Nilichojifunza ndani ya mwaka mmoja bila ajira

Nilichojifunza ndani ya mwaka mmoja bila ajira

Mbona una Shamba kubwa sanaa
Ushauri hilo Shamba ligawe upande Fanya Kilimo cha umwagiliaji na upande Kilimo cha kutegemea mvua Lima ufuta, ufuta hauhitaji mtaji mkubwa vilevile kama uko buzy shambani unaweza Lima nyanya nunua water pump inch 3 kwa laki tatu na nusu mbegu na dawa haziwezi kuwa zaidi ya laki na nusu baada ya miezi minne 4 utakuwa na mabadiliko
 
mugomangara,
Nakushauri ulime green beans soko lake uhakika ingawa bei sio nzuri sana. Kwa mpambanaji kama ww nina uhakika kwenye mavuno ungetoboa.
 
Mi nakwambia komaa lakini inaelekea un attitude issue, hata ufanye nini uwezi kufanikiwa. Kwenye ulimwengu wa Roho(mshana anajua) wewe unamakwazo tayari na chochote utakachofanya uwezi kutoboa. Be positive kwanza kwakazi ya kwanza, sahau yaliyopita, jipange, usifanye unachofanya kwa hasira ila kwa malengo na bidii. Ila ushauri wako bomba sana.
 
Pole sana..tumefundishwa uvumilivu ila uwe na mipaka..m nakushauri badili uelekeo ondoa shambani..ingia kwenye harakati za kununua mazao..
 
Nina miaka miwili sina kazi, nilifanyiwa figisu kama zako - nimepanga Tabata 250K per month, watoto wa2, mmoja anasoma std 6 Atlas na mwingine std 2 Christ the King. Nitakomaa mpaka tone la mwisho hapa mjini.

NB: Figisu za mjini naziweza vizuri tu-wala sio muoga wa maisha.
Hongera mkuu
 
Achana na kilimo hicho watu tusha poteza pesa sana.jaribu kufuga tena kama unaeneo zuri fuga kuku wa kienyeji,au chimba mabwawa ya samaki hicho kilimo cha tikiti kitakupotezea mda ukipuuza utaona cha mtema kuni.
 
Mi nakwambia komaa lakini inaelekea un attitude issue ,hata ufanye nini uwezi kufanikiwa.Kwenye ulimwengu wa Roho(mshana anajua) wewe unamakwazo tayari na chochote utakachofanya uwezi kutoboa.Be positive kwanza kwakazi ya kwanza ,sahau yaliyopita,jipange ,usifanye unachofanya kwa hasira ila kwa malengo na bidi.Ila ushauri wako bomba sana.
Walokole bana
 
Mkuu, labda uniambie ulikua hukatwi hela ya mafao kila mwezi.

Nilichosoma hapo ulikua unadai stahiki zako kwa mwajiri, kitu ambacho ingekua ni mafao ya asingeweza kukwambia nenda kashtaki popote, isitoshe yale ungepewa na mfuko husika.
rudia kusoma mwanzoni kabisa mwa post hii utaelewa alichoandika,nahsi umeanzia njiani kusoma
 
Hapa tunataka kujifunza aliyopo hapa ndani na ni mkulima wa tikiti atueleze alilima kiasi gani alipataje mavuno na faida ilikuaje?kwa pamoja tujifunze kuhusu kilimo hicho mimi sijawahi kukielewa kabisa kwa sababu kila analalamika kukata pesa.naweza sema ni bora hata mahindi soko likiwa baya unaweza weka hata miaka kadhaa...tikiti wengi halijawahi kuwaacha salama kwanini?je kuna shida gani kwenye kilimo hicho?ni juzi tu jamaangu mmoja amelima huko mbeya ekari kama 7 aliuza mbaka kapagare kake kwa ajili ya kutunza kabla ya hapo alikua amesha tumia kama m.6 akauza kapagare m.5 akaingiza huko kilicho tokea acha tu,mbaka sasa anatembea anaongea peke yake
 
Mkuu naomba nikushauri hivi

Kama utaweza fanya kilimo cha kisiasa

Chukua Sampso za udongo then peleka SUA au Ardhi University pale mtafute Dr mmoja yeye ni field coordinator wa SEST atakushauri vizuri sana kuhusiana na nn kimekosekana na nn kimezidi shambani mwako kulingana na zao unalotakakupanda, andaa kama budget ya laki 5 tu.

Kuwa mvumilivu mkuu, nipo njiani kuingia kwenye kilimo ila nataka niingie kusomi na kitechnology zaidi mugomangara,
 
Hapa tunataka kujifunza aliyopo hapa ndani na ni mkulima wa tikiti atueleze alilima kiasi gani alipataje mavuno na faida ilikuaje?kwa pamoja tujifunze kuhusu kilimo hicho mimi sijawahi kukielewa kabisa kwa sababu kila analalamika kukata pesa.naweza sema ni bora hata mahindi soko likiwa baya unaweza weka hata miaka kadhaa...tikiti wengi halijawahi kuwaacha salama kwanini?je kuna shida gani kwenye kilimo hicho?ni juzi tu jamaangu mmoja amelima huko mbeya ekari kama 7 aliuza mbaka kapagare kake kwa ajili ya kutunza kabla ya hapo alikua amesha tumia kama m.6 akauza kapagare m.5 akaingiza huko kilicho tokea acha tu,mbaka sasa anatembea anaongea peke yake
 
Unachokifanya leo, sio lazima kikulipe leo. Subira ni kitu muhimu na Mungu yu pamoja na wenye subira, kujitoa na kuwa committed kwa kile unachokifanya ndio msingi wa mafanikio yako ya kesho. Stay calm and positve, Good results will come.
 
Back
Top Bottom