Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

Dada yangu japo cijapitia coment za wana mmu kutokana na muda hila langu ni ili usijaribu kuondoka komaa mtoto wa mwanamke mwenzangu ukiondoka tu ndo unampa nafasi ya kufanya machafu yake kaa nae chini kisha mmalize tofauti zenu kuna nyimbo moja ya ..shaa anasema siku hizi wanaume wachache akienda bafundi ,kazini lazima akuage .na unachoweza weza fanya wenzio wanaweza fanya sawa mama
 
pole sana dada ndoa ni ngumu sana matatizo ndani ya ndoa ni mengi la msingi kukaza moyo na kumfatilia mumeo ndoa zina matatizo sana dunia hii stay hapo ulipo fatilia ndoa yako mimi kama mwanaume nakushauri hivyo mausiano ni magumu sana pole sana dada angu
 
Du yaani ndugu yangu pole sana nadhani kuwa mwanamke jasiri mwenye tabia yake hawezi kuacha chukua uamuzi ulio sahihi pata washauri kama utaendelea kuumizwa kila siku au kuwa huru je unaweza kujimudu mwenyew kimaisha kama unaweza ni bora kuwa huru
 
poleee.mungu ujibu maombi km we n mpagani nenda kwa mganga.
 
Duu! Huyu mweshimiwa anabalaaa yani getini na anajua wife anaweza kutoka any time, je huko ofisini ambako wife hafiki kabisa si ndo atawamaliza ofisi nzima na jinsi visister do vya siku hizi vinavyopenda mtonyo.Pole mpendwa washirikishe wazazi wako kwa undani then think twice
 
Naomba tu nikuulize maswali kadhaa, labda nitakurudisha nyuma sana;

Mume wako kabla hamjaoana ulimchunguza vizuri tabia yake?

Ni kitu gani kilichokushawishi hadi ulikubali kufunga naye ndoa?
swali zuri muhimu kujua chanzo kwanza
 
Pole sana mpendwa wanaume ni shieeeda halafu asilimia kubwa wanafanana sijui kwanini
 
UUWWIIII dah no no no no Eeeh Mungu !!! inauma sanaaaaa.. bora haikuwa mimi, Mungu huwaumba watu tofauti jamani...hapa nilipo nimeishiwa nguvu nahisi hali ambayo ngumu kuelezea...Nahisi nisingeweza kuvumilia kama wewe ningeweza fanya baya..

Ushapima ??


Pole sana mpendwa, ila huyo mumeo ni MBWA sorry kama nimekukosea....Hachagui pakuingiza hilo lifimbo lake....
Nenda kwa kiongozi wa kanisa au Msikiti km ni muislam usikilize ushauri wao huwa nawatumai sana hawa wanabusara walizojaliwa...

Ukiondoka unafungulia wengine waingie ndani kwako tena awalaze kitandani mwako, usiondokeee akitaka aondoke yeyee

Huyo nduguye mtimue bila huruma isiyokuwa na chembe Shetani mkubwa huyo...

Ooohh God naomba umpe nguvu dada huyu...please!!








naamini kwa uwezo wa mungu mko wazima!

napenda kuwashukuru sana kwa michango yenu ambayo huwa mnatoa humu mm n mdau japo huwa siyo mchangiaji sana lakini siyo mara ya kwanza kuleta matatizo yangu hapa na mkanisaidia,

kama utaweza kupitia topic zangu za nyuma utanielewa vizuri ila leo nimekuja na lingine
nimeolewa nina mtoto mmoja ana miaka 5 nimeolewa miaka 7 iliyopita, kipindi chote cha maisha yangu ya ndoa nimepitia mambo magumu sana kutokana na tabia ya ufataki aliyonayo mume wangu lakini mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo,
, kama wiki 3 zilizopita kuna mtoto wa kike wa shangazi yake na mume wangu alikuja nyumbani kama kawaida huwa anakuja kutusalimia then anaondoka ila safari hii akawa amekaa sana nkamuuliza vpi unarudi au umekuja mjini kwa lengo gani akaniambia amechoka kukaa kijijini bora akae nyumbani anisaidie kazi za nyumbani nikamwambia sawa, tumekaa nikaona tuna shida ya mfanyakazi katika biashara yetu na yeye kwa elimu yake ndogo hiyo kazi anaiweza, basi nikamweleza mume nae akakubali tukaona kuliko akae nyumbani na kuna msichana wa kazi haina sababu, basi jana kaanza kazi na hiyo kazi anafanya hadi saa nne usiku then wanarudi na mjombaake ( yaani mume wangu)

jana usiku saa nne nikiwa ndo nataka nijilaze kitandani nilisikia gari la mume wang akiwa anarudi coz najua mlio wake, basi nikakaa kama dk 10 gari ipo nje nikajiuliza mbona hafungui geti aingize gar akili ikanijia labda anaongea na simu, nikalala zangu kama dk 20 mbele bado gari ipo silent nje, nikaamka nikatoka nje nikafungua geti taratibu nilishuhudia mume wangu akikisiana na huyo mtoto wa shangazi yake,niliishiwa nguvu nikamsogelea kuwaangalia vizuri bint akashtuka sana akataka kukimbia akashuka kwenye gari, nikamuuliza mnafanya nini hapa akaniambia wanafanya mahesabu nikamwambia mbona giza ebu leta hilo daftari la mahesabu mnalofanyia, akababaika akamuita yule bint akamwambia leta daftari akakimbia ndani chumbani kwake akajifungia akalala, nilistaajabu sana sikuamini nilichokina, mume wangu akaingiza gari ndani akaja chumbani jasho linamtoka sikumsemesha wala kumuuliza chochote nikalala,

leo asubuhi nilipoamka nikamwamsha yule binti nikamwambia ajiandae arudi kwao kajiandaa nikampa nauli nikamwambia asije tena nyumbani kwangu.
wapendwa kichwa kinaniuma na kinachoniuma siyo kuwakuta katika hali ile ila roho inaniuma mume wangu alipofikia ukiangalia yule binti ni ndugu yake wa damu kabisa ana miaka 17 tu, mume wangu ana miaka 47 mtu mzima, nimefikiria cha kufanya nakosa sina wa kumueleza naogopa mume wangu ni kiongozi nikisema kwa watu ni aibu natamani nifungashe niende kwanza nyumbani kwetu kwani naishi mbali na wazazi labda huyu mume atabadilika nikiondoka au nifanye nini msaada wenu jamani
 
Maswali hayo hayana tija kwa sasa sasa ni kumtafutia suluhu au faraja huyu dada, kama ni kuingia katika ndoa ashaingia....

Nyie kama hamjaingia ndio mnatakiwa kuchunguza sasa...Na pia hata mkichunguza wanaume wengi wa sasa mmmhhh (....) labda umtengeneze wa kwako....Sababu tunaona wanavyotongoza tongoza mitaani...




swali zuri muhimu kujua chanzo kwanza
 
kwakweli pole sana...naomba usiondoke nyumbani hata kidogo, inaweza ikawa tiketi kwake chamsingi mshirikishe ndugu yake yoyote mkubwa zaidi katika hili,,,kwasababu lazima hata ndugu watajiuliza imekuwaje huyo mtoto amerudishwa ghafla,,
binadamu wanabadilika sana nakuomba uongee na mumeo kwakiutu uzima na umueleze madhara ya anachokifanya na kwamba kuna magonjwa
 
nyumba kubwa, hebu pita huku kidogo umpe Davina ushauri maana wewe na mumeo mnaishi kimalaika malaika, please, pita pande hii. Anahitaji msaada wako wa siri ya mafanikio ya ndoa yako.
 
Pole sana na huyu bingwa wa mahesabu anaonekana ameanza muda mrefu hiyo kazi, peleka shauri kwa wasimamizi wa ndoa

Charger nimependa huo ushauri wako. BINGWA WA MAHESABU!!
 
Mkuu mimi naomba nimsaidie hapo unajua, kuna vipindi vitatu katika mahusiano na lazima ujue kusoma alama za nyakati, kuna uchumba apo burdaniiii, mkiingia kwenye ndoa mwanzoni mtaingia na ule upendo wa uchumba alafu kuna ndoa yenyewe hapa mtu anatoa kucha zote kazi kwako kusuka ama kunyoa. kwenye msafala wa mamba hata kenge wapo. Mama yangu aliniambia mwanangu maisha ya ndoa ni safari ndefu UKIMFUMANIA MUMEO KAMA UNAMPANGO WA KULEA WATOTO WAKO PAMOJA NAE USIPIGE KELELE, NA KAMA HUTOISHI NAE ITA ATA MDUNDIKO,
Naomba tu nikuulize maswali kadhaa, labda nitakurudisha nyuma sana;

Mume wako kabla hamjaoana ulimchunguza vizuri tabia yake?

Ni kitu gani kilichokushawishi hadi ulikubali kufunga naye ndoa?
 
Ondoka kwa amani ukapumzike nyumbani kwanza.
Hapo utakuwa umepata jibu uamue nini[/JUE]
Unajua iko hv kuna makabila mengine hasa mkoa wa Mara, mtoto wa shangazi na mtoto wa Mjomba wanaitana binamu. Kwa hiyo siyo tu kufanya mapenzi bali wanaruhusiwa kuoana. Kama Wahindi vile! Ss kama mwanamke unaposikia binamu wa kike wa mme wako kaja nyumbani kwa makabila hayo basi kama ulikuwa unamlinda mme wako inabidi uimarishe security up to the maximum kwani hao kulana ni kitu cha kawaida kabisa!
So, isije ikwa ni kwa msingi huo ndo maana mme mtu akamtafuna binamu yake!
 
Wewe mwana dada fanya maamuzi ya kihekima kwan kuondoka c solution fanya hivi...huyo c mmeo mwite muongee mweleze waziwazi ulichokiona na akufafanulie nini maana ya hichi kitendo...na je huyo kibinti ni ndugu yake au ni nikimchapuko chake?yaani hakiki umediscuss naye yote yanayokutia wasiwasi...bac asipokuwa muwazi chuku hayo maamuzi uliyoyataka...
 
True...............




Mkuu mimi naomba nimsaidie hapo unajua, kuna vipindi vitatu katika mahusiano na lazima ujue kusoma alama za nyakati, kuna uchumba apo burdaniiii, mkiingia kwenye ndoa mwanzoni mtaingia na ule upendo wa uchumba alafu kuna ndoa yenyewe hapa mtu anatoa kucha zote kazi kwako kusuka ama kunyoa. kwenye msafala wa mamba hata kenge wapo. Mama yangu aliniambia mwanangu maisha ya ndoa ni safari ndefu UKIMFUMANIA MUMEO KAMA UNAMPANGO WA KULEA WATOTO WAKO PAMOJA NAE USIPIGE KELELE, NA KAMA HUTOISHI NAE ITA ATA MDUNDIKO,
 
Utakuwa unajiumiza bure mama kwa kuwaza na wewe tafuta dogodogo awe anakuburudisha mradi uwe unatumia Ndomu
 
Back
Top Bottom