Nilikuwa mdau mkubwa wa Vpn za free internet ila nikasanda, nililazimika nizihame moja kwa moja, kutumia vpn hapa bongo yahitaji moyo

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Off course vpn za kutumia internet bure zina faida zake ikiwemo kuokoa gharama na nikiri niliwahi kuwa mdau lakini kuna kipindi nilichoka aisee, ilibidi nizihame moja kwa moja.

-siku yoyote inafungiwa hakuna uhakika itadumu

-Hapa bongo hatuna wabunifu wa kubuni mbinu zao kwa vpn ili hata zikifungiwa wao watoboe tundu lingine, wengi wanadownload mafile mengi sana ya nchi za zingine wanajaribu moja moja ama wanajaza vpn nyingi wanajaribu moja moja, mitandao ikishajua hako kambinu wakiziba ndo basi tena,

-unakuta mtandao unakubali vpn ila unaweza kutumia mb 100 tu kwa siku au wiki

-vpn zinamaliza sana chaji

-Kuna vpn hazipo stable zinakata kata inabidi uwe unazima na kuwasha kila mara

-speed nayo huwa changamoto, uaweza kuta mtandao ni moto lakini ukitumia vpn ni slow kama konokono

-kuwasha hotspot ili uunge vifaa vingine kwa wifi ni changamoto, ni mpaka uweke vikorombwezo vya ziada

-vpn zingine kutumika ni asubuhi tu

-matapeli wa vpn ni wengi, watakudanganya wana vpn nzuri na ukijiroga kuwatumia hela unaambulia block ama kutumiwa vpn mdebwedo zenye matatizo kama speed kobe

-masnich nao hawapo mbali wakiona mnatumia internet bure, ni roho za chuki na wivu kutopenda kuona wengine wanafaidi, wao wanaenda kuchoma wazi wazi kwenye comments za page za mitandao ya simu wanatoa ushirikiano utadhani ni waajiri wa hayo makampuni, just imagine!! 😂😂..

Kwa msoto huu nilikubali yaishe tu nikajongea taratibu kwenye mfumo rasmi.
 
Tafuta hela
Sio kukimbilia kutafuta pesa tu, kuwa informed nako ni muhimu.

Nipo tigo post paid niliingia mikataba ile ya zamani nalipia shilingi 750 kwa gb.

Pia kuna rafiki yangu yupo sehemu ina waya wa simu ya mezani ttcl, ule waya huwa unabeba ADSL internet yeye aliwekewa router hatumii tena simu ya mezani, analipia elf 25 tu kwa mwezi unlimited internet japo ni ya zamani huwezi linganisha na fibre ya sasa.
 
Niliwahi kupata zari la unlimited data kipindi fulani kwenye psiphon lakini baada ya siku kadhaa wakaistukia wakakata server.

Baada ya hapo Vpn nazo kutananazo zimekuwa miyeyusho, speed ya kobe afu ads kibao.

Afu kama ulivyosema yani simu muda wote iko hot kama simu ya operator kiwanda cha steel.
 
Sio kukimbilia kutafuta pesa tu, kuwa informed nako ina save,

Nipo tigo post paid niliingia mikataba ile ya zamani nalipia shilingi 750 kwa gb.

Pia kuna rafiki yangu yupo sehemu ina nguzo za simu za ttcl mezani analipia elf 25 tu kwa mwezi anapewa unlimited internet ADSL.
Mkuu msaada kidogo kuhusu post paid inakuwaje
 
Mkuu msaada kidogo kuhusu post paid inakuwaje
 
-masnich nao hawapo mbali wakiona, roho za chuki na wivu kutopenda kuona wengine wanafaidi, wao wanaenda kuchoma wazi wazi kwenye comments za page za mitandao ya simu wanatoa ushirikiano utadhani ni waajiri wa hayo makampuni, just imagine!! ..


PARAGRAPH IMEANDIKWA KWA UCHUNGU SANA
Hao watu ni kisimpite (wambeya) wenye ohd za usnitch
 
masnich nao hawapo mbali wakiona mnatumia internet bure, ni roho za chuki na wivu kutopenda kuona wengine wanafaidi, wao wanaenda kuchoma wazi wazi kwenye comments za page za mitandao ya simu wanatoa ushirikiano utadhani ni waajiri wa hayo makampuni, just imagine!! 😂😂..
🤣🤣🤣
 
Niliwahi kupata zari la unlimited data kipindi fulani kwenye psiphon lakini baada ya siku kadhaa wakaistukia wakakata server.

Baada ya hapo Vpn nazo kutananazo zimekuwa miyeyusho, speed ya kobe afu ads kibao.

Afu kama ulivyosema yani simu muda wote iko hot kama simu ya operator kiwanda cha steel.
Mm Kuna Moja natumia Sasa huu mwezi 3 kimya kimya
 
Back
Top Bottom