Kuna kijana alikuja kupata huduma ofisini kwetu akawa amechukua namba yangu yeye ana ofisi yake huko town anauza viatu vya kike.
Mwanzoni alikuwa mpole tukawa tunawasiliana vizuri tu, kwa vile ana ofisi yake nikajua atanipa ushauri mzuri wa biashara na kujiajiri hivyo nikawa nimemuamini, na kumchukulia kama kaka au rafiki wa kiume.
Ikatokea siku akanialika kwake nikitoka kazini, kwakuwa siyo mbali na ofisini kwetu nilivyotoka nikaenda, tukakaa tukapiga story tukala chakula, baada ya hapo nashangaa mtu mara anisogelee atake kunishika, akaninyanyua kanipeleka chumbani weee hapa nilibadilika nikawa mbogo, maana mimi sikujia hayo mambo iweje atake kunibaka bila ridhaa yangu kisa nimekuja kwake ndiyo aone kuwa nimekubali kila kitu.
Tulivutana sana hiyo siku nakumbuka, mimi hadi nimefura kwa hasira ndiyo kumlazimisha akanipeleka home maana ana usafiri wake, tangu hiyo siku nimetoka sijapokea simu yake wala kujibu meseji zake, nimemuona ni mwanaume wa hovyo sana tangu lini mapenzi yakalazimishwa? Mwache mwanamke akupe kwa kuridhia mwenyewe.
Labda nikuulize umri ili nikujaji vizuri!
Kama mwanamke matured huwa anazisoma alama za nyakati usoni kwa mkware na kuzitambua mapema hata kabla jamaa hajaanza 'kusomesha'.
Iweje wewe hadi uende nyumbani kwa mwanaume bila kuhisi dhamira yake?
Utetezi wangu kwako utaupata iwapo kama umejaliwa uso wenye tabasamu la huba ulilovishwa la kudumu na muumba!
Kama una uso wenye umbo la tabasamu ya namna hiyo, basi jamaa alikuhisi wewe ni 'easygoing' na kuwa tangia mlipoonana alihisi kwa upumbafu wake kuwa umemuelewa mapema na unajilengesha kumtaka!
Mara nyingi wanaume wajinga hukosea mshesabu namna hiyo na kunasa kwenye tundu bovu, msamee ili maisha yaendelee!
Sikiliza, mapenzi siyo ugomvi wala uhasama, mapenzi ni sanaa ya kutumia akili sana, haihitaji hasira wala jazba!
Unaujua mchezo wa draft, ndiyo mapenzi namna yalivyo, hayataki hasira!
Fungua simu pamoja na mawasiliano mengine kwake, mpokelee msg zake na stori ziendelee.
Kwani mkiendeleza mawasiliano ndiyo tiketi ya kupakuliwa na kula bila kunawa?
Huyo domo zenge ningelimfahamu, ningelimnanga sana, katuangusha sana wanachama wenzake.
Kashindwaje kukutongoza pole pole na kistaarabu kisha akupate kukidhi kiu yake kama alikutamani, shida iko wapi hapo?