Mkaruka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 19,932
- 34,918
1. Duniani hakuna haki saaaana, tumia akili.Kimoja ulichosahau cha kujifunza mkuu, USIJIFANYE UNAJUA SANA KUDAI STAHIKI ZAKO UKIWA KAZINI. Mara zote pima upepo, kama huna kingine cha kufanya ridhika na ulipo, usiwe mstari wa mbele sana kudai stahiki kwa kudhani ni ukidume. By the way ukielewa duniani hakuna haki isipokuwa mbinguni tu utakuwa na kiasi katika kudai stahiki si kazini tu hata kwenye ndoa hata mtaani!
2. Hata kama unaonewa kazini, kama haikuathiri vumilia tu huku ukijipanga kwa mambo yako binafsi
3. Siku zote ingia kwenye ajira ( with an exit strategy ) huku ukikubaliana na ukweli kuwa kampuni siyo yako na unaweza kuwa terminated anytime
4. Kumbuka mahusiano yako na kampuni yanajengwa na mkataba wako tu, na wewe ni cheap labor ( Ukitimuliwa saa 4 asubuhi, saa 4.02 kuna watu 500 wanataka kazi hiyo hiyo hata kwa ujira pungufu.
5. Maisha ya kujiajiri yanaleta furaha na amani isiyo na kifani, kwa kuwa yanakupa uhuru kamili