Nilichojifunza ndani ya mwaka mmoja bila ajira

Nilichojifunza ndani ya mwaka mmoja bila ajira

Uko sawa kabisa mfano kuku wa kisasa ni so delicate.Ng'ombe wa kisasa nao wanahitaji daktari wa kuwacheki hata kama hawaumwi.Wakati mwingine wanagoma kutoa maziwa kama hawajala au kunywa maji mengi
Ufugaji kidogo kuna afadhali ingawa inabidi uwe mvumilivu kuiona faida. Pia mifugo inabidi uwe karibu nayo sana yaani kama unalea mtoto mchanga.
 
Tena huyu ana chanzo cha maji. Apande mipapai pia.

Afuge bata. Hawana maradhi mengi pia wana soko.
Mbuzi afuge atafute ile inayozaa mapacha.

Alime mboga mboga hoho,bilinganya, bamia(hizi bamia utanikumbuka) na mipapai. Mahind ya kumwagilia etc.
Mbuzi na bila kusahau na Kondoo pia
 
Nilishasahau kazi aiseee! Ila Mungu ni wa ajabu sana! Maisha yanaendelea na account inasoma vizuri tu though nimeuza baadhi ya assets
 
Tarehe kama ya leo nimetimiza mwaka mmoja tokea ajira yangu ya mkataba kwenye kampuni binafsi imalizike. Sikuongezewa mkataba kwa sababu ya kila mara kudai stahiki zangu. Sikulipwa hata mia, mwajili aliniambia ''nenda popote, sikulipi hata mia". Sikutaka kwenda mahakamani sababu sikuwa na pesa ya kuweka wakili na jamaa anapenda sana ukienda mahakamani manake anahonga ili kesi ipigwe tarehe mpaka ujute. Nikazunguka sana ofisi za serikali (Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa), jamaa ana mkono mrefu sana, sikuambulia chochote. Nikaandika barua wizara zinazohusika, hakuna aliyejibu.

Nikapiga moyo konde, uzuri nina shamba la hekari kumi na nina bwawa la maji ya kutosha. Nikakopeshwa milioni 2 na Mzazi wangu, nikachukua vijana wawili nikazama shambani vijijini huko, tukaingia kazini. Kilichonisaidia vilevile nilikuwa nimeshajenga kajumba huko shambani na nilikuwa na water pump. Nikajiingiza kwenye kilimo cha matikiti manake nilisikia kinalipa sana. Nikalima hekari moja na nusu nikiwa na vijana wangu. Miezi miwili na nusu mavuno yakawa tayari. Kwakuwa ilikuwa mara ya kwanza nilitumia gharama kubwa kuendesha mradi na ingawa mavuno hayakuwa haba niliambulia faida ya laki tatu tu sababu nilikumbana na mafuriko. Nikajipa moyo kwamba nimejifunza kitu.

Mwezi wa saba mwaka huu, nikakopa milioni moja nikaongezea na hiyo pesa ya mwanzo nikaingia tena shamabni. Sijui nilikosea wapi lakini mavuno hayakuwa mazuri sana. Akaja mnununzi shambani yuko tayari kuyanunua kwa 2.5M nikakataa. Nikaongea na dalali mmoja yuko Dar akadai kule tikiti hakuna na yana bei kubwa, tukaelewana nikayavuna tukapata gari tukayapeleka. Tumefika Vetenary (Buguruni), tukakuta zaidi ya gari kumi zimeshusha mzigo na ni quality mara nne ya niliyobeba. Nikauza kwa hasara na baada ya kutoa baadhi ya gharama kama ushuru na usafiri nikaambulia laki tano tu (hasara ya milioni 2). Dalali alinionea huruma ilibidi anipe hela ya usafiri na kuahidi kuninunulia mbegu na madawa ili tulime upya. Nikarudi nyumbani nimechoka zaidi ya maelezo. Hapa nilipo nadaiwa milioni tatu na mtaji wangu umekata. Sijakata tamaa na wala sina mpango wa kukata tamaa, nipo natafuta capital niingie mzigoni mwezi wa 12. Kwa sasa nimelima mahindi ingawa mvua nazo zimekata.

NILICHOJIFUNZA:

- ukiwa unafanya kazi sekta binafsi jiandae kisaikolojia kwani unaweza kuondoka muda wowote, jifunze kuwekeza wakati uko kazini

- wakati ukiwa kazini jifunze pia na ujasiria mali, ni ngumu kujifunza kama huna kazi. Kila utakachosikia kinalipa utakikimbilia bila information za kutosha na ni rahisi sana kuanguka

- Kama huna uwezo wa kufanya adjustment ya matumizi kutokana na kipato chako USIACHE KAZI NA USIFANYE BIASHARA. Inanibidi nilale chini, kula mara moja au mbili na kula aina ya vyakula ambavyo sijawahi kufikiria.

- Kilimo kina changamoto kubwa sana huwezi kuzijua mpaka ufanye.
- Taarifa sahihi ndio kila kitu, usifanye kitu kwa mkumbo
- Usikate tamaa, kila kitu kingekuwa chepesi kila mtu angekuwa tajiri. Pigana sana na usisahau kumtanguliza Mungu kwenye shughuli zako.

NB: Kama unaweza kunipa ushauri wa namna ya kufanya kilimo bora, namna ya kupata mtaji au kufanya partnership, unakaribishwa.
Mugomangara wewe nimegudua una tabia hizi 1.Sio mchoyo wa elimu na ushauri 2.Ni mtu asiyekata tamaa kirahisi(mungu akubariki mafanikio yako haya)
Ulivyotoa shauri zako zote zimekaa vizuri ila naomba niongezee ushauri kwa wengine walio kwenye ajira
**Kama mkeo amekaa vizuri sio mbwetekaji.anajituma,mwaminifu mko vizuri kindoa.Usisite kufungua miradi akaisimamia wewe ukiwa kazini.hii itakusaidia kutotetereka ukitolewa kazini.pia mtakuwa wazoefu tayari hasa mambo haya ya ufugaji na kilimo hili jambo limefupisha maisha ya wastaafu wengi.
**Usidharau petty business maana wasomi wengi including wewe na mimi tuna tabia ya kufikiria miradi mikubwa na tupate 100% profit margin kwani ukiporomoka unaporomoka kwa kasi na ukiwa mkata tamaa ndio basi.Kumbuka Bakhresa aliaanza kuuza maji kwenye mifuko ya nailoni na kutembeza kwenye baiskeli.

Nakuinbox
 
Una shamba la eka 10 ni bahati iliyoje. Huko Bukombe ungetenga eka mbili ukaweka mizinga ya nyuki hata kumi tu. Baada ya muda mfupi utavuna asali na kupata mtaji wa kutosha.
 
Afadhali yako umeingia kwenye ajira umepata cha kushika hata kama ni kidogo unashaurije ambao wanamalengo kama hayo unayofanya huku hawana mtaji vitendea kazi na fani ya kujitafutia riziki
 
1. Duniani hakuna haki saaaana, tumia akili.

2. Hata kama unaonewa kazini, kama haikuathiri vumilia tu huku ukijipanga kwa mambo yako binafsi

3. Siku zote ingia kwenye ajira ( with an exit strategy ) huku ukikubaliana na ukweli kuwa kampuni siyo yako na unaweza kuwa terminated anytime

4. Kumbuka mahusiano yako na kampuni yanajengwa na mkataba wako tu, na wewe ni cheap labor ( Ukitimuliwa saa 4 asubuhi, saa 4.02 kuna watu 500 wanataka kazi hiyo hiyo hata kwa ujira pungufu.

5. Maisha ya kujiajiri yanaleta furaha na amani isiyo na kifani, kwa kuwa yanakupa uhuru kamili
Ila kama uhuru huo hautumiki vizuri unaweza jikuta unaamka sa 4:00 unatafuta kijiwe cha kwenda kupiga soga na kuchati.
 
Mugomangara wewe nimegudua una tabia hizi 1.Sio mchoyo wa elimu na ushauri 2.Ni mtu asiyekata tamaa kirahisi(mungu akubariki mafanikio yako haya)
Ulivyotoa shauri zako zote zimekaa vizuri ila naomba niongezee ushauri kwa wengine walio kwenye ajira
**Kama mkeo amekaa vizuri sio mbwetekaji.anajituma,mwaminifu mko vizuri kindoa.Usisite kufungua miradi akaisimamia wewe ukiwa kazini.hii itakusaidia kutotetereka ukitolewa kazini.pia mtakuwa wazoefu tayari hasa mambo haya ya ufugaji na kilimo hili jambo limefupisha maisha ya wastaafu wengi.
**Usidharau petty business maana wasomi wengi including wewe na mimi tuna tabia ya kufikiria miradi mikubwa na tupate 100% profit margin kwani ukiporomoka unaporomoka kwa kasi na ukiwa mkata tamaa ndio basi.Kumbuka Bakhresa aliaanza kuuza maji kwenye mifuko ya nailoni na kutembeza kwenye baiskeli.

Nakuinbox

Nashukuru kwa kuianzisha siku yangu vizuri.

Hili la mke kuwa mpambanaji kwa wale walio makazini ni jambo zuri sana japo wengi hawaliwezi, ukiwa kazini mwanaume unapaswa kumtumia mkeo kama tool kwenye kutafuta kipato mbadala..
 
Bahati mbaya sana sana huwa Mara nyingi haiwi hivi! Duh very painful ngoja niishie hapa hapa
Nashukuru kwa kuianzisha siku yangu vizuri.

Hili la mke kuwa mpambanaji kwa wale walio makazini ni jambo zuri sana japo wengi hawaliwezi, ukiwa kazini mwanaume unapaswa kumtumia mkeo kama tool kwenye kutafuta kipato mbadala..
 
Nashukuru kwa kuianzisha siku yangu vizuri.

Hili la mke kuwa mpambanaji kwa wale walio makazini ni jambo zuri sana japo wengi hawaliwezi, ukiwa kazini mwanaume unapaswa kumtumia mkeo kama tool kwenye kutafuta kipato mbadala..
Samurai mimi mke wangu aliacha ajira binafsi mwaka 2008 baada ya kuona kuajiriwa uchuro.
Nimemtumia kipindi chote hicho sasa tunapeta kazi nimepigwa chini sitamani kurudi.
Ila nimesisitiza aina ya mke uliyenaye uaminifu muhimu.Hukukosea ulivosema wengine hawawezi.Wapo wanawake ukimpa uhuru huu umeliwa
 
Kimoja ulichosahau cha kujifunza mkuu, USIJIFANYE UNAJUA SANA KUDAI STAHIKI ZAKO UKIWA KAZINI. Mara zote pima upepo, kama huna kingine cha kufanya ridhika na ulipo, usiwe mstari wa mbele sana kudai stahiki kwa kudhani ni ukidume. By the way ukielewa duniani hakuna haki isipokuwa mbinguni tu utakuwa na kiasi katika kudai stahiki si kazini tu hata kwenye ndoa hata mtaani!

Safi sana hii..natamani na wengine wengi wasome na kuelewa hii..Asante nimeanza siku yangu vema
 
Aisee mimi heri nifukuzwe tu.Siwezi kusema nyeupe kwenye nyeusi.Never.Huku ni kuufinyusha ubongo,kuona kwamba hapo ni alfa na omega wakati dunia ni pana sana hii
Hakuna aliyesema nyeupe iwe nyeusi mkuu, nilichosema usilazimishe gray iwe nyeusi. Kama unapata gray ridhika fullstop.

Sasa kwa upana wa dunia ukienda lesi na kujifanya mdai haki ndio unapotea mkuu. We unaona ni heri mtoa mada angebaki kazini japo kuna madhira madogo madogo yanayovumilika au hali aliyonayo sasa hivi anavyohangaika?

Unadhani kwenye kilimo ndio kuna haki? Dunia ni moja rafiki, watu walioko makazini ndio walioko kwenye kilimo. Kama unabisha nenda kawaulize wakulima wa korosho walichofanyiwa mwaka jana.
 
Back
Top Bottom