Huwa namuangalia Mume wangu jinsi ambavyo anahakikisha tupo comfortable kila siku, hawazi another pair of shoe au cloth for himself before taking care of us...ni Mume na Baba bora sana kwetu. Sijui hata maisha yangekuwaje bila yeye. Najua najitahidi sana kuwa mke bora na labda sifanyi kilakitu sawa ila hata kwa kidogo naamini anajua nathamini sana kila anachofanya na ni maombi yangu Mungu azidi kumtunza na kumbariki.


Asante sana kwa kutukumbusha kuwashukuru na kuthamini juhudi zao za kutunza familia ni rahisi sana kuchukulia poa kwasababu ya kuwa ni jukumu lao.
Duh? Umeongea kwa hisia sana
 
Natumaini mko poa,

Nilipoteza baba nikiwa najitambua kiasi nikabaki na mama pekee. Mama alikuwa mchakarikaji sana lakini kuna vitu vilibadilika sana mambo hayakuwa kama yalivyo awali.

Maisha yalikuwa tofuti sana na kipindi baba yangu yuko hai nikaona ni kiasi gani mzee aliteseka kuhakikisha tunaishi vizuri na tunakuwa salama sisi na mama yetu nimejisikia kuwasemea leo.

Kuna wakati wanaume wanapitia mambo mengi magumu kwaajili ya familia zao ama watu wanaowapenda hasa katika utafutaji wa riziki. Kuna walio na kazi za halali, kuna wengine wahatarisha hata maisha yao Ili kuhakikisha mambo yanakuwa sawa lakini kitu kizuri ni kwamba sio wasimualiaji wazuri wa mahangaiko na mateso yao wakati wanafanya hayo.

Kuna ambao wanatamani asubuhi isifike kwani kwao ni mateso matupu. Hadi jua linazama ni mwendo wa mahangaiko na ukute kuna wakati hawapati kabisa lakini ndo hivyo waliumbiwa mateso, ni mwendo wa kichwa kupata moto tu.

Wanawake wengi tumekuwa ni wazuri kwa upokeaji lakini ni wachache wa kushukuru. Tuwahurumie na tuwaombee japo wana mabaya yao na madhaifu yao walokuwanayo lakini watabaki kuwa ni muhimu kwa ustawi wafamilia zetu.

Kwa mliopo kwenye ndoa mjitahidi kuwatia moyo na kuwahurumia pamoja na udhaifu wa waume zenu, lakini inawezekana bila huyo mambo yasingekuwa hivyo unavyoyaona; pia mkumbuke pia hatma za watoto wenu.

Na sisi wa jumuiya pia tuwaombee na tuwashukuru kwani bila wao tusingeonekana huku mtaani.

Niliowakwaza mtanisamehe, ni hayo tu.
🪴
Chukua maua yako
 
Maua yako haya hapa chukua
20230511_012247.jpg
 
RRid
Wanaume tumeumbwa mateso mateso kuhangaika

Ukizariwa mwanaume leo ujue kila kitu kwako kitakuwa ni tabu
Wazazi wako wakizeeka macho yao ni kwako
Familia yako NYUMBANI macho yao ni kwako

Ndio mana nilipopatwa na AJALII nilijua FAMILIA yangu itaathirika

Baaba wa FAMILIA ndio NGUZO ya NYUMBA
Leo nimeteteleka NYUMBA inayumba
Ninateseeka na MARADHII naumia MOSHI na mawazo
sijui WATOTO wangu watasoma viipi



Sikiliza hapo kilio Cha mwanaume akiililia FAMILIA yake
MSONDO NGOMA music Band
Sikiliza JUMBE HUSSEIN anavyolalamika
sauti ya RADI /ZEGE gurumo akitia nasaha

TX moshi william alitunga huu wimbo alipopatwa AJARI akavunjika MGUU sasa ule msoto wa kukaaa nyumbani kuuguza mguu akaja na kibao hichi maridhawa
Kuna wakati TX MOSHI ilimlazimu kwenda UKUMBINI na HOGO na magongo ya kutembelea kuimba ili kuiletea RIDHIKI familia yake isiadhilike 7bu yeye ndo alikuwa baba wa familia
Yaani yalioimbwa humo ndio yalikuwa yakimtokea dhaili TX mwenyewe mpka akaja na KIBAO hicho ambapo ndio ulikuwa utungaji wake wa mwisho kabla hajafikwa na MAUTI mguu ulimsumbua haukupona mpk akafikwa na MAUTI


Threads yako imenikumbusha mbali sana mpk nikaukumbuka huu wimbo

Riziki au rizki sio ridhiki
 
Wanaume wa second and third selection hawahusiki kabisa kwenye huu uzi. Wao wakae mbali
 
Back
Top Bottom