Nilichogundua kuhusu Arusha

Unamaanisha corporate tax...?! Hebu niambie wale wafanyabiashara wa samaki pale Kamanga wanalipa vipi kodi TRA...?! Au wale wanaopanga bidhaa chini...
 
Hiyo ni kwa mwaka mkuu... Yaani kelele zote za Mwanza kodi wanayokusanya kwa mwaka wamezidiwa mpaka na kawilaya choka mbaya cha Temeke..
Mkuu tmk sio choka mbaya. Kuna viwanda vingi tmk. Tmk imebadilika sana.
 
Unamaanisha corporate tax...?! Hebu niambie wale wafanyabiashara wa samaki pale Kamanga wanalipa vipi kodi TRA...?! Au wale wanaopanga bidhaa chini...
Corporate Tax 30% ya Profit unaweza isiwe Large Tax vile vile... Large tax payers ni wale wanaolipa kodi kuanzia Billion 1 p.a nadhani.. Nitarejea tena kuangalia kiasi.. Wewe ukiwa na kikampuni chako na una faida ya Million 500 huwezi kuwa Large tax payer lakini utalipa Corporate Tax ya 30% kwa faida yako..

Kwahiyo una maanisha Mwanza makusanyo madogo sababu wafanyabiashara wa samaki hawalipi kodi? Kwani Arusha wauza maparachichi na ndizi wao wanalipa? Alafu mbona hata HDI Arusha iko juu sana ya Mwanza.. Hapa par capita income Arusha imeizidi Mwanza..
 
Jamaa anafikiri wale raia wa kwenye slums ndio wanaolipa kodi sana...

Aangalii kuna shughuli gani eneo husika, ndio maana anajisifia wao wanalipa kodi...
Wewe ni mjinga wa mwisho.. Hizo shughuli kwanini zisiwe Mwanza? Wewe hujui hizo shughuli ndizo zinazungusha pesa kwenye hilo eneo husika?

Kwamfano Temeke tu tukisema ina maduka 50,000 yanayohudumia hiyo population ya watu Laki 7 ambao wamevutwa kuishi hapo kwasababu ya hizo shughuli husika unazozisema na kila duka likatoa kodi ya 200,000 average kwa mwaka hiyo tayari ni Billion 10.. Kwahiyo maduka pekee yaliyopo Temeke yanalipa kodi kubwa kuliko hata kodi inayokusanywa na mkoa mzima wa Lindi.. Hapo bado hujagusa biashara nyingine..

Wewe unafikiri Viwanda tu ndivyo vinaleta kodi kubwa pasi na shughuli ndogo ndogo za ujasiriamali?? Ujinga huo
 
Hapo nilikuwa nakuonyesha mantiki yako watu wa eneo fulani wanalipa kodi kuliko wengine, sasa nikawa nakuonyesha haupo sahihi...

HDI Arusha ipo vizuri, Per Capita ipo vizuri unaweza leta hesabu za per capita zinafanywaje...?!

lakini Growth Domestic Product (GDP) inazidiwa hadi na Shinyanga na Mwanza ikiwa ya pili baada ya Dar es salaam hapo ni kabla ya Mwanza na Shinyanga kugawanywa na kutoa mikoa mingine miwili ya Geita na Simiyu...

Nadhani kwa sasa Mkoa wa Arusha ni mkubwa kuliko Mwanza, lakini population bado ni kubwa kuzidi Arusha, nikirejea idadi ya wapiga kura maana baada ya Dar es salaam ilifuatia Mwanza baadae Mbeya hapo kabla Mbeya haijagawanywa kutoa mkoa wa Songwe kwa sasa Mbeya idadi itakuwa imepungua...

Ukirudi katika zile data za NBS kwa GDP Arusha ilikuwa ya saba, lakini kwa GDP per Capita ipo juu lakini na yenyewe ikizidiwa baadhi ya mikoa kama Iringa na Kilimanjaro kama sikosei...

Na hapo inatoa tathmini kwamba kuna unafuu na sio kwamba ni tajiri, au wananchi ni matajiri, la hasha...
 
Hapana aisee, ngojea nikupe elimu halafu uache maswala ya kuitana wajinga, nikupe mfano wa Banana investment hawa wapo Arusha, huwezi kuniambia banana wanahudumia Arusha tu, hawa Banana wanafika mpaka Mwanza hadi Dar es salaam ...

Sasa je kwa mantiki hiyo unataka kuniambia watu wa Arusha wanakunywa sana Banana ndio maana wameamua kujenga huko kiwanda cha Banana...?! Je na sio kwamba kimejengwa huko ili kupata urahisi wa malighafi kama vilivyo viwanda kwa mfano vya miwa...

Tukirudi pengine unaweza ukaniambia yale maduka kodi yake inaweza ikawa sawa na kiwanda au Arusha kuna maduka mengi kuzidi Mwanza, sababu unapoweka duka au bar unaangalia population, sasa je ni wapi kuna population kubwa...?!

angalia zile estate pia, taasisi a serikali linganisha Mwanza na Arusha uone nyingi zipo wapi, miradi mingi ipo wapi...?! Sasa labda tuulize waliopeleka zamani miradi pande za huko ni kwanini walifanya hivyo, ilhali inahudumia maeneo mengi...

Kwa mfano Tanzania nzima vitu vinatoka Dar es salaam kuhudumia mikoa mingine, je unataka kuniambia walifanya hivyo ku lenga watu wa Dar wenyewe tu...?! Hivyo viwanda vya Temeke vinahudumia Tanzania nzima na sio Temeke tu, na hayo maduka hayatoi kodi kubwa sana yale ya kina Mangi...
 
Unajicontradict mwenyewe bila hata kujua.. Na wala sijui nikujibu nini maana hueleweki.

Miradi mikubwa ya serikali unayoisema huko Arusha ilipelekwa kwa kupendelewa? Nitajie taasis za serikali zenye makao makuu Arusha kama unavyosema na ambazo zimepelekwa kwa upendeleo..

Tukirudi kwenye swala la viwanda bado tunarudi pale pale tu.. Kodi kubwa kubwa zina mfuko wake.. TBL ina makao makuu Dar lakini usifikiri kodi yake inalipwa Kinondoni au Ilala.. Kodi zao zina makamishna wao.. Hivyo hivyo kama Megatrade na Banana wanalipa kodi kuanzia 1 Billion hiyo kodi inalipwa TRA Makao Makuu.. Wale makamishna ndio wanakagua mahesabu na ndio wanaokusanya kodi. Hivyo hivyo kwenye biashara za mazao ya biashara kama Pamba, Korosho na Kahawa..

Unaposema eti sijui viwanda na taasis ndio zinafanya kodi ya eneo husika kuwa kubwa na si mzunguko wa fedha mahali hapo na hali ya uchumi ya wakazi wa hapo ni bla bla tu na uongo.. Kilimanjaro wana taasis zipi za serikali? Wana viwanda kuzidi Mwanza? Mbona Kilimanjaro nao wanakusanya kuliko Mwanza?? Au sababu ya Mlima Kilimanjaro na si shughuli za uchumi zilizopo?
 
Naona umeng'ang'ana kwenye angle ambayo umeibuni ili kujiweka salama zaid kwenye ligi...ok poa mkuu
 
Unao uelewa wowote wa uchumi mkuu?? Unajua maana ya GDP na GDP per capita?

Well, Tanzania tuna GDP kubwa kuliko Botswana.. Lakini Botswana wana GDP per capita kubwa mara tatu sita zaidi ya yakwetu.. Botswana GDP per capita yao inakaribia Million 14 wakati Tanzania ni Million 2 pekee..

Kukutafsiria zaidi ni kwamba, watu kumi wanaweza kulima shamba la ekari 2 kwa siku moja wakati watu wawili watalima hizo ekari 2 kwa wiki 1.. Ila kwenye kuvuna watu 10 watapata kila mmoja gunia moja tu la walicholima wakati wale watu wawili watapata kila mmoja magunia matano..
 
Okey conclude bas kuwa mosh ni zaid ya Mwanza....maana ninachokwambia huelewi.....bas service zilizopo hapo mosh zinazid mwanza... Na moshi ni zaid ya mwanza....maana hapa napigia mbuzi gitaaa
 
Okey conclude bas kuwa mosh ni zaid ya Mwanza....maana ninachokwambia huelewi.....bas service zilizopo hapo mosh zinazid mwanza... Na moshi ni zaid ya mwanza....maana hapa napigia mbuzi gitaaa
Sasa ni kipi cha muhimu kiko Mwanza na Moshi hakipo? Nitajie kimoja tu
 
Labda nikuulize tu... hivi Kilimanjaro kuna maduka mengi kuzidi Mwanza...?! Na kama hakuna je kodi ya Kilimanjaro inakusanyiwa wapi...?! Vipi kuhusu utalii..?! unajua unachangia kiasi gani, wale watu wanaokuja kupanda mlima vipi...?! Ile KIA ni international mizigo ikishukia pale hakuna inachochangia...?!

hivi hivi vyuo vilivyopo huku Arusha inamaana hawalipi kodi...?! Unaweza ukaniambia ni kwanini Nelson Mandela University imejengwa Arusha badala ya Mbeya...?!

Arusha kuna EAC, kuna TANAPA kuna AICC...

Unaweza ukaniambia ni kwanini zile cities mbili za NHC zinajengwa mkoa mmoja na nyingine inajengwa Dar es salaam Kawe...?!
 
Humu kuna vitu hata mimi nilikuwa sijui. Hata mimi nilifikiri Dar kuwa juu ni kwasababu ya makampuni makubwa na viwanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…