Nilipoamua kuwa MPAGANI nilikuwa na sababu

Nilipoamua kuwa MPAGANI nilikuwa na sababu

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2009
Posts
268
Reaction score
124
_4.jpg


Zamani enzi za ujima kabla ya ujio wa hizi dini za mapokea mababu zetu waliishi kwa amani na upendo huku wakiheshimiana na kuvumiliana.

Walikuwa wakiamini kwamba binadamu wote ni sawa na kila mmoja alikuwa akimthamini mwingine siyo kwa kile alicho nacho, bali kama binadamu aliyekamilika. walikuwa wakitofautiana kwa nguvu ya hoja na siyo kwa hoja ya nguvu. Inapotokea kuhitilafiana, kama wanadamu walikuwa wakikaa chini na kuzungumza kwa busara na hekima na kumaliza tofauti zao.

Vikao vya usuluhishi vilikuwa vikiendeshwa na wazee wenye hekima na busara ambao walikuwa ni mahiri katika kulitizama jambo na kulipima kwa uzito wake. Pale mmoja anapokutwa amekosea alikuwa akipigwa faini ambapo mara nyingi ilikuwa ni mifugo.

Viapo na kulishwa yamini kimila vilikuwa vikitumika kutatua migogoro inayoonekana kukosa suluhu na yule aliyedanganya alikuwa akipata adhabu yake kulingana na aina ya kiapo. Hivyo, kulikuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa miongoni mwa jamii kwa sababu viapo vingi vilikuwa vinasababisha vifo katika familia au ukoo.

Wazee wetu walikuwa na imani zao ambazo zilikuwa na nguvu na waliziheshimu sana. Walikuwa wakiamini katika dini za asili za matambiko na kafara. Kupitia mizimu waliyokuwa wakiamini tangu kale walikuwa wakipata ishara mbalimbali kupitia ndoto na maono na walimudu kuchukua tahadhari kungali mapema.

Walikuwa wakipata ishara za maradhi, vifo, baa la njaa na hata tufani, gharika na ukame. walikuwa wakichukua hatua za kuomba mizimu iwaepushe na dhahama hizo na mara nyingi walipewa masharti ambayo wakiyatekeleza walikuwa wakiepuka au kunusurika na majanga hayo.

Lakini leo hii,yote hayo yametoweka baada ya ujio wa hizi dini za mapokeo. Dunia imekuwa si salama tena, hofu imetanda, watu hawaaminiani tena. Dini tulizoletewa tuliambiwa kwamba, zitaleta amani na upendo hivyo tuachane na dini zetu za asili maana ni za kishenzi, zimegeuka kuwa angamio kwa vizazi vyetu.

Lakini kwa bahati mbaya kule walipotoka hawakuwa na huo upendo na amani waliyotuambia. Inashangaza kuona kwamba walikuwa wanajaribu kuzima moto kwa jirani il hali kwao kunateketea. Wazee wetu hawakuyajua hayo kutokana na ufinyu wa upatikanaji wa habari. laiti kama wangetuletea dini hizi leo hii, sidhani kama wazee wetu wangewaelewa. Kwani naamini wangewauliza. Je huko mnakotuambia kuna asali na maziwa mbona kila uchao watu wanachinjana...?

Je wangekuwa na jibu gani?

Lakini wazee wetu hawakuwa wajinga, hawakukubali kirahisi kupoteza asili yao, walikataa kuwa watumwa wa kuabudu, wengi walidiriki kukimbilia msituni. Hata hivyo haikuwa rahisi kwao kuepuka utumwa huo. Walilazimishwa kwa mijeledi na wengine kunyongwa ili kuzipokea dini hizo maana ndizo zenye kumjua Mungu.

Naam, Taifa likagawanywa vipande vipande kila mwenye dini na dhehebu lake akitupa nyavu kujaribu kuvua waumni kwa ajili ya kuongeza idadi ya waumini.

Wazee wetu wakalazimika kutupa pembe, tunguli na ngozi za wanyama walizotumia katika kufanya matambiko. Mapango yaliotumika kuomba mizimu ikatelekezwa wakavalishwa suti, kanzu na barkhashia ili kumuabudu Mungu wao.

Zile kumbukumbu za kuwakumbuka mababu zao waliotangulia mbele ya haki zikakemewa kwamba hazifai kabisa maana hao ni wafu, lakini wakalazimishwa kuwakumbuka kina Paulo, Yahaya, Musa, Said na Omar na Aboubakar Sadik...... Kebehi gani hii..............!

Siku hizi dini zao walizotuletea zimetumika kama kitega uchumi kuwakamua wanyonge na masikini. Mazingaombwe siku hizi ndio mpango mzima. Yule ambaye ni mahiri katika kufanya mazingaombwe ndiye ambaye huvua waumni wengi. Umasikini wa kifikra umegeuzwa mtaji na wajanja. Hivi sasa wananyang'anywa hata kile kidogo walicho nacho.

Yupo mwanafalsafa mmoja alipata kusema kwamba heri kukosa mali kuliko kukosa akili, lakini nawashangaa wananchi wenzangu maana naona wamekosa vyote, yaani mali na akili. haiwezekani mtu akujie kwa jina la dini kisha umpe hata kile kidogo ulicho nacho. Lakini pia unanyimwa haki ya kuhoji matumizi ya hicho ulichotoa maana unatishwa kwamba umemtolea Mungu, na Mungu haulizwi ametumia vipi...!

Nabaki najiuliza ni kitu gani wamekosa wanadamu hawa. Mungu aliwaumba wakiwa ni binadamu kamili wenye viungo vyote na akili timamu, lakini mtu akiwajia kwa jina la dini na kuwatisha wanakuwa dhalili na wanyonge wakifuata kila wanachoambiwa bila hata kuhoji.... Ujinga gani huu...!

Dini zao walizotuletea zimeigeuza dunia imekuwa si salama tena, vita kila kona, visasi, chuki na husuda zimashamiri. Kama tungeendelea kubakia na dini zetu za asili kusingekuwa na AL QAIDA wala AL SHABAAB, kusingekuwa na kutokuaminiana, kusingekuwa na chuki za kidini, kusingekuwa na matabaka, maana hata huko kwenye nyumba zao za ibada kuna matabaka, yule anayeonekana kuwa ni tajiri huwekwa mbele na hata akizungumza pumba hushangiliwa na kupigiwa makofi. Lakini pia kusingekuwa na kutokuaminiana.

Mimi naamini katika dini za asili, wengine huita upagani na ninajivunia kuwa hivyo, sina akili ya kushikiwa na ninafurahia maisha kama kawaida, ninafanya matambiko na kutoa kafara kama kawaida na maisha yangu ni mazuri na sina hofu ya kesho kwa sababu hakuna hata mmoja kati yetu anayeweza kusimama na kusema anaijua kesho.

Copy to Eiyer, Nyani Ngabu, Kiranga, Bujibuji, Kaizer, FaizaFoxy, figganigga, ladyfurahia, cacico, snowhite, gfsonwin, Heaven on earth, Kongosho

Amkeni....
 
Last edited by a moderator:
jiulize hivi,huyo aliekuumba wewe ni nani?kabla ya hapo (hujazaliwa)ulikuwa wapi,unayajua yajayo?unaweza ukasema mimi sitaki kuumwa na ikawa hivyo,kama sivyo basi mwenye kumiliki hivyo vyote ni m'mungu muumba wa vyote tunavyoviona na hata vile hatuvioni,yeye ameweka utaratibu wake ambao sisi tunapaswa tuufuate,na huo utaratibu au mfumo alitutaka tuufuate ndo huu sisi tunaita dini,na pia tumeambiwa hakuna kulazimishana ktk dini au mfumo huo.huyo ndio m,mungu......
 
jiulize hivi,huyo aliekuumba wewe ni nani?kabla ya hapo (hujazaliwa)ulikuwa wapi,unayajua yajayo?unaweza ukasema mimi sitaki kuumwa na ikawa hivyo,kama sivyo basi mwenye kumiliki hivyo vyote ni m'mungu muumba wa vyote tunavyoviona na hata vile hatuvioni,yeye ameweka utaratibu wake ambao sisi tunapaswa tuufuate,na huo utaratibu au mfumo alitutaka tuufuate ndo huu sisi tunaita dini,na pia tumeambiwa hakuna kulazimishana ktk dini au mfumo huo.huyo ndio m,mungu......

Mkuu sijasema dini yangu haimjui Mungu. Usininukuu vibaya..
Hata dini yangu ya sili inamjua Mungu na ni yeye pekee ninayemuabudu kaara na matambiko ni njia tu ya kuweza kuwasiliana naye na ndio maana sisi tunamuita Mlungu kama wamasaai wanavyomuita Ngai.
 
Yes before colonial era tulikuwa na dini zetu,ancestors wetu walikuwa na dini zao lakini look what colonialist done...wakatuaminisha dini zetu ni za kishenzi,aibu na za kishetani,tukakubali wakatuletea dini zao za kistaarabu...

Ustaarabu huu ndio tunaoutumia kuona mtu wa imani fulani siyo ila wa imani hii ni shahihi na kwamba dini ile ndiyo itakayompeleka fulani peponi na hii itamfikisha yule jehanamu! Ni mtoro wa historia tu ama aliyezaliwa kipindi 'dini za kistaarabu' zilipokwisha waingia watu ndiye anasiyejua ukweli huu ama anaujua ila anaogopa kuonekana 'mshamba' kwa wenye dini zao!

Enzi zile za pre colonial era pamoja na explorers,wafanyabiashara,missionaries walikuwa miongoni wa waliofanikisha ukoloni wakiwa watangulizi.Walitumia dini kurubuni na kupumbaza watu ambao nao walikuwa mazuzu kwa kudhani wakienda against wanamkosea Mungu!

Kupitia dini tulitawaliwa kikoloni na kupitia dini tunaendelea kuvurugwa na kuvurugana sisi kwa sisi na nionavyo hawa mabwana baada ya sisi kufa na miili yetu kuharibika watakuja kwa namna nyingine wakitumia dini hizi hizi walizozileta wao! Let me remain Sceptist nitaujua tu ukweli mbele ya safari kama kuna maisha baada ya kifo!
 
Yes before colonial era tulikuwa na dini zetu,ancestors wetu walikuwa na dini zao lakini look what colonialist done...wakatuaminisha dini zetu ni za kishenzi,aibu na za kishetani,tukakubali wakatuletea dini zao za kistaarabu...

Ustaarabu huu ndio tunaoutumia kuona mtu wa imani fulani siyo ila wa imani hii ni shahihi na kwamba dini ile ndiyo itakayompeleka fulani peponi na hii itamfikisha yule jehanamu! Ni mtoro wa historia tu ama aliyezaliwa kipindi 'dini za kistaarabu' zilipokwisha waingia watu ndiye anasiyejua ukweli huu ama anaujua ila anaogopa kuonekana 'mshamba' kwa wenye dini zao!

Enzi zile za pre colonial era pamoja na explorers,wafanyabiashara,missionaries walikuwa miongoni wa waliofanikisha ukoloni wakiwa watangulizi.Walitumia dini kurubuni na kupumbaza watu ambao nao walikuwa mazuzu kwa kudhani wakienda against wanamkosea Mungu!

Kupitia dini tulitawaliwa kikoloni na kupitia dini tunaendelea kuvurugwa na kuvurugana sisi kwa sisi na nionavyo hawa mabwana baada ya sisi kufa na miili yetu kuharibika watakuja kwa namna nyingine wakitumia dini hizi hizi walizozileta wao! Let me remain Sceptist nitaujua tu ukweli mbele ya safari kama kuna maisha baada ya kifo!
Kweli mkuu.

Ni wachache sana wanoweza kuuona ukweli huu. Mada za aina hii huwa watu wanazikwepa sana kwa sababu ya sumu hiyo waliyolishwa. Kuna matatizo mengi sana yaliyoletwa na hizi dini za mapokeo na wengi tumesoma hata huko shuleni, lakini tunaambiwa ni historia na yalishapita tuyasahau, lakini wanasahau kwmaba huwa historia inajirudia na huu ndio mwanzo.

Namini wajukuu zetu watakuja kuhoji siku moja maana pamoja na kwamba wengi tunajitia hamnazo kukana dini zetu za asili lakini wapo wengi tena kiasi cha kutosha huenda huko walikozaliwa kutambika kimya kimya.
 
Yaah! goMKULU TEGELEZENI umesomeka! DINI hz zakigeni zimetuletea MAJANGA sn! waliwaambia mababu zetu DINI zao zilikuwa nizakishenzi 7bu wanaabudu MIZIMU na mababu zetu kwakutokuwa na Elimu wakawaamini Chakushangaza hata hzo DINI zakigeni pia wanaabudu MIZIMU jiulize ni NABII au MTUME gani ambae hajafa hata YESU km anaishi hadi leo lkn pia alikufa! ss hv tumepoteza kila kitu hatujui tucmamie wapi!!
 
Mkuu sijasema dini yangu haimjui Mungu. Usininukuu vibaya..
Hata dini yangu ya sili inamjua Mungu na ni yeye pekee ninayemuabudu kaara na matambiko ni njia tu ya kuweza kuwasiliana naye na ndio maana sisi tunamuita Mlungu kama wamasaai wanavyomuita Ngai.
mimi sijakuambia haimjui mungu,nilitaka tu ujiulize ww ,mm navyojua matambiko ni pamoja kwenda kuomba kwenye mapango,makabulini na kutaja taja watu waliokufa ndo hapo huwa na jiuliza huyo mungu wenu anaitajwe?na sifa zake ni zipi ??ukirudi unieleweshe...ili tuendelee
 
Hii picha haina (lacks) ujumbe unaotaka kuufikisha!...aidha unataka kuidanganya jamii kwa Pope kwenye picha hii alikuwa anajihusisha na mambo ya ushirikina....Nop!
Kwa tunaojua hii picha inaonyesha UTAMADUNISHO, au KANISA MAHALIA!
Benedict.jpg
 

[h=1]Surat Al-Kāfirūn (The Disbelievers) - سورة الكافرون[/h]
textEnlargeActive.gif

textShrinkInactive.gif

textSize.gif



بسم الله الرحمن الرحيم

109:1 to top

109_1.png
Sahih International
Say, "O disbelievers,

Swahili
Sema: Enyi makafiri!
​

109:2 to top

109_2.png
Sahih International
I do not worship what you worship.

Swahili
Siabudu mnacho kiabudu;
​

109:3 to top

109_3.png
Sahih International
Nor are you worshippers of what I worship.

Swahili
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
​

109:4 to top

109_4.png
Sahih International
Nor will I be a worshipper of what you worship.

Swahili
Wala sitaabudu mnacho abudu.
​

109:5 to top

109_5.png
Sahih International
Nor will you be worshippers of what I worship.

Swahili
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
​

109:6 to top

109_6.png
Sahih International
For you is your religion, and for me is my religion."

Swahili
Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
​
 
Mkuu HANG'OLWA naomba nisaidie kujibu ingawa umemuuliza mleta mada! Nikweli wanapokwenda kuomba Mizimu kwenye mapango wanataja majina ya waliokufa Lengo nikufikisha ujumbe kwa MUNGU wao! Wakristo wanapomuomba MUNGU wanataja jina la YESU huyu nae alikufa ht km anaishi lkn amepitia MAUTI kwa Waislam pia wanapo muomba MUNGU wanamtaja MTUME S.A.W nivipi iwe shida kwa wapagani kuabudu Mizimu?
 
Wewe kweli huijui historia.Vita vya makabila vilikuwako na vilikuwa ni vibaya sana kuliko unavyofikiria.Wapo waliohama maeneo yao kwa vita hivyo.Historia ya kale inasema kuwa jamii ya wachaga inatokana na watu wa makabila mbali mbali ambao walihamia kwenye mteremko wa mlima Kilimanjaro baada ya kukimbia vita na wengine kukimbia baa la njaa.
Wahamiaji hao waliwazidi nguvu kivita wenyeji wa eneo hilo ambao walijulikana kama Koningo au Konyingo.
Kila eneo lilkuwa na Mangi wake,
ila Mangi Sina wa Kibosho,Rindi wa Moshi na Marealle wa Marangu walipata umaarufu Mkubwa,kutokana na jitihada zao za kutaka kuwa wafalme ili kutawala himaya nzima ya wachaga.Hata hivyo waligonga mwamba kwa kuwa hakuna Mangi aliyekuwa tayari kutawaliwa na kiongozi kutoka kundi jingine.
Hali ya kujihami na kuogopana inachukuliwa kama kielelezo kuwa chimbuko la wachaga linatokana na jamii na makabila tofauti yenye historia tofauti.
Kati ya mwaka 1750 na mwaka 1890 Wachaga walikuwa na vita vya mara kwa mara ,ambapo kila Mangi alitaka kutwaa eneo la mwenzake ili kuongeza ukubwa wa ardhi kuimarisha ngome yake kiuchumi.
Hadi mwanzoni mwa karne ya 19,wachaga waligawanyika katika makundi 30 na kila kundi lilikuwa na Mangi wake walijitenga mithili ya nchi 30 katika kisiwa kidogo.
Watu hao WALIWINDANA kila mmoja akimnyoeshea mwenzake kidole kwa uchokozi ya kutwaa mali na ardhiya kundi jingine.
Vita vya wachaga vilikwisha baada ya kuingia Wamisionary,kueneza dini ya Kikiristo pamoja na kuanzisha zao la kahawa.
Hivyo machifu waliweka silaha chini na kuelekeza nguvu zao zao kwenye kilimo ca kahawa.
Mangi Orombo,alikuwa mangi wa kwanza kuanzisha ngome yake katika kijji cha keni na kuunda jeshi,ambalo lilivamia himaya za machifu wengine na kufanikiwa kuteka eneo la Vunjo hadi mto Nanga.
Mangi sina alijenga ngome pia ya vita,eneo la kibosho,alijenga mji wa kiabiashara kati ya Waafrika na Waarabu,ambapo waarabu walimpa nguo na silaha kisha akatoa pembe za ndovu na vitu vingine vya thamani.
 
Back
Top Bottom