Nilichojifunza ndani ya mwaka mmoja bila ajira

mugomangara

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
238
622
Tarehe kama ya leo nimetimiza mwaka mmoja tokea ajira yangu ya mkataba kwenye kampuni binafsi imalizike. Sikuongezewa mkataba kwa sababu ya kila mara kudai stahiki zangu. Sikulipwa hata mia, mwajili aliniambia ''nenda popote, sikulipi hata mia". Sikutaka kwenda mahakamani sababu sikuwa na pesa ya kuweka wakili na jamaa anapenda sana ukienda mahakamani manake anahonga ili kesi ipigwe tarehe mpaka ujute. Nikazunguka sana ofisi za serikali (Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa), jamaa ana mkono mrefu sana, sikuambulia chochote. Nikaandika barua wizara zinazohusika, hakuna aliyejibu.

Nikapiga moyo konde, uzuri nina shamba la hekari kumi na nina bwawa la maji ya kutosha. Nikakopeshwa milioni 2 na Mzazi wangu, nikachukua vijana wawili nikazama shambani vijijini huko, tukaingia kazini. Kilichonisaidia vilevile nilikuwa nimeshajenga kajumba huko shambani na nilikuwa na water pump. Nikajiingiza kwenye kilimo cha matikiti manake nilisikia kinalipa sana. Nikalima hekari moja na nusu nikiwa na vijana wangu. Miezi miwili na nusu mavuno yakawa tayari. Kwakuwa ilikuwa mara ya kwanza nilitumia gharama kubwa kuendesha mradi na ingawa mavuno hayakuwa haba niliambulia faida ya laki tatu tu sababu nilikumbana na mafuriko. Nikajipa moyo kwamba nimejifunza kitu.

Mwezi wa saba mwaka huu, nikakopa milioni moja nikaongezea na hiyo pesa ya mwanzo nikaingia tena shamabni. Sijui nilikosea wapi lakini mavuno hayakuwa mazuri sana. Akaja mnununzi shambani yuko tayari kuyanunua kwa 2.5M nikakataa. Nikaongea na dalali mmoja yuko Dar akadai kule tikiti hakuna na yana bei kubwa, tukaelewana nikayavuna tukapata gari tukayapeleka. Tumefika Vetenary (Buguruni), tukakuta zaidi ya gari kumi zimeshusha mzigo na ni quality mara nne ya niliyobeba. Nikauza kwa hasara na baada ya kutoa baadhi ya gharama kama ushuru na usafiri nikaambulia laki tano tu (hasara ya milioni 2). Dalali alinionea huruma ilibidi anipe hela ya usafiri na kuahidi kuninunulia mbegu na madawa ili tulime upya. Nikarudi nyumbani nimechoka zaidi ya maelezo. Hapa nilipo nadaiwa milioni tatu na mtaji wangu umekata. Sijakata tamaa na wala sina mpango wa kukata tamaa, nipo natafuta capital niingie mzigoni mwezi wa 12. Kwa sasa nimelima mahindi ingawa mvua nazo zimekata.

NILICHOJIFUNZA:

- ukiwa unafanya kazi sekta binafsi jiandae kisaikolojia kwani unaweza kuondoka muda wowote, jifunze kuwekeza wakati uko kazini

- wakati ukiwa kazini jifunze pia na ujasiria mali, ni ngumu kujifunza kama huna kazi. Kila utakachosikia kinalipa utakikimbilia bila information za kutosha na ni rahisi sana kuanguka

- Kama huna uwezo wa kufanya adjustment ya matumizi kutokana na kipato chako USIACHE KAZI NA USIFANYE BIASHARA. Inanibidi nilale chini, kula mara moja au mbili na kula aina ya vyakula ambavyo sijawahi kufikiria.

- Kilimo kina changamoto kubwa sana huwezi kuzijua mpaka ufanye.
- Taarifa sahihi ndio kila kitu, usifanye kitu kwa mkumbo
- Usikate tamaa, kila kitu kingekuwa chepesi kila mtu angekuwa tajiri. Pigana sana na usisahau kumtanguliza Mungu kwenye shughuli zako.

NB: Kama unaweza kunipa ushauri wa namna ya kufanya kilimo bora, namna ya kupata mtaji au kufanya partnership, unakaribishwa.
 
Kimoja ulichosahau cha kujifunza mkuu, USIJIFANYE UNAJUA SANA KUDAI STAHIKI ZAKO UKIWA KAZINI. Mara zote pima upepo, kama huna kingine cha kufanya ridhika na ulipo, usiwe mstari wa mbele sana kudai stahiki kwa kudhani ni ukidume. By the way ukielewa duniani hakuna haki isipokuwa mbinguni tu utakuwa na kiasi katika kudai stahiki si kazini tu hata kwenye ndoa hata mtaani!
 
Nina miaka miwili sina kazi, nilifanyiwa figisu kama zako - nimepanga Tabata 250K per month, watoto wa2, mmoja anasoma std 6 Atlas na mwingine std 2 Christ the King. Nitakomaa mpaka tone la mwisho hapa mjini.

NB: Figisu za mjini naziweza vizuri tu-wala sio muoga wa maisha.
 
Hilo neno mkuu, ila muda mwingine uonevu unazidi.
Kimoja ulichosahau cha kujifunza mkuu, USIJIFANYE UNAJUA SANA KUDAI STAHIKI ZAKO UKIWA KAZINI. Mara zote pima upepo, kama huna kingine cha kufanya ridhika na ulipo, usiwe mstari wa mbele sana kudai stahiki kwa kudhani ni ukidume. By the way ukielewa duniani hakuna haki isipokuwa mbinguni tu utakuwa na kiasi katika kudai stahiki si kazini tu hata kwenye ndoa hata mtaani!
 
Ahsante mkuu....nipo Mkoani Geita Wilaya ya Bukombe ila pia nina shamba Kahama Shinyanga yalipo makazi yangu ya kudumu
Sasa safi, subiri wan JF waje hasa wenye uzoefu wa maeneo ya Kahama na Shinyanga. Bye the way, hebu nisaidie mimi kwa kuniunganisha na wachimba dhahabu, kama unawafahamu. Nina interest na eneo hilo.Anyway dengu vipi haiwezi kukutoa huko Shinyanga kwani nafahamu inastawi vizuri SHY na wanunuzi wapo wengi huku Dar.
 
Back
Top Bottom