Niliamini ananipenda kumbe alinifanya kichekesho

Niliamini ananipenda kumbe alinifanya kichekesho

NILIPOISHIA
Tunafanana umri na Deo lakini linapokuja suala la Ugegedu mwenzangu amenitupa mbali kiasi, nikamwitikia huku nikijiwazia huyu kichaa asije kuharibu mazima nikashindwa kuonana na chidada wangu.

Tukafika kwa kina Deo na kuwakuta madogo nje, akawauliza kuhusu bibi yake wakasema ametoka atarudi jioni.

Muda huo mwili na nguo zetu zilikuwa zimewivia vumbi jekundu. tukaoga na kujiweka sawa, muda huo sms za Laima zilikuwa zinamiminika tu Zile za 'my upo wapi sasa, mbona kimya wangu' na nyingine nyingi.


ENDELEA

Deo akaniaga anatoka atarudi muda sio mrefu ila akanipa angalizo nisimjibu chochote Laima, nilikubaliana nae huku nikijiuliza anataka kufanya nini huku kwa Laima.

Baada ya muda mchache tu akarudi.

"Oya Kim leo nataka nikuoneshe Newala, nataka tuizunguke hadi basi, japo nimechoka kuendesha lakini kwa sababu ni mizunguko isiyokuwa na haraka nikuendesha mimi mwenyewe. hapa itabidi usahau kidogo kuhusu Laima kwanza wewe kazi yako umeshamaliza kutoka Mtwara kuja huku sio jambo dogo kaka. sasa kama yeye atashindwa kuja sehemu ambayo wewe utamuhitaji atakuwa mpuuzi, kwanza nigee simu yako"

Nikampa simu deo akaandika meseji kwa laima.

'Nipo Tandahimba sasa pikipiki imezingua ila nipo kwa fundi, pia simu yangu inazima zima haina chaji nikifika huko nitakupigia'

Iliporudisha lipoti akaizima.

"Kim leo ni siku ya kupambana kwakuwa kesho tunayo, kwakuwa lengo lake yeye ni kuonana basi hata kesho mtaonana freshi tu"

"Poa mwanangu wewe ndiyo askari wangu kwenye hili"

Uhalisia ni kwamba nilikuwa na hamu ya kumuona Laima kinoma sema ilibidi nimkubalie tu Deo kwa vile yeye ndio kila kitu kwa huku tulipo.


Tukavaa viatu vya kuingiza na mbwembwe nyingine kibao tayari kwa kuingia mtaani.

Mida hiyo ilikuwa ni 5, tukatembea sana na Deo tukiwa katika chuma. Kitu niliinjoy sana kuuona kwa utulivu kabisa mji huu wa Newala huku kila tunakopita Deo akinitajia jina la kata na mtaa. lakini hiyo yote haikuniondolea wazo kuu ambalo lipo kichwani ambalo ni Laima.

Muda huo simu ipo mfukoni na sipaswi kuiwasha kwa maelekezo ya deo.

Deo alivyochoka kuendesha chuma nikaikamatia mwenyewe.

Tulizurula saana unaweza kudhani baba zetu wana sheri hapa Wilayani.

Mida ya saa nane tukaingia mgahawani tukaagiza msosi, wakati tunakula Deo akaniambia naweza kuiwasha sasa na nimwambie Laima kwamba ndiyo natoka Tandahimba.

Kufungua simu meseji kibaao za Laima.
Kabla sijafanya chochote simu inaita ni yeye ndio anapiga.

Nikapokea na kumpa maelezo kama aliyonipa Deo huku nikiongeza na yangu, alifurahi lakini pia aliniuliza itakuwaje nikifika jioni maana kutoka Tandahimba hadi Newala ni parefu kiasi.

Nilisema sijuwi maana mwenyewe nimevurugwa hadi muda huo ukizingatia sehemu ninayo kwenda ni ugenini na natakiwa kufikia Gest.

Nilimuaga na kukata simu.

"Kim kama una mawasiliano ya muhimu nyumbani kopi namba unazohitaji kwenye simu yangu, hiyo somu yako izime tena, ikifika saa 10 utaiwasha"

Nikafata kauli ya Deo na kuendelea na kuendelea kuuchapa mpunga huku tukimwaga porojo kwa wahudumu.

Tukarudi kwa kina deo na kumkuta msichana ambae ni mjukuu wa bibi yake Deo, tukasalimiana akataka kutuandalia chakula Deo akasema tupo gudi.

Nikaenda kuoga tena huku nikiisubiri saa 10 kwa hamu.

Nikaingia kwenye chumba ambacho tumeweka vitu vyetu, nikafungua begi na kuangalia tena zawadi nilizomwandalia Laima ilikuwa ni gauni moja refu jekundu, viatu na vikorombwezo vya urembo wa kike cheni, Pete hereni nk.
Kumbuka licha ya deo kunambia umbo la Laima yeye mwenyewe pia amewahi kunambia katika maongezi yetu.

Muda ulivokaribia Deo akanambia nichukue begi tuondoke, tukaziacha nguo za Deo na kuondoka kuelekea mtaani kwa kina Laima.
Hii ilikuwa ni saa 10 na dakika chache.

"Kwahiyo naiwasha sasa simu"

Deo "Hahaha! Mzee unajikuta kama unaenda kuonana na muhindi!"

MIMI "Mwanangu wewe kazi ya jeshi ingekufaa una misimamo mikali kinyama yani"

Deo "aaa Hapana Mwanangu shida ni kwamba kwa sasa mimi natumia akili wakati wewe unapelekwa na hisia.
Hapa sasa natakiwa kuwa makini maana tunakaribia mitaa ya kwao isije akanidaka hapa mchongo ukaharibika, nipe ile kepu yako nyesi"

Tukaendelea na safari hadi sehemu moja ambayo ina mchanganyiko wa watu, tukapaki pikipiki kwenye frem moja ambayo ina bendera ya chama cha siana.

Deo akasalimiana na mshikaji mmoja ambae alitoka kwenye ile fremu.

"Kim mpigie sasa lakini usifeli fanya kama nilivyokuelekeza"

Nikajitenga kidogo na kuwasha simu. Nikampigia kumwambia nimefika, aliniuliza nipo sehemu gani aje ila nikamwambia asubiri kidogo nimefatana na mdau ananipeleka Gest nikadake chumba.

Alipohitaji kujua ni Gest gani nikamwambia sijui na kuuliza ni Gest ipi ambayo itakuwa ni rahisi kwake kuja. Msimamo wake juu ya kuja Gest ulikuwa pale pale huku akisema anaweza kufika nje na mbali kabisa ya Gest nitakayo kuwepo na tutaongea huko.
Nilimfosi sana kwa kumpa vigezo vingi ikiwemo kukutana nae mazingira ya mitaani nahofia usalama wangu ukizingatia mimi ni mgeni, hata hivyo kwa nilivochoka nikipata chumba nitahitaji kupumzika kuliko kuanza kuzurula tena.

Tulipishana sana kauli hapa hadi mwisho nokaongea maneno ya nongwa na kulalamika kwamba haoni thamani yangu.

Mwisho nikakata simu bila ya muafaka kupatikana.

Nikamcheki deo nikiwa na hasira kidogo.
Deo akasema wewe hupaswi kupaniki kwa sababu hapo unaigiza, lengo lako ni kuonana nae hilo la kugonga ni wazo langu mimi.

Laima alituma sana meseji na kupiga simu ila kila akipiga nilikuwa namsubirisha, kwa kumwambia Subiri dakika chache nakucheki.

Deo akaniomba simu na kubaki nayo yeye akichati na Laima huku tukizurula sehemu mbali mbali kwa miguu maana pikipiki na begi alimwachia mshikaji wake.

Kadiri jioni inavyozidi kuingia ndivyo mji unavyozidi kushona watu mabarabarani na sehemu za masoko.

"Kim huyu malaya wako msenge sana utaenda kumuona kesho mimi nimembloku huku"

Akanipa simu huku akinisisitiza nisiitoe namba ya Laima kwenye blacklist ni bora ateseke yeye kimawazo kuliko mimi.

Kusema kweli roho ilikuwa inaniuma kwa upande mmoja kutokumuoka Laima siku ya leo lakini upande mwingine nilikuwa najiona mjinga sana kumwamini mtu ambae anashindwa kuja nilipo kwaajili yangu.

Kutazunguka hadi jua linazama tukarudi zetu kwa wakina Deo.
Tukamkuta bimkubwa na kusalimiana nae nikazama chumbani kwetu huku mwili ukiwa umechoka balaa..

Nikajitupa kitandani nikajilaza chali huku macho yakiwa mazito mno.

"Oya Kim oya, simu yako inaita hiyo"

Alinishtua Deo kutoka usingizini huku akinitikisa.

Nikashtuka nikaichukua simu na kuipokea bila kuangalia namba.

MIMI 'Halo'

'Haloo Kim uko wapi kwani, mbona napiga simu muda mwingi hupokei? halafu ndiyo umeamua kabisa kuibloku namba yangu? umeshindwa kabisa kunielewa nilichokwambia, inamaana unataka utengeneze picha kwamba mimi ni adui kwako?'

Aliongea kwa sauti ya kujiliza sana Laima, niliiangalia simu na kuona kanipigia kwenye namba ngeni.

Nilkaa kimya hata nisijue namjibu nini.

'Kim uko wapi sasa hivi'

MIMI 'Gest'

YEYE 'Gest gani?'

MIMI 'Sijuwi jina'

YEYE 'Waulize wahudumu uniambie ni Gest gani nije kim mbona una maamuzi magumu kiasi hiko'

MIMI 'Sawa'

Nakakata simu.

"Oya kwani ni saa ngapi sasa"

DEO "Ni saa mbili tu ngoja niunge Gest chapu kama tunaweza kupata tukifeli tutajua tunafanyaje"

Akawapigia watu anaowajua mwenyewe wakati mimi namuangalia tu.

"Oya mwambie upo Shamana Guest house mimi namuaga bimkubwa tuondoke"

Nikamtumia meseji Laima kumuelekeza.

Tukaondoka na chuma yetu hadi kwenye hiyo Gest ambapo ni mwendo wa kama dakika tano tu, hali ya hewa muda huu ilikuwa ni ya baridi ukilinganisha na Mtwara mjini.
Deo akanipa utaratibu wote na kuniacha.

Nikaingia chumbani na kukaa kitandani huku nikisinzia.

Kama baada ya dakika 20 hivi nikastushwa na sauti ya mlango ukifunguliwa niliinua kichwa haraka na kuangalia mlangoni.

Nikamwona mtu mnene mfipi kiasi akiwa amevalia nguo nyeusi na usoni amevaa kininja, umbo lake tu lilitosha kuniambia kwamba huyu ni mwanamke ekafunga mlango na kusogea nilipo.

Akafika na kukaa pembeni yangu akavua nikabu yake usoni na kunigeukia.

"Jamani kweli nyinyi ma last born ni watata kwahiyo ndiyo uliamua kweli tusionane"

Sauti yake ilinithibitishi kwamba kweli huyu ni Laima wangu.



Nitaendelea ndugu zangu.
 
NILIPOISHIA.
Baasi bwana pakakucha nikafanya usafi geto huku wazo likiwa ni leo nitamwingiaje yule dada.
Nikafanya kila kitu home na kuingia Road,
Wakati niko zangu mgahawani Sms hiyo.. kucheki Laima.

'Unaendeleaje na hali yako kaka, vipi ulithibitisha kwamba mimi siyo mtu ambae ulikuwa unamwitaji'

MIMI 'naendea vizuri kiasi, nitakupigia muda kidogo maana sasa nakula ili niende nikajicheki zahanati'

YEYE 'Sawa ugua pole'

MIMI 'asante'

Ni kama ladha ya supu na chapati iliongezeka hivi, nilifakamia huku moyoni nikisema tayaari.. akili yenyewe ilikuwa na kazi ya kuvuta picha tu ya anavyofanania huyo chibonge.

ENDELEA
Kipindi hiki nilikuwa natembeza mtumba naenda kulenga mnadani naingia kitaa kutafuta ugali.

Basi nikaingia zangu misele mida ya saa 7 hivi nikamrukia hewani wakati nipo kitaa natembeza nguo.

YEYE 'Halo'

MIMI 'eee mambo vipi'
Hapa nilichangamka sio kitoto.

YEYE 'poa habari za mchana'

MIMI 'amani tu dah samahani hii namba nilipewa na dada mmoja hivi anaitwa Laima, huwa tunafanya biashara ya nyanya sasa kama wiki nyuma aliibiwa simu, nilipofika kwenye biashara yake ndio akanipa hii namba kama namba yake mpya, niliisevu tu sikuwahi kumpigia nimeshangaa jana napiga nakupata wewe. hii asubuhi nimemtafuta mama flani ambae wanafanya biashara pamoja amenitumia namba za huyo dada.
Nilipomcheki
Nikamuuliza kuhusu namba hizi anasema labda alivurugwa tu wakati ananipa maana hazifanani kabisa na namba zake. Kinachonishangaza ni kwamba mmefanana majina hadi sauti yaani anaongea kama wewe'

YEYE 'Ha kweli binadamu wawili wawili!'

MIMI 'kabisa Samahi kwa kukusumbua lakini'

YEYE 'aah ni kawaida hamna shida, vipi umepona mbona umechangamka hivyo'

MIMI 'Hapana ila niko poa nimeenda kucheki ni maralia tu'

YEYE 'Ahaa kwani uko wapi'

MIMI 'Mtwara mjini kuna sehemu inaitwa Mtawanya, umeshawahi kufika Mtwara mjini?'

Nilidanga'nya mtaa ili kumlinda Deo asije julikana kama ameuza namba, lakini pia kuweka uhalisia kwamba homa imenifanya nisiwahi kwenda kuchukua nyanya maana Mtawanya ni sehemu ya Mtwara mjini ila imejitenga kidogo na sehemu zenye huduma kama stendi masoko nk.

YEYE 'Ndiyo nishafika kuna baba mdogo anaishi huko mtaa wa Ligula huwa nakuja kwake'

MIMI 'Ahaa basi kama ni hivyo namba zako sitazifuta pengine kuna siku utakuja huku unibebee ming'oko'

YEYE 'Hahaha vitu vyote vya kuomba zawadi Ndiyo utake ming'oko hata hivyo mimi naishi newala mjini hatuchimbi ming'oko labda kununua'

MIMI 'Ahaa kumbe newala nayo kuna mjini na vijijini!'

YEYE 'ndiyo, hujawahi kufika kwani!'

MIMI ' Ndiyo sijawahi ila nasikia watu wakisifia tu kwamba mandhari yake ni nzuri, natamani kufika lakini siwezi kwenza sehemu ambayo sina ndugu wa kumfikia hata kama kuna Gest'

YEYE 'ni kweli ila ndugu ushapata sasa unaweza kufunga safari utakapo amua'

MIMI 'Hahaha kweli!'

YEYE 'Ndiyo'

MIMI 'dah vizuri, nikitoka hapa naenda kwa seremala kuchonga kibubu nianze kuweka nauli'

YEYE 'Hahahaha! Kuchonga kibubu safari ya Newala? ingekuwa unataka kwenda Ulaya!'

MIMI 'hahaha sawa bhana, nakuacha kidogo nitakucheki mida'

YEYE 'Sawa mchana mwema'

MIMI 'na kwako'

Zikapita kama wiki mbili hivi nikiwa nawasiliana na Laima, kitu nilichokigundua kutoka kwake ni kwamba anapenda kucheka balaa, yaani anapenda kucheka kupindukia.

Mjomba unaesoma kama wewe ni mwalimu na umeoa huku Mtwara na umemwoa chibonge anaependa kucheka kupindukia. Nifate Pm mkuu unatakiwa kunilipa chochote kitu maana nilikuburudishia mwanamke wako bila malipo yoyote, yaani ilikuwa mimi nina kazi ya kumburudisha wewe una kazi ya kum bandua hadi ukaona haitoshi ulipohama Mtwara ukaamua kumchukua jumla jumla.

Baasi bwana... Siku ya kumtongoza rasmi ikafika, Jamani ukiwa huna hela unakuwa na ubunifu mno kwenye kutongoza.

Ilikuwa jioni ya saa moja nikiwa nimetulia tuli home, nilikuwa kitandani nimelala kichwa nimekilaza kwenye mto miguu nimeiwe kwenye ukuta.
Nikamkoli kama ilivo kawaida akapokea.

Baada ya kusalimiana:

MIMI 'Laima kuna kitoto cha ndege nahitaji tukifuge mimi na wewe, hicho kindege ni kichanga kabisa na kitahitaji huduma zetu ili kiweze kukua na hatimae kianzishe vizazi vingine vya ndege ambavyo vitaipamba dunia na kuifanya iwe sehemu nzuri zaidi ya sisi kuishi'

YEYE 'Hahahahaha! Kim umekula lakini? Habari za kufuga ndege umezitoa wapi wakati sisi tupo mbali?'

MIMI 'Nimekula eee, Umbali sio kikwazo kabisa kwa sisi kumfuga huyu kinda, na kama atakosa matunzo hadi akafa wakati sisi tupo itakuwa temefanya dhambi kubwa mno'

YEYE 'Hahahahahahaha..! unavyoweka msisitizo basi utafikili kweli huyo ndege yupo na yupo mikononi mwako'

MIMI 'eee ninacho hapa kipo moyoni kindege penzi sio vizuri tukakihujumu'

YEYE 'hahaha Jamani sasa mimi sihitaji kufuga na wewe hicho kindege penzi tuendelee na huu urafiki wetu, kama utahitaji kumfuga huyo ndege na kuruhusu tafuta mtu ambae atakuwa sahihi kwa wewe kufuga nae'

Jibu hili huwa ninalikumbuka hadi leo na kama ningemaliza maongezi yangu hapa nisingekuwa mtumwa wa mapenzi na mtumwa wa kifikra kwa huyu mwanamke.

Nimesema mtumwa wa kifikra kwa sababu kuna kipindi niliwahi kumwambia anitajie kiasi chochote kile cha pesa nimpatie ili abadilishe namba zake za simu, hii ni baada ya moyo kukubali ukweli kwamba huyu mtu hanipendi.
nilikuwa natamani kumuacha lakini nashindwa na kikwazo kikubwa ilikuwa ni namba zake zilikuwa kichwani.

Japo mwisho alinikubalia lakini hili nahisi ndiyo lilikuwa jibu sahihi.

Naendelea
Vijana wa CCM hao. Nyie ndio Mtaji wa Mama Samia. NO REFORM NO ELECTION.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom