangu aliniambia kwa sauti ya kistaarabu, kwa namna alivyokua anaongea alikua anatia huruma, alionekana kama anataka kulia kabisa.
“Mimi nina kazi nyingi, nitafute jioni, kama utawahi kurudi basi tutaongea.”Nilimjibu wka mkatao kisha nikaakata simu, alijaribu kupiga tena lakini sikupokea, sikua na kitu cha kumjibu kwa wakati huo, nilishaanza kummiss na kumunea huruma, nilijua kama nitaongea naye basi nitamsamehe kitu ambacho sikua tayari kukifanya. Baada ya kukata simu nilimfuata shoga yangu, nikamuambia mume wangu kanipigia simu anataka kunitoa lunch ili tukaongee.
“Huyo ni Malaya kabisa, yaani najua tabia zao, wakishakosea ndiyo wanajifanya vizawadi na kuomba misamaha!” Alinaimbia kwa hasira, alinisihi sana kukataa na kuniambia kuwa kama nikikubali kizawadi cha kijinga kama chakula basi ndiyo utakua mwanzo wa ndoa ya mateso.
“Wanajua akili zetu, wanatuona sisi wajinga, mtu anakurudia saa nne halafu anaenda kukununulia chips kuku anataka usahau? Ujinga mtupu, nakuambia akija hata nnje usitoke, muambie una kazi!”
Aliniambia, nilimkubalia nakurudi ofisini kwangu, ni kweli nilikua sijawahi kumfumania mume wangu, yeye ni mkimya na mara nyingi ni wale watu hata kama ni wewe umekosea basi watajishusha ili tu kuwe na amani.
“Ananichukulia mjinga huyu, nimesema kuwa kama anataka tuongee basi akubali kuwa anachepuka na ana mwanamke mwingine!” Niliongea peke yangu, wakati huo huo meseji ya mume wangu iliingia.
“Jiandae nipo njiani, hatuwezi kuishi hivi.” Niliisoma na kusonya, kisha nikamjibu.
“Nina kikao.” Nilijibu na baada ya hapo nilizima simu, sikutaka anitafute tena kwani ninavyomjua mume wangu nikiongea kidogo angenishawishi na ningemsamehe.
Baada ya kama dakika kumi hivi mume wangu alikua ofisini kwangu, alisimama nnje ya ofisi na kuniomba nitoke. Nilitoka kwa kuchungulia nikamuambia kuwa nipo bize siwezi kwenda popote. Alisoge mlangoni huku akitaka kuingia ofisini kwangui, lakini sikumruhusu, nilikua kama namsukumiza kwa nnje.
“Acha kuwapa watu faida, nisikilize kwanza.” Aliniambia kistaarabu kama anaomba kuingia.
“Niondokee! Si uende kwa hao Malaya wako ukawanunulie chakula kama una pesa zinakuwasha!” Nilimjibu kwa hasira, kusema kweli sikupanga kufanya hivyo lakini kwa namna alivyokua anasisitiza kutaka kuingia ofisini kwangu niliona kama vile analazimishia, hasira zilinipaanda na bila kujijua nilijikuta nakasirika na kumsukuma mume wangu.
Mume wangu alishtuka kuona kuwa nilikua nimekasirika kiasi kile alitaka kuondoka lakini alishindwa, alipiga hatua kama mbi.i hivi kisha akageuka.
“Ni hili hili la mimi kuchelewa kurudi nyumbani au kuna jambo jingine mke wangu?” Aliniuliza lakini sikumjibu, nilifunga mlango na kuingia zangu ndani.
Nilirudi kwenye kitu na kukaa, nilianza kulia, “Nimefanya nini?” niliwaza baad aya kukaa na kutulia, ofisi yangu ipo ghorofani hivyo unaona kila kitu kinachoendelea chini. Nilisogea mpaka dirishani nikamuangalia mume wangu jinsi alivyokua anaondoka kwa unyonge mpaka nilimuonea huruma. Alitembea taratibu mpaka kwneye gari yake, alifungua mlango na kuingia, hakuondoka, alikaa kwenye gari kwa zaidi ya nusu saa bila kuondoka.
Nilijisikia vibaya na kutaka kutoka kumfuata, lakini malngoni nilikutana na shoga yangu.
“Yule mshenzi nimesikia kaja hapa, lakini umefanya vizuri ulivyomfukuza, sasa hivi atashika adabu, hawezi kukusumbua tena, unafikir wanaume ni watu, sasa sababu ya kuja mpaka ofisini ninini kama si kutaka tu kujishaua watuwamuone anajali.” Aliongea maneno mengi kiasi kwamba nilijikuta naacha kwenda, niliona ni sawa nilivyofanya, nilirudi na kukaa kwneye kiti huku nikichungulia getini, niliona gari ya mume wangu ikitoka hapo ndipo nilijua kuwa kaondoka.
***
Jioni mume wangu aliwahi kurudi, hakuchelewa kama jana yake, saa mbili tu alikua nyumbani. Alinisalimia vizuri na mimi nilimuitikia, kwahi kwake kurudi niliona kabisa kuwa kweli kajifunza, ingaw abado nilikua na wasiwasi kuwa ana mwanamke mwingine lakini sikutaka kuingiza kisirani. Aliingia ndani na kukaa, baad aya kuoga alinifuata sebuleni, tayari nilishaanda achakula cha usiku, wakati tunakula alianza kukumbushia mambo yaliyopita.
“Hivi mke wangu kuna nini? Naona kama umebadilika sana, unakua mtu wa hasira, si mtu wa kunisikiliza, hembu niambie kuna nini?” Aliniuliza kwa ustaarabu lakini ni kama aliamshha mashetani yangu.
“Mimi si wa hivyo, mimi si mjinga kama hao wanawake wengine, yaani makosa ufanye wewe halafu ujaribu kunigeuzia kibao. Nani anarudi usiku! Nani ambaye hajibu sms! Nani ambaye kila ukimpigia simu anajifanya kuwa yuko bize na kazi, yaani kila kitu ni wewe unafanya lakini sas ahivi unataka kunilaumu, kwa taarifa yako mbinu zako zote nazijua, wewe ni Malaya lakini unataka kunigeuzia kibao ili mimi ndiyo nionekane kama nina kisirani, hapana!”
Nilimuambia, nilitukana sana lakini mume wangu hakujibu chochote, kitendo cha mume wangu kukaa kimya kiliniumiza sana, nilijua kuwa ni dharau, nilianza kulalamika kuwa ana dharau, anafanya makosa kisha ananigeuzia kibao na kujifanya mwema. Alinisihi sana nitulie lakini niliishia kumtukana, nilivyoona hajibu kitu nilichukua sahani ya chakula na kumrushia, nilitaka kumpiga kichwani ila kwa bahati aliikwepa, nilimfuata na kuanza kumpiga mangumi huku nikimtukana lakini hakujibu zaidi ya kunishika kwa nguvu ili nisimguse.
Nilijitoa mikononi mwake na kuondoka moja kwa moja mpaka chumba cha watoto, asubuhi niliwahi kuamka sikumsalimia wala sikumsubiri. Nilienda kazini ambapo sikukaa sana, sikuongea kitu chochote kwa mtu, nilikaa kidogo nikashindwa kufanya kazi, nilitoka mpaka kwa Mama, nilimuambia kila kitu kuwa Mume wangu kabadilika, amekua mtu wa kurudi usiku na nikimuuliza ananuna, hanisemeshi, niliongea mambo mengi sana nikamuambia kuwa nahitaji kupumzika kubaki nyumbani lakini Mama alinigomea.
Alikataa hata kuita wazee aliniambia kuwa hayo ni mambo madogo niende ni kamalizane na mume wangu niache kufaidisha ulimwengu. Hata Baba hakumuambia alisema ni mambo ya kitoto, nilimuambia hata ampigie simu mume wanyu na kumanya lakinia likataa. Kwa kumsikiliza niliona kama Mama yupo upende wa mume wangu, nilikasirika zazidi kwani yeye ndiyo nilimuona kama mkombozi wangu. Sikua na namna nilirudi nyumbani kwa kununa hivyo hivyo, sikuomba msamaha wala mume wangu hakunisemesha, yalienda hivyo hivyo kimya kimya mpaka yakaisha.
Maisha yaliendelea lakini sikumuamini tena mume wangu, nilianza kumfualtilia, kila siku niishika simu yake na kuangalia wanawake ambao anachata nao, mara ntyingi nilikua nikichukua namba za wanawake katika simu yake na kuwatukana sana kuwaambia waachane na mume wangu. Hali hiyo ilimkera mume wangu, akawa anakasirika na mwisho aliweka simu yape password kitu ambacho kilinikasirisha zaidi, nilaimini kuwa ni kweli anachepuka ndiyo maana anaficha hataki nione kilichomo ndani.
Ndoa yetu ilianza kuwa ya migogoro, kila siku kelele, mume wangu alizidisha kuchelewa, akisingizia kazi lakini mimi niliamini kuwa ana mwanamke mwingine. Siku moja kulikua na sherehe kazini kwao, aliniambia wiki moja kabla, nilikataa kwenda lakini nilipoongea na shoga yangu aliniambia niende ili kama anachepuka basi michepuko yake ambayo labda aliidanganya kuwa hajaoa au tumeachana basi inione tukiwa na furaha.
Siku ya tukio wakati ashamaliza kujiandaa basi nilimuambia mimi naenda, alishangaa lakini alilazimika kunisubiri kwani kwa makusudi kabisa ili kumchelewesha na kumuudhi nilijiandaa taratibu. Sherehe ilikua inaanza saa mbili usiku lakini sisi tulifika saa nne. Watu walishajaa na hakukua na siri za kukaa pamoja, mume wangu alinitafutia mimi sehemu nzuri ya kukaa kisha yeye akaenda kukaa nyuma kabisa kwani shugui ilikua inaendelea hivyo asingeweza kunyanyua watu.
Mimi nilikaa mbele hivyo sikuweza kumuona mume wangu vizuri, yeye alikaa kwenye kiti tu hakukaa kwenye meza, pamoja na kuwa alikua na cheo kikubwa lakini mume wangu si mtu wa kujikweza hivyop aliniacha mimi nikae kwenye siti yake na hata mtu alipojitolea kumpisha aligoma kwani aliyateka kunyanyuka naye alikua na mke wake. Sherehe iliendelea nikiwa sina raha kabisa, nilikua nina wasiwasi nikitamani kuwa karibu na mume wangu ili watu wasiniibie, wka sababu hiyo nilijikuta nanyanyuka mara kwa mara kutoka kana naenda kujisaidia kumbe nilikua namchungulia mume wangu kwani sehemu aliyokua amekaa ilikua karibu na choo.
Nilitoka zaidi ya mara tatu, ya nne nikiwa narudi nilimuona dada mmoja, alikua kakaa jirani na mume wangu, walikua wameinamiana na mume wangu alikua akimuonyesha kitu kwenye simu yake. Mara zote wakati napita yule dada hakua pale, siti aliyokua kakalia ilikaliwa na Kaka mwingine, inamaana alikua katoka alipokua kumfuata mume wangu. Nilijikuta napandwa na hasira niliwafuata na kumnyanyua mume wangu.
Yule dada alinyanyua uso kuniangalia, nilimuona na kumkumbuka, miezi kama miwili nyuma siku ya kuzaliwa kwa mume wangu alipost picha ya mume wangu na kumtakia heri mume wangu, nilikasirikaga na kumuuliza mume wangu lakini aliniambia kuwa ni rafiki tu. Nilipomuona nilijikuat anapandwa na hasira, nilimshika mume wangu na kumnyanyua, bila kujali nilikua wpai nilianza kumuambia tuondoke, mume wangu alijua nishakasirika hivyo alinyanyuka harakaharaka ili kuondoa aibu.
Alinishika mkono na kuniambia tutoke nnje, lakini kabla hatujaondoka yule dada aliyekua amekaa alianza kucheka kwa dharau, nilijisikia vibaya, nilipepesa macho pembeni, kwenye meza ya jirani kulikua na chupa ya bia. Niliichukua na kumrudhia yule dada, aliiona na kuikwepa ikaenda kumpiga mgongoni mhudumu ambay ealikua anapita. Nilianza kutukana bila kujali tulikua wapi, mume wangu alinishika kwa nguvu na kunitoa nnje ili kuepuka aibu, mimi niliendelea kutukana mpaka aliponiingiza kwneye gari.
Hakufanya chochote aliendesha mpaka nyumbani, njia nzima nilikua nikimtukana na kumuambia kuwa tukifika nyumbani nataka talaka yangu kwani simtaki.
“yaqani unanipeleka kwenye shrehe yenu ili wkenda kunionyesha Malaya wenu, hapana, nimesema kuwa sitaki! Nataka talaka yangu!” Nilipiga kelele lakini mume wangu hakujibu neno hata moja, alikua kakasirika sana, alielekeza akili yake kwenye kuendesha gari tu. Tulifika nyumbani ndiyo akaanza kuongea akilalamika kuwa nilikua nimemuaibisha sana.
Ni kama aliamsha mashe4ani yangu, nilimtukana sana huku nikimpiga mangumi kila sehemu, alinishika lakini nilijipigiza na kujirusharusha sana. Mume wangu kuona vile alitoka nnje ili kuondoka, lakini sikutaka kumpa nafasi, nilimfauta huko huko, aliingia kwenye gari na kuiwasha, lakini kabla ya kuondoka nilifungua mlango wa abiria, mume wangua llishaondoa gari kwani geti lilikua bado halijafungwa wakati tunaingia ananiingiza ndani aliliacha wazi.
Sijui kama aakuniona au ilikuaje lakini nilishikilia mlango, nikawa kama nabembea, wakati anarudisha gari nyuma nikawa kama naburuzwa, nilianza kupiga kelee nikusema anataka kuniua. Mume wangu alishtuka, alisimamisha gari hataka na kunifuata.
“Kwanini unafanya upumbavu, unafanya utoto sana najaribu kukukwepa lakini naona kuna kitu unakitaka!” Aliniambia ka hasira huku akinishika kama vile ananikaba. Na mimi nilimshika na kuanza kumpiga kwa hasira.
“Kama ni mwanaume kweli basi nipige, si unajifanya kidume, nipige kama hujaoze jela na ndoa ndiyo naondoka.” Nilimuambia huku nikimsukuma sukuma.
“Nipig---“ niliendelea kuongea lakini mume wangu ahsira zilimzidi, nilinyamaziswha na kofi, kabla sijakaa vizuri nilishikwa na kurushwa juju kama takataka, ile nafika chini mume wangu alinikanyanga kwa mguu wa kulia, alianza kunipiga pale chini kwa hasira, alikua anatukana, anaongea maneno mengi, alinipiga sana bila huruma, alikua anapigakelele akiniambia kuwa amechoka na ataniua ili nayeye ajiue.
Alinipiga sana mpaka nikawa siwezi hata kunyanyuka, aliingia kwenye gari na kuniacha pale chini nikigalagala, alirudisha gari nyuma vibaya kiasi kwamba badala ya kutoka nalo getini basi alirudisha nyuma akagonga ukuta, nilikua nimelala chini, nina fahamu zangu sijiwezi lakini namuona namna anavyohangaika, anaenda mbele anarudi anagomba anageuza anagonga alifanya hivyo mpakaakafanikiwa kutoka, mimi mwili ulikua unauma, damu zinanitoka puani na mdomoni, mwisho nilishindwa hata kuhema nikapoteza fahamu.
ITAENDELEA...