Nilichojifunza ndani ya mwaka mmoja bila ajira

Ukiwafuga kisasa inakula kwako, yaani wafuge pure kienyeji wajitafutie wenyewe wewe usiingia gharama kabisa kwao
yaa.. wa kienyeji mkuu. Ila wafuge kiuzalishaji. Usifuge kienyeji sana.

Taratibu tu usiwe na haraka sana jipe hata miaka 2-5

Kama imani yako inaruhusu fuga wale jamaa[emoji3][emoji3]

Epuka mazao ambayo wengi wanayakimbilia kimkumbo kama hayo matikiti watu huwa wanayashobokea lkn mimi huwa nayapita hivi.
Yaani mimi nikiona zao fulani vijana wanalizungumzia sana me huwa sihangaiki nalo maana watz nawajua.
 
Kuku Aina gani una mshauri kufuga?
AFUGE KUKU WA KIENYEJI

Hamna kuku aina nyingine hapo

Anaweza akaamua kununua vifaranga vya majogooo

zile mbegu nzuri,akawafuga kwa lengo la kuja kuwauza

atawanunua wadogo ila akija kuuza JOgoo mkubwa atamuuza hata 30,000

sio afuge kutegemea kuku atage alalie atotoe NOOOO

kuku wa kufuga ni wa Kienyeji na si wengine
 
Na ukitaka ufurahie kuku wako wa kienyeji NUNUA VIFARANGA

then pambana vifaranga visife,jitahidi kila namna vifaranga vyko visife

aseee wakikua wakubwa Utauza bei nzuri nzuri sana

ila kufuga wakienyeji utegemee mtetea atage alalie atotoe ohooooooo Utachelewaaa
 
Jaribu kilimo cha nyanya kaka, huwez kosa soko, ila target iwe kipindi cha nyanya kuwa juu.. Usilime wakat wa mavuno ya weng.. Lima kipind ambacho syo msimu.. Kwa kuwa una pampu ya umwagliaji tayari. Usikate tamaa
Nyanya ninyanyue, Nyanya ninyanyase
 
Ukiwafuga kisasa inakula kwako, yaani wafuge pure kienyeji wajitafutie wenyewe wewe usiingia gharama kabisa kwao
Mkuu kuwafuga pure kienyeji atachelewa. Nilichomaanisha afuge kuku. Wakitaga akatotoleshe au wakitotoa awanyang'anye baada ya mwezi au week kadhaa tu vifaranga awatunze mwenyewe. Halafu wakifikisha miezi miwili au mitatu awaachie wajitafutie.
Akifuga pure kienyeji aisee atakwama.
 
Pole sana Mkuu naona umepata ushauri wa kutosha ila ningependa kukujuza fanya ufugaji wa samaki[kambale] maana hakuna gharama kubwa na wanakua vyema maana una eneo kubwa sana nina amini utafika mbali sana asante.
Nimekuelewa ndugu ntafanya hivyo
 
Tarehe kama ya leo nimetimiza mwaka mmoja tokea ajira yangu ya mkataba kwenye kampuni binafsi imalizike. Sikuongezewa mkataba kwa sababu ya kila mara kudai stahiki zangu. Sikulipwa hata mia, mwajili aliniambia ''nenda popote, sikulipi hata mia". Sikutaka kwenda mahakamani sababu sikuwa na pesa ya kuweka wakili na jamaa anapenda sana ukienda mahakamani manake anahonga ili kesi ipigwe tarehe mpaka ujute. Nikazunguka sana ofisi za serikali (Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa), jamaa ana mkono mrefu sana, sikuambulia chochote. Nikaandika barua wizara zinazohusika, hakuna aliyejibu.

Nikapiga moyo konde, uzuri nina shamba la hekari kumi na nina bwawa la maji ya kutosha. Nikakopeshwa milioni 2 na Mzazi wangu, nikachukua vijana wawili nikazama shambani vijijini huko, tukaingia kazini. Kilichonisaidia vilevile nilikuwa nimeshajenga kajumba huko shambani na nilikuwa na water pump. Nikajiingiza kwenye kilimo cha matikiti manake nilisikia kinalipa sana. Nikalima hekari moja na nusu nikiwa na vijana wangu. Miezi miwili na nusu mavuno yakawa tayari. Kwakuwa ilikuwa mara ya kwanza nilitumia gharama kubwa kuendesha mradi na ingawa mavuno hayakuwa haba niliambulia faida ya laki tatu tu sababu nilikumbana na mafuriko. Nikajipa moyo kwamba nimejifunza kitu.

Mwezi wa saba mwaka huu, nikakopa milioni moja nikaongezea na hiyo pesa ya mwanzo nikaingia tena shamabni. Sijui nilikosea wapi lakini mavuno hayakuwa mazuri sana. Akaja mnununzi shambani yuko tayari kuyanunua kwa 2.5M nikakataa. Nikaongea na dalali mmoja yuko Dar akadai kule tikiti hakuna na yana bei kubwa, tukaelewana nikayavuna tukapata gari tukayapeleka. Tumefika Vetenary (Buguruni), tukakuta zaidi ya gari kumi zimeshusha mzigo na ni quality mara nne ya niliyobeba. Nikauza kwa hasara na baada ya kutoa baadhi ya gharama kama ushuru na usafiri nikaambulia laki tano tu (hasara ya milioni 2). Dalali alinionea huruma ilibidi anipe hela ya usafiri na kuahidi kuninunulia mbegu na madawa ili tulime upya. Nikarudi nyumbani nimechoka zaidi ya maelezo. Hapa nilipo nadaiwa milioni tatu na mtaji wangu umekata. Sijakata tamaa na wala sina mpango wa kukata tamaa, nipo natafuta capital niingie mzigoni mwezi wa 12. Kwa sasa nimelima mahindi ingawa mvua nazo zimekata.

NILICHOJIFUNZA:

- ukiwa unafanya kazi sekta binafsi jiandae kisaikolojia kwani unaweza kuondoka muda wowote, jifunze kuwekeza wakati uko kazini

- wakati ukiwa kazini jifunze pia na ujasiria mali, ni ngumu kujifunza kama huna kazi. Kila utakachosikia kinalipa utakikimbilia bila information za kutosha na ni rahisi sana kuanguka

- Kama huna uwezo wa kufanya adjustment ya matumizi kutokana na kipato chako USIACHE KAZI NA USIFANYE BIASHARA. Inanibidi nilale chini, kula mara moja au mbili na kula aina ya vyakula ambavyo sijawahi kufikiria.

- Kilimo kina changamoto kubwa sana huwezi kuzijua mpaka ufanye.
- Taarifa sahihi ndio kila kitu, usifanye kitu kwa mkumbo
- Usikate tamaa, kila kitu kingekuwa chepesi kila mtu angekuwa tajiri. Pigana sana na usisahau kumtanguliza Mungu kwenye shughuli zako.

NB: Kama unaweza kunipa ushauri wa namna ya kufanya kilimo bora, namna ya kupata mtaji au kufanya partnership, unakaribishwa.
Pole sana mkuu, here is my advise;
  1. Inaonekana kama kijana nimpambanaji, ila unataka zaidi ya stahiki yako
  2. Usibishane na anayekuzidi kimamlaka , kunyenyekea unaweza kufaidika zaidi
  3. Usifanye biashara kwa hasira na mapato yake ni vigumu kutajirika kwa muda mfupi.
  4. Wengi tumepitia uliyopitia, mimi ilinichukua miaka mitano au sita kwanza kuona matunda ya kazi yangu
  5. Usikate tamaa, mwaka mmoja ni muda mfupi kuna naTokyo.
  6. Jifunze na matatizo inayopotea ili kuboresha kuelewa wako.
Zaidi ya hapo nakupa hongera na pole kwa ingalau karibu bia mbadala kujitegemea.

Sasa jiweke katika position wake kijana wawili waliokussidia wangeamua kukushitaki kwa kutokuwalipa vizuri.

Mvumilivu hula mbivu.
 
Mkuu kuwafuga pure kienyeji atachelewa. Nilichomaanisha afuge kuku. Wakitaga akatotoleshe au wakitotoa awanyang'anye baada ya mwezi au week kadhaa tu vifaranga awatunze mwenyewe. Halafu wakifikisha miezi miwili au mitatu awaachie wajitafutie.
Akifuga pure kienyeji aisee atakwama.
Nitafanya hivyo ndugu....najaribu nipate mafao yangu NSSF ili nipate capital ila ndo hivyo nashindwa nimkimbilie nani anisaidie
 
Pole sana mkuu, here is my advise;
  1. Inaonekana kama kijana nimpambanaji, ila unataka zaidi ya stahiki yako
  2. Usibishane na anayekuzidi kimamlaka , kunyenyekea unaweza kufaidika zaidi
  3. Usifanye biashara kwa hasira na mapato yake ni vigumu kutajirika kwa muda mfupi.
  4. Wengi tumepitia uliyopitia, mimi ilinichukua miaka mitano au sita kwanza kuona matunda ya kazi yangu
  5. Usikate tamaa, mwaka mmoja ni muda mfupi kuna naTokyo.
  6. Jifunze na matatizo inayopotea ili kuboresha kuelewa wako.
Zaidi ya hapo nakupa hongera na pole kwa ingalau karibu bia mbadala kujitegemea.

Sasa jiweke katika position wake kijana wawili waliokussidia wangeamua kukushitaki kwa kutokuwalipa vizuri.

Mvumilivu hula mbivu.
Nashukuru sana ndg yangu...nimejifunza mengi sana..ila kiukweli nimenyenyekea sana kwa mwajili wangu wa zamani lakini imeshindikana kulipwa. Jamaa ni mkorofi sana na huwa halipi mpaka msumbuane
 
Pole sana mkuu ndio maisha haya changamoto hazikosekani hustle kama hizi ni lazima uzipitie ili uje kua mfano hai kwa watu wengine wanaokuzunguka pia ili uje kuziheshimu pesa zako siku ukifikia mafanikio

Sijajua upo wapi ila kama walivyokushauri wengine huko juu jitahidi ufuge, vitu kama kuku, nguruwe vinalipa sana (japo inategemeana na location na market pia) lakini faida yake vinakupa option nyingi, kama kuku unaweza kuuza sokoni, ukachinja ukauza nyama kwa kui roast au supu,, wakati nipo Morogoro niliona jamaa fulani wanapiga hio michakato na they make good money.. Msingi tu kupambana bila kuchoka always mwanzo hua mgumu
Ahsante sana ndugu yangu...ushauri mzuri ntaufanyia kazi
 
Nashukuru sana ndg yangu...nimejifunza mengi sana..ila kiukweli nimenyenyekea sana kwa mwajili wangu wa zamani lakini imeshindikana kulipwa. Jamaa ni mkorofi sana na huwa halipi mpaka msumbuane
Mkuu kama ushabiki Mungu, mengine muachie atashughulika nayo.
 
Mifuko ya jamii bado kuna siasa kuhusu hili suala la fao la kujitoa mimi mwenyew ni muhanga wa hili mwezi wa sita sasa bado nafuatilia haya mafao baada ya kibarua changu kuota nyasi sasa kila nikienda hela zipo ila wanadai hawatoi hela na ipo kama 7m ambay naamini itanisukuma mtaani kuendeleza nachokifanya sasa hivi labda kama mkuu una taarifa tofaut utusaidie
Meneja alinambia wao kama taasisi hawawezi kumpeleka mtu mahakamani kisa hajalipa michango...wanafanya negotiations tu. So akigoma kulipa inabidi utulie wambembeleze. Natamani kama kuna mtu ana mawasiliano ya hawa wakubwa ningeongea nao wanisaidie
 
Ilikuwaje ukafukuzwa kazi kiasi kwamba kila ulipoomba bosi aliamua kutia nuksi ya mkono wake?? It means ana kisasi naww sana
 
Mkuu kuwafuga pure kienyeji atachelewa. Nilichomaanisha afuge kuku. Wakitaga akatotoleshe au wakitotoa awanyang'anye baada ya mwezi au week kadhaa tu vifaranga awatunze mwenyewe. Halafu wakifikisha miezi miwili au mitatu awaachie wajitafutie.
Akifuga pure kienyeji aisee atakwama.
Kuku wa kienyeji unafuga ili wakusaidie kulipa bills Na kula tu Ila si wakutoe kibiashara. Soko linalotrend mtaan ni la bloiler kwa sababu bei ipo chini mtu anaweza chukua kuku 500 kwa mkupuo kwa ajili ya shughuli kwa bei ya elf 8. Sasa kuku wa kienyeji elf 20.kupata Mteja wa kuku 500 wa kienyeji kwa wakati mmoja shughuli
 
Kimoja ulichosahau cha kujifunza mkuu, USIJIFANYE UNAJUA SANA KUDAI STAHIKI ZAKO UKIWA KAZINI. Mara zote pima upepo, kama huna kingine cha kufanya ridhika na ulipo, usiwe mstari wa mbele sana kudai stahiki kwa kudhani ni ukidume. By the way ukielewa duniani hakuna haki isipokuwa mbinguni tu utakuwa na kiasi katika kudai stahiki si kazini tu hata kwenye ndoa hata mtaani!
Kwa kweli hakuna haki, huko mbinguni kunatajwa kwa kuwa nako hakuna uthibitisho.
 
MPAKA BANGI UTAJIFUNZA WE SUBIRIA TU
Tarehe kama ya leo nimetimiza mwaka mmoja tokea ajira yangu ya mkataba kwenye kampuni binafsi imalizike. Sikuongezewa mkataba kwa sababu ya kila mara kudai stahiki zangu. Sikulipwa hata mia, mwajili aliniambia ''nenda popote, sikulipi hata mia". Sikutaka kwenda mahakamani sababu sikuwa na pesa ya kuweka wakili na jamaa anapenda sana ukienda mahakamani manake anahonga ili kesi ipigwe tarehe mpaka ujute. Nikazunguka sana ofisi za serikali (Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa), jamaa ana mkono mrefu sana, sikuambulia chochote. Nikaandika barua wizara zinazohusika, hakuna aliyejibu.

Nikapiga moyo konde, uzuri nina shamba la hekari kumi na nina bwawa la maji ya kutosha. Nikakopeshwa milioni 2 na Mzazi wangu, nikachukua vijana wawili nikazama shambani vijijini huko, tukaingia kazini. Kilichonisaidia vilevile nilikuwa nimeshajenga kajumba huko shambani na nilikuwa na water pump. Nikajiingiza kwenye kilimo cha matikiti manake nilisikia kinalipa sana. Nikalima hekari moja na nusu nikiwa na vijana wangu. Miezi miwili na nusu mavuno yakawa tayari. Kwakuwa ilikuwa mara ya kwanza nilitumia gharama kubwa kuendesha mradi na ingawa mavuno hayakuwa haba niliambulia faida ya laki tatu tu sababu nilikumbana na mafuriko. Nikajipa moyo kwamba nimejifunza kitu.

Mwezi wa saba mwaka huu, nikakopa milioni moja nikaongezea na hiyo pesa ya mwanzo nikaingia tena shamabni. Sijui nilikosea wapi lakini mavuno hayakuwa mazuri sana. Akaja mnununzi shambani yuko tayari kuyanunua kwa 2.5M nikakataa. Nikaongea na dalali mmoja yuko Dar akadai kule tikiti hakuna na yana bei kubwa, tukaelewana nikayavuna tukapata gari tukayapeleka. Tumefika Vetenary (Buguruni), tukakuta zaidi ya gari kumi zimeshusha mzigo na ni quality mara nne ya niliyobeba. Nikauza kwa hasara na baada ya kutoa baadhi ya gharama kama ushuru na usafiri nikaambulia laki tano tu (hasara ya milioni 2). Dalali alinionea huruma ilibidi anipe hela ya usafiri na kuahidi kuninunulia mbegu na madawa ili tulime upya. Nikarudi nyumbani nimechoka zaidi ya maelezo. Hapa nilipo nadaiwa milioni tatu na mtaji wangu umekata. Sijakata tamaa na wala sina mpango wa kukata tamaa, nipo natafuta capital niingie mzigoni mwezi wa 12. Kwa sasa nimelima mahindi ingawa mvua nazo zimekata.

NILICHOJIFUNZA:

- ukiwa unafanya kazi sekta binafsi jiandae kisaikolojia kwani unaweza kuondoka muda wowote, jifunze kuwekeza wakati uko kazini

- wakati ukiwa kazini jifunze pia na ujasiria mali, ni ngumu kujifunza kama huna kazi. Kila utakachosikia kinalipa utakikimbilia bila information za kutosha na ni rahisi sana kuanguka

- Kama huna uwezo wa kufanya adjustment ya matumizi kutokana na kipato chako USIACHE KAZI NA USIFANYE BIASHARA. Inanibidi nilale chini, kula mara moja au mbili na kula aina ya vyakula ambavyo sijawahi kufikiria.

- Kilimo kina changamoto kubwa sana huwezi kuzijua mpaka ufanye.
- Taarifa sahihi ndio kila kitu, usifanye kitu kwa mkumbo
- Usikate tamaa, kila kitu kingekuwa chepesi kila mtu angekuwa tajiri. Pigana sana na usisahau kumtanguliza Mungu kwenye shughuli zako.

NB: Kama unaweza kunipa ushauri wa namna ya kufanya kilimo bora, namna ya kupata mtaji au kufanya partnership, unakaribishwa.
 
Aisee mimi heri nifukuzwe tu.Siwezi kusema nyeupe kwenye nyeusi.Never.Huku ni kuufinyusha ubongo,kuona kwamba hapo ni alfa na omega wakati dunia ni pana sana hii

Pole lakini hongera sana!
Kwa kifupi huko pekeyako ktk dilemma ya kukosa soko la mazao yako.
Sababu kubwa ni kushuka kwa purchasing power miongoni mwawapa wananchi. Hawana kipato kabisa.
Shughuli zote za uchumi lazima ziendane na soko la ndani na nje.
Hayo matikiti na matunda mengine mtu hawezi kuwapa watoto kama hata chakula milo mitatu hawezi kuwapa!
Na kwakuwa hadi sasa mwajiri mkuu ni Serikali, bila kuboresha mishahara ya civil servants wanunuzi wa bidhaa za sokoni watabaki wengi wasio na ajira.
Wenye mitaji mikubwa bila soko la nje nao watakufa au watakimbia.
Tutaendelea kula makombo na kuvaa mitumba tusipojithamini na kujikomboa.
 
Mi nakwambia komaa lakini inaelekea un attitude issue ,hata ufanye nini uwezi kufanikiwa.Kwenye ulimwengu wa Roho(mshana anajua) wewe unamakwazo tayari na chochote utakachofanya uwezi kutoboa.Be positive kwanza kwakazi ya kwanza ,sahau yaliyopita,jipange ,usifanye unachofanya kwa hasira ila kwa malengo na bidi.Ila ushauri wako bomba sana.
Natamani niufahamu zaid huo ulimwengu wa kiroho...yes sometimes nakuwa na hasira but what do I do??
 
Back
Top Bottom