Nilichokiona ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza leo

Nilichokiona ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza leo

Yaani hisia zangu juu yako sijawahi kukosea.., uko kama ninavyokuwazia... Strong woman.
Walaahi hadi nimejitoa potelea mbali Asha ani loge lakini nimesema, hahahahahahahahahahah
 
Yaani ndugu yangu, ungekuwepo ungejiuliza swali hili, "hivi ni ofisi ya serikali au nimefika bandarini kwa wabeba mizigo" mbaya zaidi alikuwa anatukana kwa sauti kubwa kiasi kwamba ofisi nyingi walikuwa wanamsikia, du! nilimhurumia yule kaka ambaye niliambiwa ni mfungwa wa kifungo cha nje.
Nadhani ungeenda physically kwa hao uliowaombà ktk uzi wachukue hatua kuripoti tukio hilo, badala ya kusema hauogopi kurogwa huku umejificha nyuma ya keyboard..Bahati mbaya tena uliowaomba kuchukua hatua ni sehemu ya menejiment hiyo hiyo inayomgwaya asha!
 
Hebu hiyo picha ya Asha mwenyewe iwekwe humu kusapoti uzi

ushauri wa bure
 
Nadhani ungeenda physically kwa hao uliowaombà ktk uzi wachukue hatua kuripoti tukio hilo, badala ya kusema hauogopi kurogwa huku umejificha nyuma ya keyboard..Bahati mbaya tena uliowaomba kuchukua hatua ni sehemu ya menejiment hiyo hiyo inayomgwaya asha!
Ushauri wako hautekelezeki, hahahahaha
 
Leo nimeona maajabu, kituko, jambo la kusikitisha ambalo sikutegemea kuliona katika ofisi ya Serikali Kuu, ofisi ambayo ndio "ikulu" yetu ya Mwanza, ofisi ambayo inamwakilisha Rais.

Nimefika ofisi hiyo leo muda wa saa 5.00 asubuhi kufuatilia mambo fulani yanayohusiana na ofisi yangu ninapopatia riziki ya kila siku.

Nilipofika kwenye korido la jengo la zamani nikasikia sauti kubwa, sauti kali, matusi ya nguoni yakitokea ofisi ya masjala ya wazi/bayana (open registry), nikashuhudia watu wengi wamesimama kwenye korido hilo wanasikiliza matusi yale ambayo ama kwa hakika hayakuwa hata na "skin tight" yalikuwa makavu yakiporomoshwa kutokea ofisi hiyo ya Masjala kwa sauti kubwa. Baadhi ya matusi hayo yalikuwa "MB.WA WEWE, MSEN.GE, YAANI WEWE NDIE UNANIFANYA NIITWE KWA MKUU WA MKOA," na matusi mengine mengi mengi machafu machafu.

Nikawapita watu waliokuwa wanasikilizia huo mziki wa matusi, nikaenda moja kwa moja hadi ofisi ya masjala kushuhudia kuna nini!!!

Oooooooooooooooops! nikakuta dada ambaye nimesikia wakimuita ASHA, ni Office Supervisor, anamtolea matusi hayo kaka ambaye ni mfungwa wa kifungo cha nje.

Mimi kama mtumishi wa umma, pia kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ya mwaka 2005, nilijisikia vibaya sana. Sikutarajia ofisi kubwa kama ile kukuta mtumishi anamtukana mwenzie matusi ya nguoni kwa sauti kubwa kama vile amapandisha mashetani!

Nikawauliza baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo, huyu Asha anaumwa au ni tabia yake? wakasema Asha ndivyo alivyo na uongozi unajua tabia zake, lakini WANAOGOPA KULOGWA!

Sasa mimi siogopi kulogwa na huyo Asha wenu, nawaomba viongozi wa mkoa, kaka Mongela, Mtweve, Rubanzibwa fuatilieni utendaji wa huyo Asha hapo Masijala sio kwa matusi hayo!

Mwisho wanaJF msiponiona hapa JF kwa muda mrefu basi mjue labda Asha kaniloga nimekufa.

Nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko
hafi mtu, pole sana kwa uliyoyasikia na kuyaona..
 
Hebu hiyo picha ya Asha mwenyewe iwekwe humu kusapoti uzi

ushauri wa bure
Nilivyoshikwa na butwaa hata sikukumbuka kumrekodi na hali alikuwa anaongea kwa sauti kubwa saaanaa
 
Back
Top Bottom