Nilimuacha akiwa mdogo sana na alikuwa anasoma shule ya msingi wakati ule Mimi nilikuwa naondoka mkoani kuja Dar kutafuta Maisha.
Miaka ilienda baadae akakua na akawa anaanza elimu ya sekondari , wakati huo Mimi nilikuwa nimeanza kupata vijihela kidogo nikaona ni bora dogo akasome private ili muda wake mwingi uwe ni shuleni
Ada kwa mwaka ni mil 1.6 amesoma miaka 4 mwaka huu alitakiwa amalize kidato cha 4 ,lakini napigiwa simu na mwalimu wake eti ana mimba tena ya miezi 4
Na ada nimelipa miaka yote minne ,ni zaidi ya milion 7 imetumika.Hapa nawaza naona bora ningeliacha mapema nisingehangaika nalo..
Mwalimu wake ananiambia tuma nauli mtoto arudi nyumbani, nimemwambia kama hawezi kutembea kwa miguu basi atembelee tumbo kurudi nyumbani kwao.