Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

Usimuulize chochote nyamaza kimya ili Roho imuume. Ukimuukiza atajitetea utashangaa.
 
Mshirikishe na Mungu,,, naamini ni ndoa takatifu, zungumza nae ktk maombi ya kweli kutoka kumoyo wako, maadam huyo mpwa keshaondoka tuliza moyo... Usijaribu kuondoka hapo nyumbani... utakuta mwenzio kahamia..... usikome kusali.... then tafuta muda muafaka zungumza nae.... usiite vikao kwanza.....ni yako lazima uyashinde...

Mkuu samahani ndoa takatifu ni ipi na isiyotakatifu ni ipi.
 
Naamini kwa uwezo wa Mungu mko wazima.

Napenda kuwashukuru sana kwa michango yenu ambayo huwa mnatoa humu mm ni mdau japo huwa siyo mchangiaji sana lakini siyo mara ya kwanza kuleta matatizo yangu hapa na mkanisaidia.

Kama utaweza kupitia topic zangu za nyuma utanielewa vizuri ila leo nimekuja na lingine.
Nimeolewa nina mtoto mmoja ana miaka 5 nimeolewa miaka 7 iliyopita, kipindi chote cha maisha yangu ya ndoa nimepitia mambo magumu sana kutokana na tabia ya ufataki aliyonayo mume wangu lakini mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo.

Kama wiki 3 zilizopita kuna mtoto wa kike wa shangazi yake na mume wangu alikuja nyumbani kama kawaida huwa anakuja kutusalimia then anaondoka ila safari hii akawa amekaa sana nkamuuliza vpi unarudi au umekuja mjini kwa lengo gani akaniambia amechoka kukaa kijijini bora akae nyumbani anisaidie kazi za nyumbani nikamwambia sawa.

Tumekaa nikaona tuna shida ya mfanyakazi katika biashara yetu na yeye kwa elimu yake ndogo hiyo kazi anaiweza, basi nikamweleza mume nae akakubali tukaona kuliko akae nyumbani na kuna msichana wa kazi haina sababu, basi jana kaanza kazi na hiyo kazi anafanya hadi saa nne usiku then wanarudi na mjombaake ( yaani mume wangu).

Jana usiku saa nne nikiwa ndo nataka nijilaze kitandani nilisikia gari la mume wangu akiwa anarudi coz najua mlio wake, basi nikakaa kama dk 10 gari ipo nje nikajiuliza mbona hafungui geti aingize gari akili ikanijia labda anaongea na simu, nikalala zangu kama dk 20 mbele bado gari ipo silent nje, nikaamka nikatoka nje nikafungua geti taratibu nilishuhudia mume wangu akikisiana na huyo mtoto wa shangazi yake.

Niliishiwa nguvu nikamsogelea kuwaangalia vizuri binti akashtuka sana akataka kukimbia akashuka kwenye gari, nikamuuliza mnafanya nini hapa akaniambia wanafanya mahesabu nikamwambia mbona giza ebu leta hilo daftari la mahesabu mnalofanyia, akababaika akamuita yule binti akamwambia leta daftari akakimbia ndani chumbani kwake akajifungia akalala, nilistaajabu sana sikuamini nilichokiona, mume wangu akaingiza gari ndani akaja chumbani jasho linamtoka sikumsemesha wala kumuuliza chochote nikalala.

Leo asubuhi nilipoamka nikamwamsha yule binti nikamwambia ajiandae arudi kwao kajiandaa nikampa nauli nikamwambia asije tena nyumbani kwangu.

Wapendwa kichwa kinaniuma na kinachoniuma siyo kuwakuta katika hali ile ila roho inaniuma mume wangu alipofikia ukiangalia yule binti ni ndugu yake wa damu kabisa ana miaka 17 tu, mume wangu ana miaka 47 mtu mzima.

Nimefikiria cha kufanya nakosa sina wa kumueleza naogopa mume wangu ni kiongozi nikisema kwa watu ni aibu natamani nifungashe niende kwanza nyumbani kwetu kwani naishi mbali na wazazi labda huyu mume atabadilika nikiondoka au nifanye nini msaada wenu jamani.
Pole kubwa. Kuna mambo makuu 2 uyafikirie.
1. Je huna HIV?
2. Watoto

Kuhusu no. 1: Kama wewe ni HIV negative basi usifanye naye mapenzi mpaka ajirekebishe
Kuhusu no. 2: Usiondoke maana huyo mtoto utampa tabu.

Sasa ufanyeje? Kuwa na Imani, amini Mumeo siyo fataki na amini kwa maombi ameacha.

Kukimbia haitasaidia labda kama ninyi ni waislamu hapo kazi ipo
 
Pole Davina. Inaumiza na kukwaza kwa kiwango kisichopimika. Usimpe nafasi huyo mumeo kwa wewe kuondoka. Kama ni fataki kama ulivyoeleza na ni dhahiri kwa matendo yake hayo, ukiondoka ndio unampa nafasi. Babatizana naye hadi kieleweke. Kwanza yeye kukataa kitu ambacho umeshuhudia kwa macho ni ubazazi na uzuzu wa kupindukia. Ongea naye ukiwa huna hasira kabisa na asipokiri kosa na kuomba msamaha lifikishe jambo hilo kwa wazee au washauri wa kiimani. Huo ni udhalilishaji mkubwa kabisa. Na mwambie akileta za kuleta utamjulisha Shangai yake. Tena huyo ni kesi ya udhalilishaji mana binti bado ni chini ya miaka 18.

Na mwisho nashauri ushike sana imani yako. Sali na kuomba sana. Fanya toba kwa ajli yake na familia nzima. Toa sadaka na zaka kwa maskini na Umwombe Mwenyezi Mungu ambadikishe. Tabia hiyo na umri huo nakuhakikishia hakuna kitakachombadilisha zaidi ya Mungu Mwenyezi na wewe. Nitaomba kwa ajili yenu kabla sijalala.

Pole sana.
 
Acha wivu, mbuzi mzima unataka ule peke yako Darisalama hii? yaani dume zima na pesa zake ulifungie ndani mwenyewe tu?? kwa uzuri upi ulionao...ukishuka wenzio wanapanda...kwahyo rudi kwenu ila ujue mzee ndo atafaidi sasa...wewe akianza kukufatilia vimarioo vyako je? au unadhan hajui, wanawake wabnafsi duh!
 
Pole sana my dear hakuna haja ya kuondoka cha kufanya washirikishe wazazi wa pande zote ikishindikana washirikishe na viongozi wenu wa dini pia, Mungu akusaidie katika majaribu unayopitia.
 
Naamini kwa uwezo wa Mungu mko wazima.

Napenda kuwashukuru sana kwa michango yenu ambayo huwa mnatoa humu mm ni mdau japo huwa siyo mchangiaji sana lakini siyo mara ya kwanza kuleta matatizo yangu hapa na mkanisaidia.

Kama utaweza kupitia topic zangu za nyuma utanielewa vizuri ila leo nimekuja na lingine.
Nimeolewa nina mtoto mmoja ana miaka 5 nimeolewa miaka 7 iliyopita, kipindi chote cha maisha yangu ya ndoa nimepitia mambo magumu sana kutokana na tabia ya ufataki aliyonayo mume wangu lakini mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo.

Kama wiki 3 zilizopita kuna mtoto wa kike wa shangazi yake na mume wangu alikuja nyumbani kama kawaida huwa anakuja kutusalimia then anaondoka ila safari hii akawa amekaa sana nkamuuliza vpi unarudi au umekuja mjini kwa lengo gani akaniambia amechoka kukaa kijijini bora akae nyumbani anisaidie kazi za nyumbani nikamwambia sawa.

Tumekaa nikaona tuna shida ya mfanyakazi katika biashara yetu na yeye kwa elimu yake ndogo hiyo kazi anaiweza, basi nikamweleza mume nae akakubali tukaona kuliko akae nyumbani na kuna msichana wa kazi haina sababu, basi jana kaanza kazi na hiyo kazi anafanya hadi saa nne usiku then wanarudi na mjombaake ( yaani mume wangu).

Jana usiku saa nne nikiwa ndo nataka nijilaze kitandani nilisikia gari la mume wangu akiwa anarudi coz najua mlio wake, basi nikakaa kama dk 10 gari ipo nje nikajiuliza mbona hafungui geti aingize gari akili ikanijia labda anaongea na simu, nikalala zangu kama dk 20 mbele bado gari ipo silent nje, nikaamka nikatoka nje nikafungua geti taratibu nilishuhudia mume wangu akikisiana na huyo mtoto wa shangazi yake.

Niliishiwa nguvu nikamsogelea kuwaangalia vizuri binti akashtuka sana akataka kukimbia akashuka kwenye gari, nikamuuliza mnafanya nini hapa akaniambia wanafanya mahesabu nikamwambia mbona giza ebu leta hilo daftari la mahesabu mnalofanyia, akababaika akamuita yule binti akamwambia leta daftari akakimbia ndani chumbani kwake akajifungia akalala, nilistaajabu sana sikuamini nilichokiona, mume wangu akaingiza gari ndani akaja chumbani jasho linamtoka sikumsemesha wala kumuuliza chochote nikalala.

Leo asubuhi nilipoamka nikamwamsha yule binti nikamwambia ajiandae arudi kwao kajiandaa nikampa nauli nikamwambia asije tena nyumbani kwangu.

Wapendwa kichwa kinaniuma na kinachoniuma siyo kuwakuta katika hali ile ila roho inaniuma mume wangu alipofikia ukiangalia yule binti ni ndugu yake wa damu kabisa ana miaka 17 tu, mume wangu ana miaka 47 mtu mzima.

Nimefikiria cha kufanya nakosa sina wa kumueleza naogopa mume wangu ni kiongozi nikisema kwa watu ni aibu natamani nifungashe niende kwanza nyumbani kwetu kwani naishi mbali na wazazi labda huyu mume atabadilika nikiondoka au nifanye nini msaada wenu jamani.
Dada binamu ni kinyama cha hamu, sio Haram kumuoa!!

Labda humkojozi vya kutosha huyo mumeo!! Jitahidi kumkojoza vya kutosha hatotoka nje ya ndoa
 
Msamiati huu unatumika zaidi kwa jinsia KE. Mwanaume kutokojozwa sio issue kabisa.

Anyway, Dada davina tabia za binadamu sometimes zinatokana na maradhi mtambuka ya akili.

Zungumza na mumeo amuone mtaalamu wa masuala ya Saikolojia. Huenda ikasaidia..

Pole!
 
Watu bana MNA MPA pole Leo wakati huu Uzi kaandika miaka mitano iliyopita na huyo mzee alikuwa na miaka 47 saivi ana miaka 53 na yule binti alikuwa na miaka 17 saivi 22
 
Vita haikimbiwi dada, komaa hapohapo mpaka kieleweke...
 
Watu bana MNA MPA pole Leo wakati huu Uzi kaandika miaka mitano iliyopita na huyo mzee alikuwa na miaka 47 saivi ana miaka 53 na yule binti alikuwa na miaka 17 saivi 22
Hahaha kwani pole zina expire date? Kuna ushauri pia ambao unaweza kumsaidia mtu mwingine yeyote atakayesoma hapa..
 
Watu bana MNA MPA pole Leo wakati huu Uzi kaandika miaka mitano iliyopita na huyo mzee alikuwa na miaka 47 saivi ana miaka 53 na yule binti alikuwa na miaka 17 saivi 22
C Ndo apo sasa lkn huenda hawajaangalia tarehe
 
Back
Top Bottom