Niliamini ananipenda kumbe alinifanya kichekesho

Niliamini ananipenda kumbe alinifanya kichekesho

BAADA YA HII, SEHEMU INAYOFUATA NI YA MWISHO.

NILIPOISHIA

Baasi bwana asubuhi pakakucha deo akanifata tukaelekea kwao.

Nikamsimulia kila kilichojili, akacheka sana nilipomwambia sikugonga kisa dogo alikua kwenye masiku (sikumsimulia kwamba alisema nimkague).

Tukapiga zetu chai na kusubiri ifike saa nne niende kwa kina Laima ambae muda wote nachati nae kwenye simu.

ENDELEA

Muda ukafika Deo akashauri nipande chuma nyingine ili kwenda kwa kina Laima.

Nikaondoka na yeye kwa mguu hadi tulipotokomea mbali na pale kwao nikapanda bodaboda safari kwa kina Laima.

Nikafika maeneo ambayo laima alisema nishuke, ni barabarani pana mti mkubwa ambao sikujua ni mti gani.

Nikamtext Laima nimefika.
Baada ya muda mfupi nikamuona kwa mbaali akiwa anaendesha baiskeli ndogo.

Akanikaribia na kunifikia kabisa.

Alikuwa amevaa gauni huku kichwa kikiwa wazi, nilipata muda wa kumkagua vizuri zaidi Laima, kilichonishangaza zaidi ni umbo lake yaani ana makalio makubwa mno, unaweza kudhani ni mtu mwingine ambae jana sikuwa nae chumbani.

Tukaanza kutembea mdogo mdogo kuelekea nyumbani kwao, nilishangaa kuona anafungua geti katika fensi ambayo imejitenga kidogo na makazi mengine.

"Mme wangu karibu nyumbani"

MIMI "Asante"
Niliitikia huku nikijitahidi kuangalia kwa udadisi maeneo haya, japo nilijitahidi kuficha hisia ili Laima asistuke.

'Mbona kama anaenda kuniuza huyu dogo'

Nilijiwazia huku tukiingia ndani kwa kina Laima.

Ulikuwa ni mjengo mkubwa mno, japo nimeona mijengo mikubwa kama hii huku Newala lakini sikuwahi kufikiria kwamba Laima anaweza kuwa anaishi katika mjengo mkubwa na wa kisasa kiasi hiki.

Laima aliwahi kunambia kwamba baba yake ni mkulima na mfanya biashara ya mazao lakini hata hivyo bado nilikuwa najiwazia itakuwa ana uwekezaji mkubwa kiasi gani.

Tukaingia ndani ya fensi, yeye akaingia ndani ili kuchukuwa viti.

Nikatuma meseji kwa Deo haraka sana kumuuliza juu ya nyumba ya kina Laima.

Deo akatuma mejeji ya kicheko kirefu sana na mwisho kuandika 'sikukupanga kwani? Ndiyo kwa wakwe zako hapo mjomba kula maisha'

Nilicheka kidogo na kujikausha huku nikimsubiri Laima

'Hivi ndiyo paaap babake Laima anatokea pale getini nitafanyaje'

Nilijiwazia hiku nikitazama uzio huu mrefu uliojengwa kwa tofali.

Laima akaleta viti tukakaa.

Tukaanza kugonga stori huku moyoni nikiwa sijiamini kabisa.

"Kim ngoja nikalete chai"

Akainuka na kwenda ndani. michakato ya Laima kuja na kuondoka ilikuwa inanipa burudani mno kwa kuuangalia mzigo wake ambao unatetemeka kizembe japo amevalia gauni la heshima.

Akarudi na kijimeza cha plastiki chupa ya chai na sahani limejaa mazaga zaga hadi nikashangaa.
Akaingia tena ndani na kutoka na bakuli kubwa vikombe na jagi.

"Kim karibu chai mimi nishakula muda tu"

MIMI "Kwahiyo Hivi vitafunwa vyote umeeka kwa ajili yangu tu, umesikia mimi full tenki?"

Alicheka huku akiushika mkono wangu wa kulia na kuninawisha.

YEYE "Wewe nikikusikiliza utanipasua mbavu zangu"
Nikaanza kupambana na vitafunwa hivi vya aina tofauti tofauti huku tukigonga stori na kucheka.

Kidogo geti likafunguliwa Wakaingia madogo wawili wakiume wakiwa wamebeba ndoo ndogo, wakampa Laima akafungua na kuangalia ndani, japo sikuona kilichomo lakini harufu tu niliyoipata ilinijulisha kwenye ndoo kuna korosho zilizochomwa na kutolewa maganda.
Laima akawapa elfu moja wale madogo wakaondoka.

Kidogo akaingia mdada mmoja mwembamba kimo cha wastani, akatusalimia na kuingia ndani akarudi na stuli na kuketi tulipo.

Laima akanitambulisha kwamba yule dada anaitwa Aisha ni rafikiyake, yeye pia akamtambulisha jina langu na kumwambia ni shemeji yake naishi Mtwara town.

Tukapiga stori na Aisha hadi muda wangu wa kutoka ukawadia.
Laima akanifungia korosho kwenye mfuko wa msala msala, akanisindikiza hadi Umbali kidogo kutoka ilipo nyumba yao, tukaagana kisha nikapanda pikipiki na kurudi kwa kina Deo.

Tukaweka kila kitu sawa na hatimae mida ya saa sita tukaanza safari kurudi nyumbani.

Njiani ilikuwa ni mwendo wa korosho na juisi tu.

Hadi saa 9 alasiri tukaingia Mtwara mjini.

Deo akaniacha magetoni kwangu Mtaani Reluwe yeye akaondoka na pikipiki.

Mawasiliano yetu yalizidi kunoga huku tukiendelea kuaminishana mambo kibao ambayo kama tungeyatekeleza, inawezekana Maisha yangu yangekuwa ya furaha zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.

Changamoto ilikuwa katika jambo moja tu na ndiyo baada ya muda kwenda lilifanya nishtuke kwamba Laima hakuwa ananipenda kweli kama anavyotamka mdomoni pake. Kipengele ili kuwa ni kukutana kimwili, Laima alijitahidi kadiri awezavyo kukwepesha suala zima la sisi kukutana kimwili.

Hili nilikuja kulijua baada ya kama mwaka na miezi kadhaa kupita tukiwa wapenzi na miaka miwili tangu kufahamiana kwetu.

Tuliwahi kupanga mara nyingi tu yeye aje huku mtwara alifelisha.
Lakini pia tulipanga mara nyingi tu mimi niende tena Newala lakini kila siku tulizopanga zilipo karibia Laima alileta sababu zilizofanya tusogeze safari mbele.

Japo tulikuwa tukionana alipokuwa akija huku Mtwara kwa dharura kama vile kumwona mgonjwa na dharura nyingine ambazo zingempa sababu ya kukwepa kufika nyumbani ama katika mazingira ambayo yangeweza kutukutanisha kimwili.

Katika kipindi chetu chote cha mahusiano Laima hakuwa akiniomba pesa kabisa ni mara moja moja sana ambapo nilikuwa nikimtumia pesa, tena ni maamuzi yangu tu kulinda brand lakini hakuwa akiniomba hela.

Hii pia imeniachia somo hadi leo, kama mwanamke haniombi hela huwa naamini siko mwenyewe tu kuna wenzangu ambao ndio wanaombwa, haijalishi ana kazi ama kipato gani.

Hadi moyo unakuja kukubaliana na ukweli kwamba huyu mtu hanipendi nilikuwa nishaathirika pakubwa sana. Nilikuwa nimekwisha jenga picha kwamba huyu ni mke wangu mtarajiwa.
Nilikuwa namchukulia Laima kama mwanamke ambae atakuwa Mama wa wanangu.
nilikuwa nimeshazama katika bahari ya mapenzi kiasi cha kuwa kujinasua ni kazi ngumu mno.

Nilianza kwa mbinu ya kulalamika kuhusu kitu ninachokiona katika mapenzi yetu, japo Laima alinipa maneno ya faraja lakini bado kipengele ilikuwa ni kile kile.

Ilikuwa inanikata sana kuona ninampenzi lakini hataki tukutane kimwili, nilikuwa naona wazi Laima hanipendi kutoka moyoni, nilikuwa najua kwamba duniani hakuna mapenzi ya namna ile, lakini changamoto ilikuwa ni kujinasua kwenye mtego wake ambao sikujua ameutega kwaajili gani.

Nikaanza zoezi la kukaa kimya, yaani simtafuti akinitafuta sipokei wala sijibu meseji.

Haikuwa kazi rahisi kama ambavyo nilidhania, hata kabla ya wiki nilianza kupokea simu zake na kurudisha mawasiliano kama kawaida.

Baada ya muda flani nikamchana kwamba nahitaji tuachane na sababu ni hiyo kwamba nimeshindwa kuwa mtumwa wa penzi kivuli.

Aliitikia lakini akisema yeye hana tatizo na mimi kama mimi naona hivyo ni sawa.

Nilifuta namba zake na kuendelea na maisha, nilitoboa kama mwezi tu tena kwa tabu sana nilijikuta nashindwa na kumpigia kwani namba zake zilikuwa kichwani mwangu.

Nilipompigia alipokea na kunicheka sana akiniambia alijuwa tu nisingeweza kutoboa maana anajuwa ninampenda sana yeye pia ananipenda lakini kila kitu kina muda na kwamba mimi nina haraka.

Majibu yake yalionesha kutokuwa na mabadiliko kabisa.

Nilijaribu tena na tena kumuacha lakini nilishindwa na kikubwa ilikuwa ni namba zake zilikuwa kichwani hivyo hata nilipobadilisha namba ili yeye asinipate nilijikuta namtafuta mwenyewe na kuanza mawasiliano.

Kuna muda niliwahi kumpigia na kumuomba anitajie kiasi chochote kile cha pesa, ama akishindwa kutaja nimtumie kiasi kisichopungua laki moja ili abadilishe namba yake kwa ajili ya kuninusuru kijana mwenzake katika ule uwendawazimu ambao nilikuwa nao wakati ule.
Alikataa na kusema hangeweza kufanya hivyo kwani yeye bado ananihitaji na anajua kuna muda sahihi utafika.

Nilipoona njia hii imefeli nikamwomba tu aibloku namba yangu hadi huo muda ambao yeye anauna ni sahihi, na hata nikimpigia kwa namba ngeni akijuwa ni mimi akate simu, hii hakukubali pia.

Nyie, mnapoambiwa mapenzi ni uchizi tambueni ni uchizi hasa, sana sana yale mapenzi ya mwanzo mwanzo kabla hujapigwa matukio mengi.

Nilipoona ombi la kunibloku hajalikubali nikaona Hapana, huyu ataniblock kwa lazima. Nikawa nanunua sms za mwezi kipindi kile ilikuwa elfu moja unapata sms 10,000.

Nilichokuwa nafanya ni kuingia sehemu ya meseji na kuitafuta meseji yake moja kisha naenda reply hapo nakuwa na kazi ya kubonyeza batani moja tu ile ya juu kushoto.
Hapo ni kwamba nareply meseji hewa bila kikomo kwenda kwenye namba yake.
Yaani ilikuwa kutwa nzima nafanya shughuli zangu huku nina reply tu.

Nilitumia hii mbinu kwa sababu kwenye kitochi huwezi kufanya chochote huku meseji nikiingia mfululizo, yaani hupigi huchati wala hufanyi matumizi yoyote ya simu maana kila utakachohitaji kufanya ukija katika uwanja wa nyumbani inaingia meseji, ukisema ukate urudi tena ni hivyo hivyo (sijuwi kwa vitochi vya sasa lakini)

Siku ya kwanza alituma meseji kadhaa usiku sana nikiwa nimelala, nilipoamka nikaifungua moja katikameseji hizo ilikuwa inasema 'vipi kwani mbona unatuma sms nyingi hewa hadi simu yangu inaganda?'

Mimi nikamjibu 'block namba yangu'
Kisha nikaanza kuzitiririsha tena sms hewa zisizo na idadi. Ilikuwa betri moja naweka kwenye kobe lingine kwenye simu kazi yangu ni moja tu, tangu nikiamka hadi ninapolala, yaani hata kama niko kitaa napiga miradi kazi yangu ni kubonyeza tu ile batani.

Hii vita ilikuwa ngumu upande wangu kwani pamoja na yote hayo Laima hakublock namba yangu, lakini nikasema atachoka tu na mwisho atanibloku mwenyewe.

Siku moja asubuhi nikiwa home nikapokea simu kwa mdada ambae alijitambulisha ni Aisha rafiki yake Laima, Kumbuka ni zaidi ya mwaka na nusu tangu nionane na Aisha kule kwa kina Laima.

SEHEMU INAYOFUATA NI YA MWISHO.

Mwaka ikitokea nimekutana na huyo dada (Laima wetu feki) na kumwonyesha hiki kisa, pengine atacheka sana ama pengine atadondosha machozi kwa kukumbuka mbali maana haya yote niliyoandika humu ni ya kweli.

Namba ya huyu dada haijawahi kufutika kichwani mwangu hadi leo.
Na tangu hapo sijawahi kuhifadhi tena namba ya mwanamke kichwani hadi leo, hata mwanamke ambae niliwahi kumwoa sikuwahi kuhifadhi namba yake kichwani.

Tukutane sehemu ya mwisho.
Katika kitu ambacho mshukuru sana mwenyezi Mungu ni kutokuww na mwanamke hyu ktk maisha yako huyu ni mwanamke hatar sana, ukiskia mwanamke anajua mwanamke wenzake kaolewa tena ana watoto halaf asababishe mwanaume amwache ili aolewe yeye aisee ogopa sana, huyo ni nyoka ktk maisha ni aina ya watu ambao hajali utaumia kiasi gani bora anachohtaji yeye amekipata,asui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake na adui wa mwanaume ni mwanaume mwenzake.
 
Katika kitu ambacho mshukuru sana mwenyezi Mungu ni kutokuww na mwanamke hyu ktk maisha yako huyu ni mwanamke hatar sana, ukiskia mwanamke anajua mwanamke wenzake kaolewa tena ana watoto halaf asababishe mwanaume amwache ili aolewe yeye aisee ogopa sana, huyo ni nyoka ktk maisha ni aina ya watu ambao hajali utaumia kiasi gani bora anachohtaji yeye amekipata,asui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake na adui wa mwanaume ni mwanaume mwenzake.
Asante kwa kushea nami maono yako mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom