Niliamini ananipenda kumbe alinifanya kichekesho

Niliamini ananipenda kumbe alinifanya kichekesho

NILIPOISHIA.

YEYE 'hahaha Jamani sasa mimi sihitaji kufuga na wewe hicho kindege penzi tuendelee na huu urafiki wetu kama utahitaji kumfuga huyo ndege na kuruhusu tafuta mtu ambae atakuwa sahihi kwa wewe kufuga nae'

Jibu hili huwa ninalikumbuka hadi leo na kama ningemaliza maongezi yangu hapa nisingekuwa mtumwa wa mapenzi na mtumwa wa kifikra kwa huyu mwanamke.

Nimesema mtumwa wa kifikra kwa sababu kuna kipindi niliwahi kumwambia anitajie kiasi chochote kile cha pesa nimpatie ili abadilishe namba zake za simu, hii ni baada ya moyo kukubali ukweli kwamba huyu mtu hanipendi.
nilikuwa natamani kumuacha lakini nashindwa na kikwazo kikubwa ilikuwa ni namba zake zilikuwa kichwani.

Japo mwisho alinikubalia lakini hili nahisi ndiyo lilikuwa jibu sahihi.

ENDELEA.
Kama ilivyo ada hakuna mwanaume anaridhika kwa kukataliwa kwa jibu moja, aidha umkatae ama umkubali lakini ni lazima kutakuwa na papatu papatu za hapa na pale hasa Kama jibu la kwanza litakuwa ni la kupinga ombi.

Nikaendelea kuongea na Laima lakini hapa sikufanikiwa kufua dafu.

Maongezi yaliendelea kwa wiki kadhaa huku nikikumbushia ombi langu kila baada ya siku mbili tatu lakini msimamo wa Laima ulibaki pale pale.

Ilifika hatua nikajikatia tamaa kabisa ya kumnasa mrembo huyu. taratibu nikaanza kupunguza mazoea bila yeye kujua, hadi ikafika muda nilikuwa simtafuti kabisa yeye tu ndiyo anaanza kunitafuta, kigezo changu ilikuwa ni ubize kutokana na kazi japo nikimpokelea simu tuna piga stori vile vile tu yaani kiasi alishindwa kujua kwamba moyoni nilianza kuipanda chuki juu yake.

Taratibu mpango wangu ukaanza kukomaa, ikawa sasa nikiongea nae naongea kawaida tu na sio uzuzu na porojo Kama alivyonizoea, ama muda mwingine naongea nikiwa mkavu kabisa.

Niwe muwazi kwenye sekta ya kuusoma udhaifu wa huyu mwanamke nilifanikiwa pakubwa, hivyo nilikuwa situmii nguvu kubwa kwenye kumfanya afurahi, yaani hata nikiwa nimekasirika kabisa lakini naweza kumuuliza maswali ambayo yatamfanya akatoka kwenye point ya msingi ya kujitetea na kuanza kucheka, halafu baada ya hapo namuuliza "kwa hiyo unanidharu sio?"

Baada ya muda kwenda akashtuka sasa kwamba ni yeye tu ndiyo huanza kunitext na kunikolu na hata hivyo nimebadilika pakubwa tunapoongea, aliponihoji kwa nipo hivyo nilijitetea vile ambavyo niliona itakuwa ni point huku moyoni nikisema "WEWE MJINGA USHANIONA MATAKO YAKO SASA YAANI HUNITAKI HALAFU BADO NIKUKENULIE MIDOMO MDA WOTE"
Kumbuka muda huu nilikuwa simgusii tena kuhusu mapenzi.


Baasi bwana... siku moja akanipigia ilikuwa ni usiku sana kama saa sita hivi.

Baada ya kusalimiana:

YEYE 'Kim, mimi ni msichana bado sio mtumzima lakini nina uwezo wakutambua mambo na kumwelewa mtu.

(mimi kimoyomoyo EENHEE..)

najua kwamba hauko sawa japo unajaribu kulificha hili, ni muda mrefu sasa ni mimi tu ndiyo nakutafuta kuanzia asubuhi mchana hadi usiku, najua hakuna binadamu anaweza kuwa bize kiasi hiki, sitaki nikufiche Kim nimekuwa wa tofauti sana tangu mimi na wewe tumejuana, nimekuwa ni mtu mwenye furaha muda wote, wewe pia nimekuzoea unakuwa ni mwenye furaha na sio kama ulivyo sasa.

Nimetafakari sana kwamba nini kitakuwa kinakusumbua lakini jibu nimepata ni ombi lako la mapenzi tu, nimewaza hivyo kwasababu ndani ya hii miezi michache umewahi kunishirikisha changamoto kadhaa, mimi pia nimekuamini na kukwambia mambo mengine pengine hakuna msiri wangu nimewahi kumwambia, kwahiyo kama ungekuwa na jambo lolote zaidi ya hili najua ungeniambia.

Kim unanisikia lakini?"

MIMI "ndiyo nakusikiliza"

YEYE "Sawa, Kim nikwambie tu ukweli mimi sijakukatalia ombi lako kama unavyo dhania lakini embu vuta picha ndiyo nimekukubalia, halafu baada ya kuonana ikawa mimi sijaridhika na wewe kimwonekano na umbo ama wewe ikawa hujaridhika na mimi ni nini kitakokea?

Kimsingi makubaliano yetu hayakuwa na maana yoyote, Kim kusema kweli kutoka moyoni mwangu karibia asilimia 99 nimekupenda kutokana na picha ninayo itengeza kwamba ndiyo upo lakini ni vipi sasa kama hautokuwa hivyo? hupaswi kuchukia, kikubwa ni tujadili tufanyeje kuhusu kuonana."

Kumbuka Kipindi hiki smartphone hazijamwagika kwa wingi mtaani kama ilivyo sasa (walokuwepo Mtwara kipindi hiko watanielewa) hapo kulikuwa na Itel flani kuubwa za kutachi zilikuwa na kava ambalo linafunika hadi kioo mtu akiwa na hiyo anavimba mtaani mzee, tena zilikuwa na kijiti cha kutachia 😂.

Kuhusu mtandao ni labda mtu uingie FB kwa kutumia kitochi ila yeye hakuwa na acount mimi pia.

Baasi bwana... nikamjibu ki-mikausho mikausho hivyo hivyo ila mwisho wa siku maneno yake nikaona yana point za msingi.
Tukajadili kuhusu kuonana nikamshawishi afunge safari kuja kwa babaake ila akasema itachelewa maana wazee wataingilia kati na kupanga wao muda wa yeye kuja huku.
Mwisho nikakubali nitakwenda kwao ili kuonana, huku nikimuwekea mkwara kwamba asiloridhika na mimi ananilipa nauli yangu.

Baada ya maongezi ya ule usiku mawasiliano yalirudi tena upya tena kwa kasi kiasi hata watu wa mtandao walikuwa wanajivunia kuwa na mteja mzuri wa vocha za buku buku kama mimi.

LAIMA akanipangilia mazingira yote kuhusu Newala, huku akinipangilia nyumba ya wageni ambayo nitafikia maana kwa siku ambayo aliipanga ningeweza kufika kwao mchana ila usiku wazazi wake watakuwepo hivyo hataki wajue ujio wangu.

Ingawaje nilimtaka na kumshauri nae aje katika hiyo guest house ambayo nitakuwepo lakini hakukubali kabisa kwa kigezo cha kuwa hatotaka kuona hapo kwani itajenga picha kwamba yeye ni malaya, nikaona sio kesi nitajua huko huko nitafanyaje.

Nilipoona safari inakaribia nikampangilia Deo mchongo wote ila akanilaumu sana kwamba nakubali vipi kwenda kwa demu, hata kama hatutalala pamoja lakini bado kwenda kwenye mji mgeni kwa ajili ya mwanamke halafu nilale huko huko ni kipengele, akasema ningefanya ninachokiweza demu ndiyo aje kwangu.

Baada ya kunilaumu sana mwisho tukashauriana kwamba tutakwenda wote lakini Laima asijue kwamba nitaenda na Deo.

Kwahiyo nitazuga kama nimefikis Gest kama Laima atakubali kuja Gest basi deo ataniungia Gest chapu, na kama hatokubali tutalala tu kwa kina Deo na asubuhi tutageuza.

Kumbuka deo ni mwenyeji wa newala alisoma primary huko wakati akiishi kwa bibi yake na ndiyo sababu anajuana na Laima ila hawaishi kata moja.

Pia akanishauri tuondoke kwa pikipiki ili tufike kwa wakati, japo tutatumia gharama kubwa lakini nitaturahisishia mizunguko.

Baasi bwana masiku yakaenda siku ya safari ikakaribia hadi machoni, na hatimae ikafika sasa.

Nilitaka kutupia viwalo vikali lakini Deo akaniambia vaa kawaida tu ila code zako za kuulia weka kwenye begi ukivaa sasa nguo kali utajilaumu, kwani sehemu nyingi za barabara ni kidongo chekundu.

Baasi bwana... mishale ya saa 1 asubuhi hiyo wahuni tukiwa katika sanlg tukaanza kuiaga mandhari ya Mtwara town taratiibu.. huku Deo ndiyo anakimbiza chuma mimi nikiwa nyuma na begi langu ambalo limeshiba nguo zetu na zawadi za Laima.

Hapo ni mwendo wa kuchati na mrembo tu vidole havipoi yani.

Japo mwanzo nilichukulia kama unyamwezi kuvaa lile begi mgongoni lakini baadae nilimuomba edo asimame ili tulifunge lile begi nyuma.

Edo alipeleka pikipiki pembeni ya barabara huku akisema "Hapo tu Nanyamba hatujafika"
Jamani kusafiri safari ndefu kwa pikipiki ni mateso.

Tulipofika Nanyamba tukanywa chai mgahawani safari nikaendelea.

Nilishangazwa na vingi njiani siwezi kueleza vyote ila kikubwa ni Mlima 'S' uliopo Nanyamba.

Wamakonde wanasema Time iz makangabiliti.
Muda ukafika na hatimae tukaingia Newala.

Ilikuwa ni mshale ya saa 3 na dakika kadhaa wahuni tunatimba katika wilaya hii yenye jina kubwa mkononi Mtwara na Tanzania kwa ujumla.

Macho yangu yalithibitisha moja kwa moja kile kinachosemwa na watu wengi kuhusu madhali ya Wilaya hii.

DEO "Ushampangilia Laima kwamba tumeingia?"

MIMI "Hapana"

DEO "We muache tu nataka nitenfeneze mazingira hadi atom.eke huyu malaya asitulee usen.e sisi hatuwezi kufunga safari yote hii halafu tukarudi bure, kwanza yeye ana uzuri gani wa kutaka akague wenzake muda sio mrefu tunaingia kwa bibi tukifika pale nitachakata akili tutafanyaje"

"Freshi mwanangu dah unanipambania!"

Tunafanana umri na Deo lakini linapokuja suala la Ugegedu mwenzangu amenitupa mbali kiasi, nikamwitikia huku nikijiwazia huyu kichaa asije kuharibu mazima nikashindwa kuonana na chidada wangu.

Tukafika kwa kina Deo na kuwakuta madogo nje, akawauliza kuhusu bibi yake wakasema ametoka atarudi jioni.

Muda huo mwili na nguo zetu zilikuwa zimewivia vumbi jekundu tukaoga na kujiweka sawa, muda huo sms za Laima zilikuwa zinamiminika tu Zile za 'my upo wapi sasa, mbona kimya wangu' na nyingine nyingi.



Muendelezo naweka sasa hivi leo nataka nimalize hiki kisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom