Niliacha chuo ili nifanye biashara, sasa mtaji umekatika sijui nifanye nini?

Dogo cha kwanza biashara lazima uwe na maleng. Pili, kama mtaji umekata tafuta kazi inayoendana na mtaji ulionao. Hapo ungekuwa upo mkoa Mwanza ningekwambia biashara moja inayolipa huku na mtaji wake ni chini ya 30k afu unafanya masaa labda 6 tu unaondoka na 10000 yako au zaidi.

Vijana kazi zipo nyingi mno ila shida tunazionea aibu. Lakini kingine kama hujawahi kufanya biashara jaribu kuulizia kwanza, wewe ulifikiri huwezi kuuza nguo huku unasoma? Mbona wengine tunafanya umachinga na chuo hatuachi? Dogo fanya maamuzi sasa
 
Binadamu hashindwi kitu jamaa, fanya hata udalali. Nenda Bagamoyo kule watu hawajasoma ukawape shule. Vijijini hapo pwani kuna malofa kibao, nenda kawapige. Unaeza ukaopoa hata mtumishi akawa anakulisha huku unatafuta mdogo mdogo
 
Mkuu pole usikate tamaa ndio mitihani ya Dunia.Yaani hapo ulipofikia ndio maisha halisi ya ujasiriamali yanaanza.
Msingi anza na connection ya karibu then angalia biashara yenye mtaji kidogo pambana nayo.
Nenda hata kkoo ongea na chinga wanaotandika vitu ujifunze mdogo mdogo.cha msingi katika kipindi hiki usiwe mwoga.
Ni kawaida binadamu unapochukua abnormal decisions kukuhukumu so usikate tamaa.
You are the champion.Mateso,dharau, kudondoka na mafanikio yanakungoja genius.msingi komaa
Mkuu unajua bei ya kupata nafasi ya kutandika vitu pale kariakoo? Sio mchezo
 
Umefika ile hatua ya kujiuliza kwanini nobody can stop reaggae... pole sana mkuu...
 
Binadamu hashindwi kitu jamaa, fanya hata udalali. Nenda Bagamoyo kule watu hawajasoma ukawape shule. Vijijini hapo pwani kuna malofa kibao, nenda kawapige. Unaeza ukaopoa hata mtumishi akawa anakulisha huku unatafuta mdogo mdogo
😂😂😂😂😂 we jamaa mjanja kweliii!!
 
Naona wengi wakiku tukana hapa jukwaani, wakikashifu hasa kuhusu suala la shule sijui una sup 4, sijui ni kilaza, sijui hujui biashara na vyote hivi.

Mkuu hata biashara ukizingatia huwezi kulala njaa, fanya biashara ya kuchuhuza kwanza upate nguvu ya kurudi au relief.
Changamoto kama hizi hupitii wewe tu hata mimi napitia sana, simama tu kwenye line jiamini na biashara ipo siku.

wengi hapa wanaongea shule shule shule umeacha university umeacha university sijui serikali inakupa boom hayo yote ni makwazo unawekewa tu ili uone umeshashindwa lakini sio kweli pambana bado.
 
namba ya simu iko wapi upate michongo..
Naanza kwa kuwasalimu ndugu zangu wa JF,

Moja kwa moja niende kwenye mada, mimi ni kijana umri wa miaka 21, nilimalza A-LEVEL mwaka jana na nikachaguliwa kujiunga chuo.

Ingawaje nilikidhi vigezo ila sikuweza kuchaguliwa kozi niliyoitaka. Kutokana na umasikini na ufukara ulioikumba familia yangu ilinilazimu nikasome kozi hiyo hiyo, hivyo maisha yangu ya chuo sikuwah kuwa na furaha kutokana na kusoma kitu ambacho sikipendi hali iliyopelekea kupata supplementary kozi nne kati ya saba kwa muhula wa kwanza.

Hali hiyo ilinikatisha tamaa na kuamua kuchukua maamuzi magumu ya kuacha chuo, na kujiingiza kwenye ujasiriamali hela ya mwisho ya kujikimu tulipopewa ilinilazimu niondoke nalo na kuanza maisha mapya Jijini Dar. Nilitafuta sehemu mtaani nikalipa pango la miezi mitatu na kuanza biashara ya kuuza mtumba.

Hadi sasa nimepoteza mtaji na sijui nini la kufanya na hadi dakika hii, mama kjijini anajua niko chuoni nasoma nikamkomboe kwenye umasikini.

Kwa hiyo ninachoomba kweli wapendwa dada na kakazangu, kama kuna mtu yeyote anaweza kunipa kazi ya kufanya niko tayari maana hapa pango limeisha na sina hela ya kulipa tena pango. Nawaz nirudi kjijini ila sijui ntamweleza nini mama akanielewa.

Pia, kama kuna mfadhili yuko tayari kunisomesha tuandikiane mkataba nimlipe nikipata kazi kwa riba ile ile ya Bodi ya mikopo maana kule siwezi kukopesheka tena mpaka nilipe kiasi fulani nitashukuru.

Ahsante.
 
Hukutakiwa kuacha masomo wewe kijana...

Hela uliyolipwa na serikali ungevumilia na kuikusanya kidogo kidogo hadi unamaliza chuo ungekuwa na mtaji na wazo thabiti...

Ushauri kwa sasa, tafuta namna ya kurejea chuo
 
Usirudi chuo, usirudi chuo na usirudi chuo
Hukua na wazo baya ila ulikua na mategemeo mabaya, kwahiyo we jitathmini upya uanze kazi, usirudi chuo.
 
Dont be defeated by a temporary defeat......Kaka hayo ni ya muda tu.....kubali tu kwamba kwa sasa unapitia kipindi kigumu,usikubali kuwa umeshindwa kwa sababu umepitia kikwazo cha muda.....pambana mkuu......pambana boss wang najua mwanga upo mbele.......ukiwa unajifunza kuendesha baiskeli mara ya kwanza lzm utaanguka,utaumia,marafiki zako watakucheka na kukukebehi lkn kesho utakuwa more determinant usianguke tena,na utakapoweza kuendesha nakuhakikishishia utaendesha hata bila kufikiria na ikitokea umeanguka utajua ni vipi na kwanini umeanguka so haitakupa shida kusahihisha kosa lako.......keep going dont quit!
 
Back
Top Bottom