NILIFANYIWA HIVI NIKIWA SEKONDARI...

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,797
6,795
Habari wana chit chat

Katika wakati huu wa mvua nimejikuta nakumbuka nilichofanyiwa 2006 nilipokuwa form 3.

Mwaka huo kule Kibosho kulikuwa na mvua mfululizo hatari alafu baridi na ukungu. kipindi icho nimehamia alafu hali ya hewa mbaya nisiyoitarajia.

Mimi shida yangu nilikuwa siwezi oga maji ya baridi(kibosho baridi sana). Mwezi wa nne mpaka wa sita kulikuwa mvua nyingi.

Nikitaka kuoga kama jua lipo nakaa kwenye jiwe moja hivi naota likijificha nyuma ya mawingu basi nduki bafuni. Jua likitoka ndo naoga ilikuwa policy yangu.

Mwezi wa nne mpaka sita ilikuwa mvua na mimi sikuoga kabisa ivyo nikawa natoka harufu plus harufu za miguu.

Siku moja tukafanya general cleanliness basi tukapewa omo nyingi. usiku ulipofika nikapata kashkash.

siku hiyo narudi tu bwenini wakaniambush wakanibebe juu juu wakanitumbukiza kwenye pipa. wakanitoa, na kwa kuwa walikuwa wameweka maji plus omo wakaanza kuniogesha pale nje. wakaniogesha na kila aina walichookota mpaka brush za chooni, za miguu, za buibui, ma lapulapu ya
 
ya kuoshea masufuria, madodoki na steel wire. siku ile nilikoma.

sasa kelele zilivyozidi wakanichukua wakanitumbukiza kwenye pipa tena. kwa kuwa nilikuwa nimeumia na michubuko basi nikatulia huko huko

usiku ule ulikuwa mrefu kwangu kesho yake asubuhi nikatangazwa kuwa mimi ndo mchafu shule nzima.

japokuwa hii sifa mpaka wenzangu wanaikumbuka mpaka leo ila siipendi

nawasilisha
 
pole. kweli tuliwafanyia hivyo wengi! na wale waliokuaa wanavuanguo then wanaosha mkono mmoja... mguu mmoja ..... mguu wa pili...... mkono wa pili


tinawamwagia maji mgongoni. kuna mmoja aliwahi kudondoka kwa shock ya maji baridi. so ujanja ilikuwa ukifika tu bafuni unawahi mwenyewe kujimwagia maji kabla watu hawajaanza kukuwazia.
 

Umenikumbusha Minaki class 2010/2012.

Mirambo dormitory kuna mduanzi mmoja alikuwa hapendi kuoga wala kufua. Ilifkia hatua hadi room yake ikàanza kuwa na wadudu huku ikitoa harufu sasa ile hali ikawa kero kwa roommate wake. Akaja kuomba ushauri afanyaje.

Tulichofanya ni kuwahi kutoka class, tukamlowekea nguo zake zote hadi mashuka alivyokuja kuuliza tukamchana tu ukweli. Basi ilimbidi tu kufua nguo zake na kuoga alipomaliza. Btw ilimsaidia kwa kiasi fulani kubadilika.

Boarding school raha sana, kuna vingi sana vya kujifunza huko.
 
Tushawahi kumsugua dogo mmoja o level na mabrash ya chooni kisa haogi way back seminary huko moshi
 
Back
Top Bottom