Nilipoamua kuwa MPAGANI nilikuwa na sababu

Nilipoamua kuwa MPAGANI nilikuwa na sababu

Mkuu HANG'OLWA naomba nisaidie kujibu ingawa umemuuliza mleta mada! Nikweli wanapokwenda kuomba Mizimu kwenye mapango wanataja majina ya waliokufa Lengo nikufikisha ujumbe kwa MUNGU wao! Wakristo wanapomuomba MUNGU wanataja jina la YESU huyu nae alikufa ht km anaishi lkn amepitia MAUTI kwa Waislam pia wanapo muomba MUNGU wanamtaja MTUME S.A.W nivipi iwe shida kwa wapagani kuabudu Mizimu?
.....hao ni viongozi wao ambao ndio waliowaelekeza mambo kutoka kwa mungu wao mlezi,na yesu ,mussa .muhamad,suleiman hao wote walikuwa wanatajwa na wafuasi wao kabla hawajafa na mpaka vifo vyao!
 
Dini zilizoletwa na melikebu ni miyeyusho kabisa

Ni zaidi ya miyeyusho mkuu,..yaani hazina/zimeshindwa kabisa kujibu matatizo ya wanadamu na hasa waafrika ingawa sisi ndio mabingwa wa kujipendekeza kwenye dini hizi za kuletwa.
 
Surat Al-Kāfirūn (The Disbelievers) - سورة الكافرون

textEnlargeActive.gif

textShrinkInactive.gif

textSize.gif



بسم الله الرحمن الرحيم

109:1 to top

109_1.png
Sahih International
Say, "O disbelievers,

Swahili
Sema: Enyi makafiri!
​

109:2 to top

109_2.png
Sahih International
I do not worship what you worship.

Swahili
Siabudu mnacho kiabudu;
​

109:3 to top

109_3.png
Sahih International
Nor are you worshippers of what I worship.

Swahili
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
​

109:4 to top

109_4.png
Sahih International
Nor will I be a worshipper of what you worship.

Swahili
Wala sitaabudu mnacho abudu.
​

109:5 to top

109_5.png
Sahih International
Nor will you be worshippers of what I worship.

Swahili
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
​

109:6 to top

109_6.png
Sahih International
For you is your religion, and for me is my religion."

Swahili
Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
​

Hebu toa hii taka taka hapa.
 
Bado hatujapata jukwaa huru na watu huru wa kueleza ukweli kuhusiana na Dini

Ni jambo lisilokuwa la haki kujumlisha dini zote kama vile zinafanana
Ni vigumu sana kusema ukweli hapa kuhusiana na dini
Mada itafungwa kwa madai kuwa inaleta uchochezi
Lakini sio sawa na haya ni matokeo yake

Mkuu ni jambo la maana sana mtu kuwa na dini,lakini kwanini unadhani kuwa ni lazima kila mtu kuwa na dini yake?
 
Mada inahusu UPAGANI na DINI kiukweli hz dini zilizokuja na MTUMBWI zimetuletea matatizo makubwa! chakuckitisha zaidi wenye kutuletea wanafanya mambo mengine huku kwetu Inafikia watu wanategengana kisa? DINI kabla yakuja mambo hayo watu waliishi kwa AMANI naupendo MKUBWA lkn ss hali ni Mbaya Jiulize kwa nn ss hv maovu yanazidi ikiwa DINI ndo zinaenezwa kwelikweli 2we wakweli hz DINI nizawasaka TONGE2 dunia hii ucpochanganya nazako unakuwa FULSA kwa wengine!
 
Tamaduni zao wakatuletea eti nasie tunuwana kutetea hilo! Looh poor afrikans
 
Tumefindishwa kuwa mwili hufa ila nafsi huishi milele... Ina maana nafsi za mababu zangu woote bado zingali zikiishi n'a haiwezikana hata kidogo kuwa nafsi Hizi hazina cha kufanya n'a maisha yangu n'a uzao wangu... Naamini nafsi Hizi zinanifuatilia n'a ziko pamoja nami kwa kila jambo n'a Nina ogopa sana kuzidharau... Ninyi mnaziita mizimu n'a kuziamini mnaita ushirikina...ila mimi naamini hiyo ndio njia sahihi kabisa kuishi.... Mungu yupo nami namjua sana namuita NGULUVI...!!!!
 
Ndg yangu MJUVIkiTAMBO watu weupe wanatufanya cc maBWEGE wanatwambia tusiabudu mizimu yetu lkn wana2cctizia tuabudu ya kwao kwanini Na wao cnibinadamu km mababu zetu? vp mizimu yao iwe bora kuliko yetu!!! Yuko mjinga 1 kawaambia Zake atakae taka msaada wake anatakiwa afuate DINI yake ikafikia mahari akakataa kumsomesha Dadake kisa alikataa kuwa sehemu ya hiyo DINI upuuzi plus!
 
Bado hatujapata jukwaa huru na watu huru wa kueleza ukweli kuhusiana na Dini

Ni jambo lisilokuwa la haki kujumlisha dini zote kama vile zinafanana
Ni vigumu sana kusema ukweli hapa kuhusiana na dini
Mada itafungwa kwa madai kuwa inaleta uchochezi
Lakini sio sawa na haya ni matokeo yake

Mkuu ni jambo la maana sana mtu kuwa na dini,lakini kwanini unadhani kuwa ni lazima kila mtu kuwa na dini yake?

Mchungaji_salama...?
 
Hebu toa hii taka taka hapa.
Kukosa elimu ni tatizo kweli,yaani washindwa kutofautisha taka na maandishi.Halafu ndio mwasema mmesoma,aliyesoma anashindwa kuelewa hata lugha ya kiingereza au ya kiarabu.Matatizo ya kukimbia umande watu wasoma wewe wakimbia umande,matokeo yake wajasoma elimu ya watu wazima.Ujinga sijui utakwisha lini.
 
Wewe kweli huijui historia.Vita vya makabila vilikuwako na vilikuwa ni vibaya sana kuliko unavyofikiria.Wapo waliohama maeneo yao kwa vita hivyo.Historia ya kale inasema kuwa jamii ya wachaga inatokana na watu wa makabila mbali mbali ambao walihamia kwenye mteremko wa mlima Kilimanjaro baada ya kukimbia vita na wengine kukimbia baa la njaa.
Wahamiaji hao waliwazidi nguvu kivita wenyeji wa eneo hilo ambao walijulikana kama Koningo au Konyingo.
Kila eneo lilkuwa na Mangi wake,
ila Mangi Sina wa Kibosho,Rindi wa Moshi na Marealle wa Marangu walipata umaarufu Mkubwa,kutokana na jitihada zao za kutaka kuwa wafalme ili kutawala himaya nzima ya wachaga.Hata hivyo waligonga mwamba kwa kuwa hakuna Mangi aliyekuwa tayari kutawaliwa na kiongozi kutoka kundi jingine.
Hali ya kujihami na kuogopana inachukuliwa kama kielelezo kuwa chimbuko la wachaga linatokana na jamii na makabila tofauti yenye historia tofauti.
Kati ya mwaka 1750 na mwaka 1890 Wachaga walikuwa na vita vya mara kwa mara ,ambapo kila Mangi alitaka kutwaa eneo la mwenzake ili kuongeza ukubwa wa ardhi kuimarisha ngome yake kiuchumi.
Hadi mwanzoni mwa karne ya 19,wachaga waligawanyika katika makundi 30 na kila kundi lilikuwa na Mangi wake walijitenga mithili ya nchi 30 katika kisiwa kidogo.
Watu hao WALIWINDANA kila mmoja akimnyoeshea mwenzake kidole kwa uchokozi ya kutwaa mali na ardhiya kundi jingine.
Vita vya wachaga vilikwisha baada ya kuingia Wamisionary,kueneza dini ya Kikiristo pamoja na kuanzisha zao la kahawa.
Hivyo machifu waliweka silaha chini na kuelekeza nguvu zao zao kwenye kilimo ca kahawa.
Mangi Orombo,alikuwa mangi wa kwanza kuanzisha ngome yake katika kijji cha keni na kuunda jeshi,ambalo lilivamia himaya za machifu wengine na kufanikiwa kuteka eneo la Vunjo hadi mto Nanga.
Mangi sina alijenga ngome pia ya vita,eneo la kibosho,alijenga mji wa kiabiashara kati ya Waafrika na Waarabu,ambapo waarabu walimpa nguo na silaha kisha akatoa pembe za ndovu na vitu vingine vya thamani.
Nadhani wewe hujaelewa mada, mimi nazungumzia dini za mapokeo wewe unazungumzia historia ya wachaga....

Wapi na wapi......!
 
Kuna msemo niliusikia mahali unasema,mila inaua kuliko dini..na ndio maana wale ndugu zangu kule kasikazini kila mwisho wa mwaka wanaenda makwao kuendeleza mila ingawa wengi hudhani sababu ni sikukuu..pamoja na kwenda kwao makanisani na misikitini lakini bado wanajali mila zao.
 
Yesu alisema wazi kabisa hakuja kuleta amani duniani bali upanga (lk 12: 51) amani yake yeye ni kwa wale wanaomwamini tu, hata ukiamua kumkana Mungu usifikir utakua na amani, maana ipo roho ya Mungu ndani yako ambayo daima itakuhukumu.
 
_4.jpg


zamani enzi za ujima kabla ya ujio wa hizi dini za mapokea mababu zetu waliishi kwa amani na upendo huku wakiheshimiana na kuvumiliana.

Walikuwa wakiamini kwamba binadamu wote ni sawa na kila mmoja alikuwa akimthamini mwingine siyo kwa kile alicho nacho, bali kama binadamu aliyekamilika. Walikuwa wakitofautiana kwa nguvu ya hoja na siyo kwa hoja ya nguvu. Inapotokea kuhitilafiana, kama wanadamu walikuwa wakikaa chini na kuzungumza kwa busara na hekima na kumaliza tofauti zao.

Vikao vya usuluhishi vilikuwa vikiendeshwa na wazee wenye hekima na busara ambao walikuwa ni mahiri katika kulitizama jambo na kulipima kwa uzito wake. Pale mmoja anapokutwa amekosea alikuwa akipigwa faini ambapo mara nyingi ilikuwa ni mifugo.

Viapo na kulishwa yamini kimila vilikuwa vikitumika kutatua migogoro inayoonekana kukosa suluhu na yule aliyedanganya alikuwa akipata adhabu yake kulingana na aina ya kiapo. Hivyo, kulikuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa miongoni mwa jamii kwa sababu viapo vingi vilikuwa vinasababisha vifo katika familia au ukoo.

Wazee wetu walikuwa na imani zao ambazo zilikuwa na nguvu na waliziheshimu sana. Walikuwa wakiamini katika dini za asili za matambiko na kafara. Kupitia mizimu waliyokuwa wakiamini tangu kale walikuwa wakipata ishara mbalimbali kupitia ndoto na maono na walimudu kuchukua tahadhari kungali mapema.

Walikuwa wakipata ishara za maradhi, vifo, baa la njaa na hata tufani, gharika na ukame. Walikuwa wakichukua hatua za kuomba mizimu iwaepushe na dhahama hizo na mara nyingi walipewa masharti ambayo wakiyatekeleza walikuwa wakiepuka au kunusurika na majanga hayo.

Lakini leo hii,yote hayo yametoweka baada ya ujio wa hizi dini za mapokeo. Dunia imekuwa si salama tena, hofu imetanda, watu hawaaminiani tena. Dini tulizoletewa tuliambiwa kwamba, zitaleta amani na upendo hivyo tuachane na dini zetu za asili maana ni za kishenzi, zimegeuka kuwa angamio kwa vizazi vyetu.

Lakini kwa bahati mbaya kule walipotoka hawakuwa na huo upendo na amani waliyotuambia. Inashangaza kuona kwamba walikuwa wanajaribu kuzima moto kwa jirani il hali kwao kunateketea. Wazee wetu hawakuyajua hayo kutokana na ufinyu wa upatikanaji wa habari. Laiti kama wangetuletea dini hizi leo hii, sidhani kama wazee wetu wangewaelewa. Kwani naamini wangewauliza. Je huko mnakotuambia kuna asali na maziwa mbona kila uchao watu wanachinjana...?

Je wangekuwa na jibu gani?

Lakini wazee wetu hawakuwa wajinga, hawakukubali kirahisi kupoteza asili yao, walikataa kuwa watumwa wa kuabudu, wengi walidiriki kukimbilia msituni. Hata hivyo haikuwa rahisi kwao kuepuka utumwa huo. Walilazimishwa kwa mijeledi na wengine kunyongwa ili kuzipokea dini hizo maana ndizo zenye kumjua mungu.

Naam, taifa likagawanywa vipande vipande kila mwenye dini na dhehebu lake akitupa nyavu kujaribu kuvua waumni kwa ajili ya kuongeza idadi ya waumini.

Wazee wetu wakalazimika kutupa pembe, tunguli na ngozi za wanyama walizotumia katika kufanya matambiko. Mapango yaliotumika kuomba mizimu ikatelekezwa wakavalishwa suti, kanzu na barkhashia ili kumuabudu mungu wao.

Zile kumbukumbu za kuwakumbuka mababu zao waliotangulia mbele ya haki zikakemewa kwamba hazifai kabisa maana hao ni wafu, lakini wakalazimishwa kuwakumbuka kina paulo, yahaya, musa, said na omar na aboubakar sadik...... Kebehi gani hii..............!

Siku hizi dini zao walizotuletea zimetumika kama kitega uchumi kuwakamua wanyonge na masikini. Mazingaombwe siku hizi ndio mpango mzima. Yule ambaye ni mahiri katika kufanya mazingaombwe ndiye ambaye huvua waumni wengi. Umasikini wa kifikra umegeuzwa mtaji na wajanja. Hivi sasa wananyang'anywa hata kile kidogo walicho nacho.

Yupo mwanafalsafa mmoja alipata kusema kwamba heri kukosa mali kuliko kukosa akili, lakini nawashangaa wananchi wenzangu maana naona wamekosa vyote, yaani mali na akili. Haiwezekani mtu akujie kwa jina la dini kisha umpe hata kile kidogo ulicho nacho. Lakini pia unanyimwa haki ya kuhoji matumizi ya hicho ulichotoa maana unatishwa kwamba umemtolea mungu, na mungu haulizwi ametumia vipi...!

Nabaki najiuliza ni kitu gani wamekosa wanadamu hawa. Mungu aliwaumba wakiwa ni binadamu kamili wenye viungo vyote na akili timamu, lakini mtu akiwajia kwa jina la dini na kuwatisha wanakuwa dhalili na wanyonge wakifuata kila wanachoambiwa bila hata kuhoji.... Ujinga gani huu...!

Dini zao walizotuletea zimeigeuza dunia imekuwa si salama tena, vita kila kona, visasi, chuki na husuda zimashamiri. Kama tungeendelea kubakia na dini zetu za asili kusingekuwa na al qaida wala al shabaab, kusingekuwa na kutokuaminiana, kusingekuwa na chuki za kidini, kusingekuwa na matabaka, maana hata huko kwenye nyumba zao za ibada kuna matabaka, yule anayeonekana kuwa ni tajiri huwekwa mbele na hata akizungumza pumba hushangiliwa na kupigiwa makofi. Lakini pia kusingekuwa na kutokuaminiana.

Mimi naamini katika dini za asili, wengine huita upagani na ninajivunia kuwa hivyo, sina akili ya kushikiwa na ninafurahia maisha kama kawaida, ninafanya matambiko na kutoa kafara kama kawaida na maisha yangu ni mazuri na sina hofu ya kesho kwa sababu hakuna hata mmoja kati yetu anayeweza kusimama na kusema anaijua kesho.

Copy to eiyer, nyani ngabu, kiranga, bujibuji, kaizer, faizafoxy, figganigga, ladyfurahia, cacico, snowhite, gfsonwin, heaven on earth, kongosho

amkeni....
what a piece of junk.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani wewe hujaelewa mada, mimi nazungumzia dini za mapokeo wewe unazungumzia historia ya wachaga....

Wapi na wapi......!
Wewe ulisema watu wallishi kwa amani wakati kabla ya kuja waletaji dini,nakuonyesha jinsi watu walivyoishi,waliishi kivita vita,soma vizuri post yangu.
 
Ni kweli mkuu, kuna dini moja kati hizo zilizoletwa na mitumbwi, waumini wake huabudu picha ya mzungu mwenye ndevu nyingi pamoja na nywele ndefu, sijui wenyewe wanamuita "bwana", wakati mwingine pia humlilia huyo bwana wao pamoja na mama yake!
 
jiulize hivi,huyo aliekuumba wewe ni nani?kabla ya hapo (hujazaliwa)ulikuwa wapi,unayajua yajayo?unaweza ukasema mimi sitaki kuumwa na ikawa hivyo,kama sivyo basi mwenye kumiliki hivyo vyote ni m'mungu muumba wa vyote tunavyoviona na hata vile hatuvioni,yeye ameweka utaratibu wake ambao sisi tunapaswa tuufuate,na huo utaratibu au mfumo alitutaka tuufuate ndo huu sisi tunaita dini,na pia tumeambiwa hakuna kulazimishana ktk dini au mfumo huo.huyo ndio m,mungu......
angaweka mifumo tusingeuana kwa kusingizia hiyo mifumo.
 
Back
Top Bottom