Nilimwambia atakufa akafa kweli

Duh..Mkuu mshana unatutisha humu?

Maana utafanya watu wakuogope zaidi ya kawaida
 
Ewaaa....

Damu ya Yesu itufunike kila Mshana akitaka kuturoga aone taswira yake mwenyewe.... Mungu wewe ni Mkuu, naomba utulinde na babu yangu, tufiche kwenye mbawa zako mfalme wa amani.... Katika jina la Yesu naomba na kuamini Aaaaammmeenn

Eiiimeeeeeennnn!!
 
Hivi kumbe mwenye mamlaka ya kufuta kesi ni mlalamikaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sishangai, Yuko Boss wangu mmoja akikwambia kitu lazima kitokee, akikwambia huyu atavunja hiki, basi kinavunjika, akikwambia huyu ataleta madhara haya kwenye kazi lazima itokee..

Na mwenyewe anasemaga msinikere, Mimi na mdomo mbaya!
kiki hizo!
 
haya mambo yanawezekana kuwepo

mamangu alinambia unaenda shule lakini hauna muda mrefu utafukuzwa (nilikuwa nimemkera jambo fulani) na kweli wakanifukuza wala hakuonesha kushangaa.

aliwahi mwambia dadangu maneno flani na yakawa ivo, huwa anaogopa kunena mabaya kwa mtu maana hutokea.

kilicho nishangaza ni nduguze wakiugua ama watoto wao humpigia simu na kumuomba awanenee mazuri na kuwaombea wapate nafuu na kupona na huwa ivo.

mkuu leo niambie ni uchawi ama ni nini?
 
Hivi kumbe mwenye mamlaka ya kufuta kesi ni mlalamikaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
Iko hivi baada ya kutokea lile timbwili simu ilipigwa kituo kidogo cha Mwenge wakaja askari wa patrol na defender, wakajaribu kumtuliza lakini akawa kiburi na kuwaporomoshea matusi mazito kabisa.. Kwahiyo akabebwa huku sisi tukidrive,
Tulipofika Mwenge akazidisha fujo ndio tukaenda mabatini, kesi ikafunguliwa mimi nikiwa mlalamikaji na kutakiwa kurudi Jumatatu yake
Niliporudi nikaulizwa kama nina interest ya kuendelea na ile kesi nikasema hapana, ikafutwa
Mlalamikaji ana haki hiyo ila jamhuri ikiamua inaweza kufungua kesi upya kwakuwa msamaha haufuti kosa husika kwa mujibu wa katiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…