kaburu mdogo
JF-Expert Member
- Dec 19, 2011
- 567
- 400
binafsi napenda sana kuwaheshimu hawa wasaidizi wa ndani maana ndo wanaobeba majukumu yote ya familia kuanzia asubuhi hadi usiku,kiusalama na kila kitu ndani na nje ya familia.nilichokiona leo hapa nyumbani kwetu kimeniskiktisha sana na sikujua kama mzazi wangu anaweza kufanya hivyo;miezi miwili iliyopita alichua msichana kutoka mkoa wa arusha (meru) na kuja nae huku kwa ajili ya kumsaidi kazi za ndani maana wa awali aliondoka na hakurudi,sababu sizijui.baada ya wiki kadhaa nikanza kusikia msichana wetu anaanza kulalamika kuwa bora angerudi na mwisho wa mwezi huu angemwambia bosi wake kuwa anataka likizo fupi maana nyumbani kwao kuna tatizo na ameitwa ghafla na wazee wake!wiki moja baadae mama akapata hizo taarifa na kuniuliza kama nimemsikia akisema nami nikamjibu kuwa binanfsi ahajanambia ila naskia akiwaambia wenzake juu ya swala hilo.wiki iliyopita mama alitafuta msichana kisiri na kumficha kwa jirani na kuanza kumtahutia mdada wa watu sababu lukuki ikiwemo hujui usafi,hujui kupika na mengine mengi ,mdada wa watu akawa anavumilia na mwisho alinambia anahisi mama amemchoka na anamtafutia sababu ili amfukuze.
jana asubuhi bi mkubwa anampa msichana taarifa kuwa anatakiwa kujiandaa aende kwao leo na kunituma nikamkatie tiketi ya basi,jana hiyo hiyo nilimkatia ticket,huku nyuma kumbe bi mkubwa alikua anafuatilia hatua kwa ahatua kila kitua alichokuwa anakifanya huyo mdada kwenye maandalizi yake ya kufungusha mizigo,jioni ndo mzozo ulipokua mkali sana maana msichana wa watu alikua amefungasha vitu vyake vizuri kwa ajili ya safari lahuala bi mkubwa anaanza kuulizia kitu kimoja baada ya kingine alichokua mempa na kuanza kumnyang'anya.nilikereka na iliniuma sana mdada wa watu anabaki kutazamatu asijue la kufanya na alichofanay ni kwenda kununua mfuko wa kirba kwa mangi muuza duka na kufungasha upya mizigo yake,inauma kwa kwel,wazai wetu wana roho nzuri pindi wawa chukuapo wadada ila pindi wawachukiapo ni kiama kikubwa kwao.tujirekebishe maana hizi ni laana kwetu na kwa wajukuu zetu kutoka kwa hawa wadada jamani